Maendeleo kama haya hatuwezi kuyapata nchi yetu hii?

Mwalimu Nyerere alituachia kauli mbiu ambayo nafikiri mpaka leo bado ina logic, alisema "ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE, ARDHI, WATU SIASA SAFI NA UONGOZI BORA". Ukitazama wote wenye maendeleo wanapitia katika misingi hii hii aliyoisema Nyerere, China moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa sana kimaendeleo katika muda mfupi ukiwa kiongozi na ukavunja maadili ya uongozi jua shaba unakusubiri. Kwa nini wasiendelee, sisi ndio kwanza utapewa heshima kubwa, ajabu!!!!!!!!!!.
 
Maendeleo kama haya hatutayapata ng`o,kama tutaendelea na tabia yetu ya kutegemea misaada na mikopo ya wahisani.Wenzetu wameyapata yote haya kutokana na kufanya kazi kwa bidii,kuziba mianya ya rushwa na uwajibikaji uliotukuka maana kwa mchina akikupa jukumu ukashindwa kufikia lengo adhabu yake ni kifo.Sasa sisi kila leo tunashindwa hata kufikia nusu ya malengo yetu, maendeleo kama haya tutayapata lini .Kama tumeshindwa kumshinda mbu tu yule aenezaye malaria,tutayaweza haya?Acha nikajinywee valuu zangu mie..
 
Maendeleo kama haya tunaweza kuyapata kama tukithubutu zaidi. hapa ninamaanisha kwamba tungeanza na mambo ya msingi kwanza kabla ya kukimbilia vitu vya namna hiyo, tunapenda sana kuishi maisha ya hali ya juu kuliko uwezo wetu na ndio maana matokeo huwa sio mazuri katika mpango mzima wa maendeleo, hebu chukulia mfano Jiji la Dar es salaam kwa sasa kuna ujenzi wa maghorofa unaendelea kila kona , lakini ukianga lia miundombinu unaozunguka haya majengo ni ovyo kabisa, barabara ni Finyu na zenye mashimo kila pembe, najua mahitaji yataongezeka huko mbeleni na hapo itabidi tuanze kuyaporomosha tena hayo majengo ili kupanua barabara, hapa tunasonga ama tunarudi nyuma?

Kitu kingine ni kwamba pesa na utajiri tunao, lakini Mipango na utekelezaji tuko nyuma kabisa, wenzetu wako makini sana katika kutekeleza mambo ya muhimu kwanza. Hebu chukulia ni miradi mingapi imecheleweshwe kulingana na timeline? chukulia mfano Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi!! mpaka leo hii wazungu wanajua makao makuu ya Tanzania yapo Dar es salaam. cha muhimu hapa ni kwamba hatuwezi kuchukua maamuzi magumu ndio maana tuko katika umaskini huu wa kutisha.
 
Mwalimu Nyerere alituachia kauli mbiu ambayo nafikiri mpaka leo bado ina logic, alisema "ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE, ARDHI, WATU SIASA SAFI NA UONGOZI BORA". Ukitazama wote wenye maendeleo wanapitia katika misingi hii hii aliyoisema Nyerere, China moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa sana kimaendeleo katika muda mfupi ukiwa kiongozi na ukavunja maadili ya uongozi jua shaba unakusubiri. Kwa nini wasiendelee, sisi ndio kwanza utapewa heshima kubwa, ajabu!!!!!!!!!!.
"ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE, ARDHI, WATU SIASA SAFI NA UONGOZI BORA". ( SIASA SAFI NA UONGOZI BORA) Je Vitu hivi Vipo hapo kwetu Tanzania?
 
Ili kujua kama unaendelea inabidi ujue maendeleo ni nini???

Kama hujui maendeleo ni nini? Basi chochote unachofikiri kuwa ni Maendeleo basi utaamini kuwa ni Maendeleo hata kama ni kukimbia kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu!

Kabla hujamlaumu kiongozi uliyemchagua kwa nidhamu yako ya woga..kwanza Jilaumu wewe mwenyewe kwa kushindwa kutumia haki yako na pia kuendelea kulalamika kwa maneno matupu...

.................... Karaghabaho!..........
 
Lawama si kwa serikali na viongozi peke yao. Watu binafsi wanstahili lawama pia. Ni kweli kuna wizi na ufisadi kila mahali kuanzia kwa wadogo mpaka kwa vigogo. Je, hizo pesa zinazoibiwa zingekuwa zinawekezwa katika maendeleo ya maana kama kujenga viwanda (vidogo mpaka vikubwa), kuanzisha mashamaba ya kisasa, karakana za kufua vyuma, tafiti mbali mbali, n.k. Je, hata bila ya serikali si tusingeona maendeleo? Badala yake tunajenga mijumba mikubwa ambayo haifikiki kwa ukosefu wa barabara, haina maji wala umeme; tunaendesha sherehe za gharama kubwa kwa ajili ya sifa; tunavaa mavazi aghali kutoka kwa wengine; tunapenda starehe kuliko kazi; hatuthamini ushauri wa kitaalamu; .................... Mimi nasema DEVELOPMENT STARTS WITH YOU. Kama huna mawazo ya kimaendeleo serikali au viongozi hawawezi kukuendeleza.
 
............... tunapenda starehe kuliko kazi; hatuthamini ushauri wa kitaalamu; .................... Mimi nasema DEVELOPMENT STARTS WITH YOU. Kama huna mawazo ya kimaendeleo serikali au viongozi hawawezi kukuendeleza.

..... +1
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom