Maendeleo kama haya hatuwezi kuyapata nchi yetu hii?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,941
5,884
Mbona tumekwisha yapata - mabasi yaendayo kasi tayari yapo kuanzia mwenzi wa kumi; ujenzi wa reli Ubungo - Tegeta upo kwenye hatua za mwisho, flyovers tayari nne zimekwisha kamailika - pale Ubungo, Tazara, Morocco na Magomeni mapipa!!!!!!!!!!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,364
Watu wenye roho mbaya na fikra finyu yao ni mateso ya hapa duniani awali kabla ya yote.

Hivi kila siku kunusa vikwapa vya wenzio si mateso ni nini?

Hivi kila siku kusikiliza mashuzi ya mwenzio wa nyumba chumba cha pili kwa kukosa hata mpangilio wa kujega kama si mateso ni nini?

Hivi kila kukicha wewe ukiamka roho inakuuma kwa nini mwenzako anacho wewe hauna na kufikiri kuwa huyu lazima kaiba tu. Kama si mateso hayo ni nini?

Hivi kuwafundisha watu kila siku kuwa jamani msitupe taka hovyo, zitunzeni taka zenu vizuri na watu wanaendelea kutupa taka hovyo, kama si mateso ni nini?

Hivi kila kukicha watu wakiamka, wakilala, wakiamaka wanafikiria leo tumpachike kosa lipi Kikwete kama si mateso haya ni nini?

Hivi kila huduma unayostahili kupewa hata ya kuagiza soda kwa pesa zako mwenyewe mpaka uiombe na yule anaekuletea amekufanyia favor. Kama si mateso haya ni nini?

Matatizo ya Tanzania tunajitakia Watanzania wenyewe badala kuona fulani kafanya na mimi nifanye zaidi yake (progressive competition). Sisi tunaona ngoja nifanye na yeye akose kabisa kwani tunaona ni bora tukikosa wote. Kuna cha kuendelea hapo?
 
Good Guy

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
3,806
1,384
FF wewe ndo naona fikra zako ni finyu! Kauliza kwa hoja jibu kwa hoja.Wivu wa maendeleo unaita 'kuskiliza mashuzi ya wenzako' bila kutamani kwa mwenzake mwanafunzi wa mwisho darasani angebaki wa mwisho. Najua unatetea serikali ya JK(cjui kwa malipo au vp) ila panapofika kukubali kua katika maendeleo kuna uzembe umefanyika,hii ni kutokana na ufisadi na rushwa zilizokithiri. Mfano katika secta ya umeme.Matatizo ya umeme,maswala ya Richmond na Dowans nayo ni masuala ya 'kuamka na kulala na kumpachika JK?' Afu kwenye taka,hivi wewe unaweza ukanunua mua mjini ukala ukatunza maganda mpaka kwenye dampo eti ndo utupe,yaani uko mjin uweke taka mfukon mpaka dampo. Serikali ya mitaa pamoja na jiji ni wajibu wao kujenga bins throughout the city. Angalia wenze2 walioendelea kila anapopita kuna bin kwanini atupe taka chini? Tafadhal kama unapinga pinga kwa hoja,sio marumbano.Tanx
 
Malunde

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
341
88

Sisi bado tunagombea Mi Daladala Ubungo Kariakoo

Uwezekano wa kuyapata upo, lakini si kwa lelemama hii tunayoenda nayo. Nidhamu yetu katika kazi ni ndogo na hatuna viongozi wenye vision ya kutuongoza kuelekea huko waliko wenzetu. Mzee Kibaki hapo jirani anafanya mambo mazuri kwenye barabara mpaka inatia wivu.Rwanda hawana muda mrefu toka mapigano yao ya 1994 lakini kasi yao ya maendeleo kwa sasa ni kubwa mno. We need to radically do something, otherwise, we will always be lagging behind.
 
Last edited by a moderator:

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,858
30,259

you have good idea thank you.
 
Barraza

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
481
270
hatutayafikia kwa sababu ya watu wasiojiamini kama wewe, kwa nini useme hatuwezi?
 
Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,858
30,259
hatutayafikia kwa sababu ya watu wasiojiamini kama wewe, kwa nini useme hatuwezi?
kama wewe unavyowachagua viongozi mafisadi, mimi nimeuliza Swali sasa wewe unanifananisha na viongozi wako,hii nchi hatutaweza kufikia hayo maendeleo ya wenzetu wa ulaya hata baada ya miaka 1000 ijayo hata wewe upate wajukuu hali itakuwa hivyo hivyo kama jana hakuna Maendeleo yoyote yale njaa tupu umeme hakuna maji masafi hakuna.
 
Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,858
30,259
Mbona tumekwisha yapata - mabasi yaendayo kasi tayari yapo kuanzia mwenzi wa kumi; ujenzi wa reli Ubungo - Tegeta upo kwenye hatua za mwisho, flyovers tayari nne zimekwisha kamailika - pale Ubungo, Tazara, Morocco na Magomeni mapipa!!!!!!!!!!
Basi ndizo hizo huku kuna hizo flyovers zinapita hata zaidi 20 kila sehemu zipo huwezi kuzihisabu. Treni bus na (Tram Vay) zipo kila sehemu huko nyumbani bado tunagombea Ma Daladala? Kweli maendeleo yatakuwepo hapo kwetu?
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,364
Hakuna maendeleo wakati bado kuna wachawi na roho za kichawi, saa ngapi mtawanga na saa ngapi mtafikiria maendeleo?
 
Shakazulu

JF-Expert Member
Feb 23, 2007
956
280
Hakuna maendeleo wakati bado kuna wachawi na roho za kichawi, saa ngapi mtawanga na saa ngapi mtafikiria maendeleo?

Sema tu ukweli acha kuzunguka mbuyu. Hakuna maendeleo wakati bado kuna watu wanafikiria wafanye nini ili wapate kupewa "zawadi" za nguo?
 
Mar 9, 2011
89
17
Maendeleo kama haya yanaweza kufikiwa na nchi yeyote inategemea malengo na mikakati ya kufikia malengo hayo, utekelezaji wa mipango na dhamira na utashi wa wasimamizi wa mipango iliyowekwa. Serikali nyingi na hasa za ulaya zimefikia hatua hiyo baada ya kubanwa na mahitaji na matatizo ambayo viongozi wao huketi na kufanya maamuzi ambayo wataalamu huwezeshwa na kuipangia mipango ya utekelezaji. bahati mbaya sana sisi hufanya mambo yetu ili mradi. Tumetanguliza sana ubinafsi badala ya maslahi ya umma. wizi na ufisadi ni masula ya kujisifia badala ya kuonea haya.Viongozi na wananchi kwa ujumla hawachukii vitendo vinavyotuletea madhara badala yake tunashabikia na kuwasifu. magari makubwa, nyumba nzuri, anasa bila kuangalia vyanzo vya mapato vya wahusika hii ndo hulka ya watanzania. Bila kubadilika itatuchukaa muda mrefu lakini tukidhamiria hatuhitaji zaidi ya miaka 50
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,857
8,673
FF,
It is unbelivable mpaka leo we work basing on the witch doctors directives. We have taken the guys with no idea of how to run things in the large scale to become our economic, social and political advisors. Wengine mpaka leo hii pamoja na kupewa dhamana kubwa kabisa, wanaendelea kulipia waganga wa klabu zao za soka mpaka leo? Shame on us!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,364
FF,
It is unbelivable mpaka leo we work basing on the witch doctors directives. We have taken the guys with no idea of how to run things in the large scale to become our economic, social and political advisors. Wengine mpaka leo hii pamoja na kupewa dhamana kubwa kabisa, wanaendelea kulipia waganga wa klabu zao za soka mpaka leo? Shame on us!

Exactly. And remember it is imperative, none is better than the other. Simply, when you see peoples talk about peoples rather than talking about ideas, be it well known, there is something very wrong in a large scale.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom