Maendeleo hayana chama/Twende na Samia

Mzee makoti

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
2,569
3,051
Wakuu bwana hawe nanyi:

Kiukweli Rais Samia hangeruhusu mchakato wa katiba mpya ufanyike, kwa Hali tuliyopitia kipindi Cha Rais aliyepita, ilikuwa ni kutokana na madhaifu ya katiba iliyopo na Ngosha alitumia madhaifu ya katiba ya sasa kufanya baadhi ya mahamuzi kwa utashi wake, mengine hayakuwa mahamuzi sahihi,hila yaliyopita sindwele, marehemu apumzike.

Nashauri Itengenezwe katiba mpya ambayo itakidhi vigezo, na ianze kutumika mwaka 2025, na wakati huo itahesabika Rais wa sasa hii awamu anayoendanayo aliyompokea Rais Magufuli , haitohesabika kwenye katiba mpya,Bali itakuwa imezikwa rasmi,

Bali itakapoanza kutumika katiba mpya 2025 ndio itahesabika awamu yake ya Kwanza Rais Samia ambayo itakuwa ya vipindi vitatu kwa mujibu wa katiba mpya, kwaiyo ataongoza Hadi 2040 akamilishe awamu tatu zake ,
Baada ya hapo utafuata uchaguzi mwingine.

kiukweli vipindi viwili ni vichache mno kwa Rais kukamilisha mipango madhubuti ya kuivusha Nchi, na hili hata wafuasi wa Rais aliyepita kina Pascal Mayalla walipendekeza Sana kipindi kile Cha Rais wa awamu ya Tano kuwa apewe muda zaidi kuiletea Nchi maendeleo,

Maendeleo hayana chama/ Urais awamu Tatu

Mungu ibariki Tanzania, mbariki Rais wetu na team yake
 
Back
Top Bottom