Maendeleo hayana chama; Rais Magufuli amjibu vibaya mwananchi aliyeelezea tatizo la maji jimbo la Momba(CHADEMA)

Kama kweli ameyasema hayo, kuna haja ya kufanya uchunguzi. Lazima.kuna kitu kitakuwa hakipo sawa kichwani mwake.
 
WANANCHI 'TWITANI' WASHANGAZWA NA JPM 'KUMSHUSHUA' MWANAMKE ALIYEMUOMBA MAJI.

Akiwa njiani kutoka mkoani Songwe kuelekea mkoani Rukwa, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amenukuliwa akimjibu mwanamke aliyemuomba maji kuwa akamuombe mumewe, diwani au mbunge aliyemchagua.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo mara baada ya kusimamishwa na wananchi waliotaka kufikisha kilio cha tatizo la maji katika eneo lao, ambalo ni sehemu ya jimbo la Momba linalokaliwa na Mbunge wa upinzani kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Silinde.

"Baba tusaidie maji" ilisikika sauti ya mwanamke mmoja kutoka kwenye umati mkubwa wa watu waliokuwa wamezingira gari la Rais Magufuli.

Akijibu ombi la mwanamke huyo, Rais Magufuli alimwambia kuwa, "Wewe acha kiherehere, mpelekee mume wako. We subiri. Mtoe huyo mama. Nimesimama hapa, nyinyi ndugu zangu. Sasa huyu anaanza kupiga kelele si akampigie mume wake. Sasa ndio mnataka mnilaumu mie. Kwahiyo huyu mama akamuombe huyo diwani wake pamoja na mbunge wake ambaye amempigia kura. Saa nyingine muwe mnajifunza,"

Kauli hiyo imeibua hisia tofauti kwa wananchi hususani wanaotumia mitandao ya kijamii kuhusu kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo ambaye ni mkuu wa nchi.

Wananchi wengi katika mtandao wa Twitter wameonekana kushtushwa na kauli ya Rais Magufuli kwakuwa mara kadhaa amekaririwa akisema kuwa maendeleo hayana chama na kila anachokifanya kinalenga kuwanufaisha wananchi wote.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Aneth Stanley (@AnethStanley) amesema kuwa Rais Magufuli ana tabia ya chuki za wazi sana.

"Wewe ni Rais wa taifa letu lakini cha ajabu bado hujiamini. Unahisi kwamba uko kwenye kampeni tu. Rudisha taifa letu kwenye misingi ya demokrasia. Kwa kauli hii utakuja kutugawa kikabila mpaka kidini pia," ameandika Aneth.

Nae Martin M. M (@IAMartin) ameandika kuwa, "Rais Magufuli kiongozi wa nchi, mbaguzi wa maendeleo kwa itikadi za kisiasa,"

Goodluck Haule (@Goodluck_Gbless) ameandika kuwa, "Rais hapaswi kufuata itikadi za kichama au kubagua wananchi kutokana na itikadi za kichama."

Kenneth Mwageni (@KennethMwageni4) ameandika kuwa, "Kesho utasikia maendeleo hayana chama. Wanasahau kuwa hayo maendeleo yanaletwa na walipa kodi. Na hao ndio wananchi ambao leo mnawabagua kesho mtawaomba walipe kodi. Serikali inapoleta maendeleo kwa wananchi sio hisani ni jukumu lake na fedha hizo sio za chama ni za wananchi,"

Elangwa Elangwa (@MlangwaH) ameandika kuwa, "Kuchagua upinzani ni uadui? Baba yetu uliye mbinguni tuongoze kwenye haki kwa maana hatujui kesho yake,"

Quadratus Jr (@Mleziwawana) ameandika kuwa, "Kwahiyo wanaadhibiwa kwa kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua wanaye mtaka? Hii tabia isipodhibitiwa huko tuendako tutaigawana hii nchi kama walivyofanya mataifa mengine..."

Sarafina (@SaraZone222) ameandika kuwa, "Chuki za chama hadi kwa wananchi tunakwenda wapi?"

Allyborry (Allyborry2) ameandika kuwa, "Kiukweli tunaishi tu kwa kwakuwa tumeumbwa tuishi lakini ingekua amri yake angetukatia pumzi zetu tusiishi. Kwanza ajue hakuna mbunge wala diwani anayetoa pesa mfukoni mwake kwa maendeleo ya jimbo wala kata bali wote wanategemea mfuko wa serikali,"

Willy Kaswela (@WillyKaswela) ameandika kuwa, "Mungu ni pendo. Bila pendo hakuna Mungu. Na pendo halichagui, pendo halibagui. Pendo halina dini wala kabila."

Ochu (@Ochu20724137) ameandika kuwa, "Daaah! Mungu anamuona.
Itikadi za chama kwa mkuu wa nchi wakati anaelezwa shida za wananchi wake! Kwani alikuwa kwenye ziara ya kichama au kiserikali?"

INASHANGAZA SANA.HUWEZI KUAMINI
 
Kwani wapinzani hawalipi kodi,?

Na hiyo fedha magufuli hatoi mfukoni kwake

Nikodi zetu, asijifanye mbabe kwa fedha tunazolipa wote.

Tulipe Kodi wote, kwenye mgao wanapewa ccm peke yao?

Basi tuwaachie ccm walipe kodi peke yao kama ndio hivyo.
 
Kwani wapinzani hawalipi kodi,?

Na hiyo fedha magufuli hatoi mfukoni kwake

Nikodi zetu, asijifanye mbabe kwa fedha tunazolipa wote.

Tulipe Kodi wote, kwenye mgao wanapewa ccm peke yao?

Basi tuwaachie ccm walipe kodi peke yao kama ndio hivyo.
Mkuu kwani hakuna wanaccm?, mtu mshamba ni mshamba tu
 
Halafu mtu akisema Magufuri kichaa watetezi wanasema unamkashifu Rais, ingawa yeye mwenyewe alikwisha kiri alipokuwa ziarani mkoa wa Mara mwaka jana.

Ila kwenye hii ziara ya Songwe -Katavi, huenda amesahau kutembea na dawa wanazoandikiwa kutuliza. Kiongozi yeyote mzima na mwenye akili timamu hawezi kutoa jibu la kifedhuli namna ile. Ni kichaa tu
 
Back
Top Bottom