Maendeleo hayana Chama, nini maana tafsiri yake?

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Tumekua tukimsikia mara nyingi Mh Rais Magufuli akisema maendeleo hayana Chama, Ila je ni wangapi wanaojua maana ya maneno hayo?

Niseme tu kwamba kuna watu wachache sana wanapotosha maneno hayo. "maendeleo hayana chama" anayopenda kuyatumia Mh Raisi Magufuli kwa makusudi au kwa kutokujua.

Maana ya maneno "maendeleo hayana Chama ni kwamba" hata kama wewe una mapenzi na Chama kingine tofauti na CCM ila maendeleo anayofanya Mh Rais Magufuli mfano miundombinu ya Usafiri kama Barabara, Madaraja, Meli, Ndege, Treni n.k watu wa vyama vyote watatumia.

Pia kuna miundombinu ya Afya aliyojenga Mh Rais Magufuli kama Hospitali, Zahanati n.k pia watatumia watu wa vyama vyote.

Miundombinu ya Elimu kama Mikopo ya vyuo vikuu, Elimu bure kwa Shule za Sekondari na Msingi n.k hivyo vyote wanafuika ni watu wa vyama vyote.

Nimejaribu kuandika kwa kifupi ili ieleweke.
Magufuli mitano tena (2020-2025)
Chagua Magufuli kwa maendeleo ya kweli.
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,817
2,000
Yafaa kufahamu kuwa ubaguzi ni ubaguzi tu hata kama utapakaliwa asali ili uwe mtamu,yawezekanaje ukampangia mwajiri wako akupe nini, ilihali mnaingia mkubaliano wakati wa makubaliano ya akira, haki na stahiki zote huwa zinawekwa batana. Ilene upande mmoja uwe ni wenye kukiuka makubaliano wakati wote, halafu ufikiri kuwa mambo yako sawa.
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Asante kwa ufafanuzi mkuu, kama una weza tuwekea maana ya hii nyingine itapendeza "Mkichagua Upinzani sitaleta maendeleo, Imekula kwenu"

Maana nayo inapotoshwa sana huku mtaani
Asante kwa swali zuri
Maana yake ni kwamba katika Taifa kuna miradi ya aina tofauti.
1. Kuna miradi ya kitaifa
2. Kuna miradi ya kijimbo
3. Kuna miradi ya kiwilaya n.k

Sasa Raisi ana uwezo wa kusimamia moja kwa moja miradi ya kitaifa, kiwilaya n.k
Ila miradi ya kijimbo lazima mbunge na madiwani wahusike kupitisha hasa kwenye kwenye Halmashauri zenye Meya wa upinzani.

Hivyo Rais Magufuli anaposema mkichagua upinzani sileti maendeleo maana yake hawezi kupeleka miradi ya kijimbo sababu kisiasa atakua anamnufaisha Chama kingine pia katika kupitisha miradi ya kijimbo lazima mbunge na madiwani wahusike.
Ila kwa upande wa miradi ya kitaifa hawezi kubagua mikoa au Wilaya kupeleka maendeleo.
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,817
2,000
Asante kwa swali zuri
Maana yake ni kwamba katika Taifa kuna miradi ya aina tofauti.
1. Kuna miradi ya kitaifa
2. Kuna miradi ya kijimbo...
Yaweza kuwa huo ni mtindo huru ambao wengi bado no wageni kwao yafaa tupate elimu zaidi juu yake.
 

Malimi Jr

JF-Expert Member
May 28, 2017
816
1,000
Hiyo miundombinu hata wakoloni walitujengea. Rais yeyote yule lazima atajenga miundombinu na si suala la kujivunia sababu hizo hela hatoi mfukoni mwake ni zetu.

Tunahitaji Rais ambaye atafuata sheria juu ya matumizi ya hela zetu na si huyu anayegawa hela barabarani.

Miaka 60 ya uhuru bado unaongelea miundombinu tu na muda wote mmetawala awamu hii ni mitano kwanza.
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Yafaa kufahamu kuwa ubaguzi ni ubaguzi tu hata kama utapakaliwa asali ili uwe mtamu,yawezekanaje ukampangia mwajiri wako akupe nini, ilihali mnaingia mkubaliano wakati wa makubaliano ya akira, haki na stahiki zote huwa zinawekwa batana. Ilene upande mmoja uwe ni wenye kukiuka makubaliano wakati wote, halafu ufikiri kuwa mambo yako sawa.
Hayo ni mawazo yako, uzuri Tanzania tuna uhuru mzuri wa kuongea na kutoa mawazo
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Hiyo miundombinu hata wakoloni walitujengea. Rais yeyote yule lazima atajenga miundombinu na si suala la kujivunia sababu hizo hela hatoi mfukoni mwake ni zetu.

Tunahitaji Rais ambaye atafuata sheria juu ya matumizi ya hela zetu na si huyu anayegawa hela barabarani.

Miaka 60 ya uhuru bado unaongelea miundombinu tu na muda wote mmetawala awamu hii ni mitano kwanza.
Nchi gani Afrika chini ya Jangwa la Sahara ambayo imemaliza kujenga miundombinu ukitoa nchi ya Africa Kusini?
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Asante sana mkuu..
Hivyo hapo Wananchi wa jimbo husika bila kujali chama gani hawatapata maendeleo ambayo hayana chama?
Kama nimekupata vizuri..!!
Wananchi watapata miradi ya kitaifa, kimkoa, Wilaya n.k
Ila kwa miradi ya kijimbo ni ngumu sana kama mbunge na madiwani ni upinzani sababu mara nyingi miradi ya kijimbo ni ya kisiasa zaidi
 

Bad Man Tivu

Senior Member
Jan 16, 2019
167
250
Kwan Rais akiwa mpinzani maendleo ndo yatakuwa na chama??kwmb akchaguliwa Lissu barabaran watkuw wanapita chadema tu??PATHETIC
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Unaonaje kikabaki chama kimoja ili tupate maendeleo ya haraka yani vifutwe vyama vya upinzani
Wananchi watapata miradi ya kitaifa n.k
Ila miradi ya kijimbo ni ngumu sababu mara nyingi miradi ya kijimbo ni ya kisiasa zaidi
 

Malimi Jr

JF-Expert Member
May 28, 2017
816
1,000
Nchi gani Afrika chini ya Jangwa la Sahara ambayo imemaliza kujenga miundombinu ukitoa nchi ya Africa Kusini?
Kama ni hivyo na nyie mmetosha kula tuwape na wengine nao washiriki kwenye kula keki ya taifa, mmeifanya nchi hii kuwa ni mali ya CCM awamu hii hampati kitu.

Afrika kusini waliamua kuwaacha wakoloni na kuamua kushirikiana nao ndio maana wako mbele sana. Ila nyie mliona wakoloni wanawawekea kauzibe ka kupigia madili yenu. Hakika hii laana itawaandama.

Miaka 60 mnapiga kampeni za umeme, maji, afya, miundombinu, ajira, kilimo yaani nyie kimoja mlichokifanya kwa mafanikio hakipo ukiondoa wizi na ufisadi mengine yote mmefeli.

MEREMETA, EPA, RICHMOND, RADA, RUGUMI, NHC,ESCROW. Yote haya chini ya CCM.
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Kama ni hivyo na nyie mmetosha kula tuwape na wengine nao washiriki kwenye kula keki ya taifa, mmeifanya nchi hii kuwa ni mali ya CCM awamu hii hampati kitu..
Una maana CHADEMA mnataka mchukue nchi ili mle keki ya nchi vizuri na wazungu?
hiyo ni hatari sana kwa wananchi masikini.
 

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,314
2,000
Yaweza kuwa huo ni mtindo huru ambao wengi bado no wageni kwao yafaa tupate elimu zaidi juu yake.
Jambo la maendeleo ni dogo sana kwa Magufuli, watanzania walio wengi sana sasa wameshamuelewa Magufuli kwamba ni kiongozi mzuri na ni mtendaji.
Hivyo tukimpa Kura za kutosha tunatengeneza future nzuri kwa vizazi vyetu.
Magufuli mitano tena(2020-2025)
 

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,369
2,000
Asante kwa swali zuri
Maana yake ni kwamba katika Taifa kuna miradi ya aina tofauti.
1. Kuna miradi ya kitaifa
2. Kuna miradi ya kijimbo...
Mfano kwenye jimbo unajua kuna asilimia ngapi ya wapiga kula ? Tuseme wote18+ wapige je wale ambao hakupiga kula tuseme watoto hao wanakosa gani la kutopelekewa Maendeleo

Mtu wa namna hiii si wa kutetea kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom