‘Maendeleo hayana chama’.je upinzani unatambua hili?

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Tangu kuingia kwa awamu ya tano, tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na viwanda. Maageuzi ya haya ni matokeo ya usimamizi bora rasilimali za nchi unaofanywa na Rais Maguful. Kwa kufanya mageuzi haya, Rais Magufuli anaamini katika maendeleo ya Tanzania kwa watanzania wote na huwa anajaribu kuelezea umuhimu wa watanzania kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya nchi bila kujali itikadi za vyama

Ushahidi wa haya ni kauli ya Rais Magufuli ya kuwa ‘maendeleo hayana chama’. Kupitia kauli hii Mhe. Rais anajaribu kutukumbusha umuhimu wa watanzania kushirikiana kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya vyama vyao. Licha ya kwamba CCM ndio ndio inaongoza nchi na kuleta sera za maendeleo kwa wananchi na ni CCM hiyohiyo inaamini haiwezi kuleta maendelo pekee yake bila ushirikishwaji wa vyama vya upinzani na watanzania kwa ujumla. Je, upinzani unashiriki ipasavyo kuleta maendeleo?

Katika shughuli za kimaendeleo wapinzani wanagoma kushiriki kwa sababu za kisiasa na kushindwa kukubaliana na kauli ya rais kwamba maendeleo hayana chama. Ushiriki wa upinzani ktika shughuli za maendeleo ni muhimu kwa nchi. Je, upinzani unafahamu kutoshiriki shughuli za kimaendeleo kwa sababu za kisiasa kunafanya waamini maendeleo ni ya CCM tu?

Maendeleo hayana chama inamaanisha kuwa miradi ya serikali inapowekwa mahali ni wananchi wote watafaidika nayo na si wanaCCM ama wapinzani pekee, kila mtu atatumia kadiri ya mahitaji na uwezo wake.

Serikali ya CCM inajizitatiti kupeleka maendeleo yatakayotumiwa na kila mtanzania na si wanachama wa chama Fulani cha siasa.

Wapinzani wamekuwa na ufinyu wa fikra kwamba serikali ya CCM inapendelea baadhi ya sehemu, sehemu zingine haipeleki kwa sababu za kisiasa. Huu sio ukweli, serikali inapeleka maendeleo sehemu kwenye fursa za kiuwekezaji ili kukuza uwekezaji hasa wa viwanda ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.

Karlo Mwilapwa
 
Wapinzani (wanasiasa wa upinzani) nchini Tz, ambao mimi napendelea kuwaita wanasiasa uchwara, kiukweli hawajitambui. Hawana cha kupongeza au kusifia katika serikali iliyoko madarakani, wao ni kupinga tu, tena bila hoja zenye mashiko. Wamejitoa ufahamu kabisa na kusahau kuwa siasa za vyama vingi ni siasa za kupongezana na kukosoana, na kamwe si kupingana hasa linapokuja suala la maendeleo ya jamii ua linalogusa maslahi ya umma.

Nchi ya Tanzania haiboreshi demokrasia, sababu kubwa ni kuwa na vyama vya upinzani dhaifu, zenye viongozi na wanachama maskini wa fikra. Kamwe siasa ya kupinga haijengi demokrasia au kurekebisha mapungufu ya kijamii na kisiasa na hata kiuchumi katika taifa. Siasa ya kupinga inabomoa na kuharibu taswira ya sera bora (kama inakuwepo) inayoweza kujenga nchi. Siasa ya kupinga ni tofauti sana na siasa ya kukosoa. Mbali na kupongeza, sera mbovu au mwenendo mbovu katika taifa yafaa ukabiliwe kwa ukosoaji, tena ukosoaji wenye kutoa mbinu mbadala ili kujenga mantiki na kuleta maafikiano kama si mabadiliko.

Siku zote siasa ya kukosoa hujenga chuki, badala ya umoja, hujenga uoga badala ya mshikamano na huharibu kabisa imani ya wakereketwa wa siasa hizo dhidi ya serikali yao. tena madhara haya hutokea pasipo kujali serikali inafanya vyema au la. Kwa maneno mengine, siasa za baadhi ya vyama vya upinzani Tanzania ni siasa haribifu na chochezi, si siasa endelevu.
 
kwani hii kauli ya MAENDELEO HAYANA CHAMA huwa inamaanisha nn hasa? maana kwa jinsi inavyosisitizwa kila siku huenda ina maana tofauti na wengi tunavyoielewa
 
Wanawake wenzako wote saizi wamelala wanachezea mishedede, single mothers utawajua tu mnaishi kwa buku saba saba za polepole
Mleta hoja kaja na hoja yake, ijibu kwa hoja sio kwa kejeli. Tanzania ina watu wa hovyo kabisa
 
Namshukuru Mungu tumepata rais kama Magufuli, yaani nawaza kama tungekuwa na rais chizi kama Zitto, mwehu kama Lissu, asiyejitambua kama Membe sijuwi hii nchi ingekuwaje kwa sasa.
 
Ushahidi wa haya ni kauli ya Rais Magufuli ya kuwa ‘maendeleo hayana chama’. Kupitia kauli hii Mhe. Rais anajaribu kutukumbusha umuhimu wa watanzania kushirikiana kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya vyama vyao.

Maendeleo hayana chama ila vyama ndivyo vyenye maendeleo, kwanini viwe suppressed vinapoendelea
 
Wapinzani (wanasiasa wa upinzani) nchini Tz, ambao mimi napendelea kuwaita wanasiasa uchwara, kiukweli hawajitambui. Hawana cha kupongeza au kusifia katika serikali iliyoko madarakani, wao ni kupinga tu, tena bila hoja zenye mashiko. Wamejitoa ufahamu kabisa na kusahau kuwa siasa za vyama vingi ni siasa za kupongezana na kukosoana, na kamwe si kupingana hasa linapokuja suala la maendeleo ya jamii ua linalogusa maslahi ya umma.

Nchi ya Tanzania haiboreshi demokrasia, sababu kubwa ni kuwa na vyama vya upinzani dhaifu, zenye viongozi na wanachama maskini wa fikra. Kamwe siasa ya kupinga haijengi demokrasia au kurekebisha mapungufu ya kijamii na kisiasa na hata kiuchumi katika taifa. Siasa ya kupinga inabomoa na kuharibu taswira ya sera bora (kama inakuwepo) inayoweza kujenga nchi. Siasa ya kupinga ni tofauti sana na siasa ya kukosoa. Mbali na kupongeza, sera mbovu au mwenendo mbovu katika taifa yafaa ukabiliwe kwa ukosoaji, tena ukosoaji wenye kutoa mbinu mbadala ili kujenga mantiki na kuleta maafikiano kama si mabadiliko.

Siku zote siasa ya kukosoa hujenga chuki, badala ya umoja, hujenga uoga badala ya mshikamano na huharibu kabisa imani ya wakereketwa wa siasa hizo dhidi ya serikali yao. tena madhara haya hutokea pasipo kujali serikali inafanya vyema au la. Kwa maneno mengine, siasa za baadhi ya vyama vya upinzani Tanzania ni siasa haribifu na chochezi, si siasa endelevu.
Pio sio siasa za kupigana risasi na kubambikiana kesi!
 
Namshukuru Mungu tumepata rais kama Magufuli, yaani nawaza kama tungekuwa na rais chizi kama Zitto, mwehu kama Lissu, asiyejitambua kama Membe sijuwi hii nchi ingekuwaje kwa sasa.
Huyu shetani anayetutawala sasa hana lolote zaidi ya chuki na kuendesha nchi kama anaendesha familia yake
 
Tangu kuingia kwa awamu ya tano, tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na viwanda. Maageuzi ya haya ni matokeo ya usimamizi bora rasilimali za nchi unaofanywa na Rais Maguful. Kwa kufanya mageuzi haya, Rais Magufuli anaamini katika maendeleo ya Tanzania kwa watanzania wote na huwa anajaribu kuelezea umuhimu wa watanzania kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya nchi bila kujali itikadi za vyama

Ushahidi wa haya ni kauli ya Rais Magufuli ya kuwa ‘maendeleo hayana chama’. Kupitia kauli hii Mhe. Rais anajaribu kutukumbusha umuhimu wa watanzania kushirikiana kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya vyama vyao. Licha ya kwamba CCM ndio ndio inaongoza nchi na kuleta sera za maendeleo kwa wananchi na ni CCM hiyohiyo inaamini haiwezi kuleta maendelo pekee yake bila ushirikishwaji wa vyama vya upinzani na watanzania kwa ujumla. Je, upinzani unashiriki ipasavyo kuleta maendeleo?

Katika shughuli za kimaendeleo wapinzani wanagoma kushiriki kwa sababu za kisiasa na kushindwa kukubaliana na kauli ya rais kwamba maendeleo hayana chama. Ushiriki wa upinzani ktika shughuli za maendeleo ni muhimu kwa nchi. Je, upinzani unafahamu kutoshiriki shughuli za kimaendeleo kwa sababu za kisiasa kunafanya waamini maendeleo ni ya CCM tu?

Maendeleo hayana chama inamaanisha kuwa miradi ya serikali inapowekwa mahali ni wananchi wote watafaidika nayo na si wanaCCM ama wapinzani pekee, kila mtu atatumia kadiri ya mahitaji na uwezo wake.

Serikali ya CCM inajizitatiti kupeleka maendeleo yatakayotumiwa na kila mtanzania na si wanachama wa chama Fulani cha siasa.

Wapinzani wamekuwa na ufinyu wa fikra kwamba serikali ya CCM inapendelea baadhi ya sehemu, sehemu zingine haipeleki kwa sababu za kisiasa. Huu sio ukweli, serikali inapeleka maendeleo sehemu kwenye fursa za kiuwekezaji ili kukuza uwekezaji hasa wa viwanda ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.

Karlo Mwilapwa
Wanatambus hilo, jiulize kwa nini hawataki kushiriki!
 
Wapinzani (wanasiasa wa upinzani) nchini Tz, ambao mimi napendelea kuwaita wanasiasa uchwara, kiukweli hawajitambui. Hawana cha kupongeza au kusifia katika serikali iliyoko madarakani, wao ni kupinga tu, tena bila hoja zenye mashiko. Wamejitoa ufahamu kabisa na kusahau kuwa siasa za vyama vingi ni siasa za kupongezana na kukosoana, na kamwe si kupingana hasa linapokuja suala la maendeleo ya jamii ua linalogusa maslahi ya umma.

Nchi ya Tanzania haiboreshi demokrasia, sababu kubwa ni kuwa na vyama vya upinzani dhaifu, zenye viongozi na wanachama maskini wa fikra. Kamwe siasa ya kupinga haijengi demokrasia au kurekebisha mapungufu ya kijamii na kisiasa na hata kiuchumi katika taifa. Siasa ya kupinga inabomoa na kuharibu taswira ya sera bora (kama inakuwepo) inayoweza kujenga nchi. Siasa ya kupinga ni tofauti sana na siasa ya kukosoa. Mbali na kupongeza, sera mbovu au mwenendo mbovu katika taifa yafaa ukabiliwe kwa ukosoaji, tena ukosoaji wenye kutoa mbinu mbadala ili kujenga mantiki na kuleta maafikiano kama si mabadiliko.

Siku zote siasa ya kukosoa hujenga chuki, badala ya umoja, hujenga uoga badala ya mshikamano na huharibu kabisa imani ya wakereketwa wa siasa hizo dhidi ya serikali yao. tena madhara haya hutokea pasipo kujali serikali inafanya vyema au la. Kwa maneno mengine, siasa za baadhi ya vyama vya upinzani Tanzania ni siasa haribifu na chochezi, si siasa endelevu.
Neno
Ubarikiwe sana walahi
Inasikitisha kwa kweli
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom