Maendeleo endelevu hupatikana kama kuna siasa safi

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Wanajamvi nawasalimu nyote kwa jina la jamhuri ya muungano.

Napenda nijadili kidogo kuhusu suala la siasa safi. Hili ni shida kubwa sana hapa kwetu tanzania. Siasa safi si kuwa na amani au kuwa na utulivu hapana kulingana na uelewa wangu. Amani na utulivu ni matokeo tu kipo kinachofanya watu kuwa na amani na utulivu ukawepo. Kwangu mimi amani ya tanzania ina msingi wake katika siasa ya ujamaa na kujitegemea ya julius nyerere. Mabaki ya siasa ile ndo inafanya tanzania kuwa na amani na imeeleweka sana, kuvunja msingi huo ni kama kuondoa jiwe la msingi wa nyumba.

Moja ya hoja kubwa ya siasa ya ujamaa ni ARDHI KUWA MALI YA UMMA. Hii hoja imeeleweka sana kwa watanzania na wanaiishi kila siku. Kwa mfano mtu anatoka usukumani akaja mbeya wala hamna wa kuuliza kwa kuwa havunji sheria alipofikia ni kwake mwisho anaoa mnyakyusa maisha inaendelea na watoto wake watakuwa hapo. Baadaye watoto wake wanaweza kwenda morogoro akaolewa au kuoa mpogoro no problem. Huu ndo msingi wa amani. Yapo mengine kama kuvunjwa kwa uchifu na ukabila pamoja na kugawa keki ya taifa equaly kitu ambacho hakipo kwa sasa.

Sasa mimi nimeona leo niongelee siasa safi. Siasa safi ni siasa inayoweza kukumbatia watu wote wenye mawazo tofauti na kuweza kubaini adui wa taifa na pia yenye kutoa fursa ya watu kujiletea maendeleo. Siasa safi ni siasa isiyoonea mtu. Siasa safi ni mfumo usio kandamizi. Ni mfumo wa jamii usio kandamizi unaoweka watu makini madarakani wanaoweza kusimamia rasilimali ya nchi. Siasa safi huzalisha viongozi safi na wazalendo wanaochukia rushwa na wanaoweza kulinda nchi dhidi ya maadui zake wa ndani na nje. Siasa safi inaweza kubaini adui wa kweli na adui feki. Siasa safi inazaa mifumo makini ya usalama wa nchi na jeshi la nchi. Angalau kwa misingi iliyokuwepo huko nyuma tunajikongoja lakini tunakwenda mbali sana kwa sasa. Jeshi inatoa ushahidi mahakamani alafu anaongea utumbo mtupu unaona kabisa mchongo wenye nia ambayo sisi wengine tunashindwa kuelewa. Mfano huo na mifano mingine inaonyesha siasa chafu.

CCM imeshindwa kutupa siasa safi badala yake wanafanya uchafuzi na kutushangaza maana maadui zetu wa kweli hatuwashughulikii ipasavyo. Hatuna mipango ya kujinasua kwenye mitego yao na tunazidi kunasa kwenye mitego yao. Magu alipoingia alienda kichwa kichwa akakwama mkwamo mbaya ila tulimuona usoni nia yake kwa maadui zetu wa ukweli. Lakini nadhani ni muda muafaka wa ccm kuwataka waache siasa chafi tutengeneze mifumo safi waachane na uchafuzi huu.

Ombi langu ebu tuungane kama taifa kwa ujumla wetu tupambane na adui wetu anayetukwamisha na kushindwa kutoka kwenye umaskini huu kama nchi kuliko kuwa kupoteza nguvu nyingi kwa adui asiye adui. Acheni kuwaza kubaki madarakani maana mawazo hayo imewapofusha na kupeleka rasilimali nyingi sehemu ambayo haikustahili huku adui yetu anatupiga kweupe.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom