Maendeleo bila 'Mapinduzi' ya Utawala wa sasa ni ndoto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maendeleo bila 'Mapinduzi' ya Utawala wa sasa ni ndoto!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ndyoko, Nov 5, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Nimetafakari kwa muda nimegundua yafuatayo. Kwamba maendeleo ya kweli kwa TZ yetu kamwe hayawezi kuja ndani ya utawala wa sasa wa CCM. Wengi tunajilinganisha na jirani zetu Rwanda, Kenya, Uganda, Burundi nk. Ukweli ni kwamba wenzetu wamefika hapo baada ya kukubali kunywa dawa chungu ambayo sisi watanzania tunaogopa kuitumia. Maendeleo ya Rwanda na nchi nyingine hayakuja hiv hivi, wananchi waliigharamia maendeleo hayo.

  Ni nani asiyejua kuwa ugumu wa watawal kuachia madaraka kwa njia za kidemokrasia ndiyo chanzo cha maendeleo na ufahamu mkubwa wa haki na wajibu wa serikali tawala kwa wananchi wake? Damu iliyomwagika Rwanda, leo inalipa kwa nchi kuwa na discipline ya hali ya juu ktk matumizi ya rasilimali za nchi kwa manufaa ya watu wote. Vurugu zilizoambata na vifo vya wakenya wengi mwishowe vimepelekea serikali kuweka misingi imara ktk utawala wa nchi kwa kuwa na katika isiyo toa nafasi kwa mambo ya kijinga kufanywa na watawala. Hali sio tofauti kwa majirani wengine kama burundi na uganda ingawa museveni tayari amesha sahau wajibu wake kwa waganda na tayari hana tofauti na watawala wa TZ.

  Ukiangalia yanayotokea TZ, kuna jambo moja ninaliona, kwamba watawala wameshafika mahali wanaona kama hii nchi ni yao na hakuna wa kuwababaisha kwani wao, kundi la watu wacahche na familia zao, wanaona nchi ni kwa ajili yao pamoja na rasilimali zake. Wanafanya haya wakiamini hakuna wa kuwababaisha-ukiangalia ni kama kweli mawazo yao-kwani ni mambo mengi mabaya wamefanya hakuna ambaye amethubutu kuwawajibisha na wanaona kelele zinazopigwa ni sawa na bure kwani kila uchaguzi unapokuja mbona wanashinda tena kwa madai ushindi wa 'kishindo'? Hawaoni sababu ya wao kuwajibika kwa wananchi kwani watz ni kama tumekubaliana na wao kuendelea kufanya ufedhuli wao.

  Binafsi nadhani wakati umefika sasa kwa watanzania kurudisha heshima na utu wa wananchi kwa kuamua kuchukua maamuzi ya maana. Kwa sasa iemdhihirika Utawala wa sasa nchi hauko tayari kuwatumikia wananchi na wameamua kuegemea ufisadi na watu wengine w mlengo huo, wa ndani ya nchi n nje ya nchi pia. Hatua za kujinasua zichukuliwe hata ikibidi kwa kwa damu kidogo kumwagika, hili litaleta adabu na kuturudisha ktk mstari wa kuwa na hofu ya kutenda uovu na hari ya kuwatumikia wananchi badala ya matumbo yetu binafsi, familia zetu na makuwadi wengine wa ufedhuli toka nchi za ughaibuni.

  Nimewasilisha!
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kabla hata sijamaliza kusoma hiyo unayoiita tafakuri yako, naona kuna mapungufu makubwa sana. Hebu niambie ni maendeleo gani waliyopiga katika nchi ulizozilist hapo juu, Kenya na burundi kabla na baada ya hayo unayoyaita mapinduzi. Uganda kuna maendeleo gani. Ama kweli hii ni tafakuri y abunuasi.
  HAlafu sijakusoma. SASAUNATAKA TUPIGANE? UKO TAYARI? This is real porojo.
   
 3. n

  ngwele Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo umetumia masaburi ktk kuwaza kwako. Hujui misingi iliyojengwa kenya baada ya uchakachuaji wa kura. Uliza ndo utajua kabita ya kenya sasa inasemaje kuhusu mamlaka ya rais. Jaribu kufikiri kwa kichwa badala ya masaburi, lol!
   
 4. n

  ngwele Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona mimi nimeielewa fresh kabisa
   
Loading...