Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
MAEMBE YA KWETU MATAMU, YAKIDONDOKA YENYEWE!
Maembe yalodondoka yenyewe
Maembe yetu matamu, matamu yanipa hamu
Ladha yake ni adimu, yana vigezo muhimu,
Si machachu kama ndimu, yanataka utaalamu,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!
Hayahitaji vurugu, hayapopolewi mawe,
Ya Kisarawe na pugu, hata ya kule Kongowe,
Hata pwaguzi na pwagu, wanavyopata kiwewe

Si maembe ya kizungu, ni maembe ya kikwetu,
Utaapia kwa Mungu, ukila roho i kwatu,
Ni radhi nitiwe pingu, matamu madodo yetu,

Yanapokuwa mtini, mabichi yanavutia,
Yanini purukushani, kuiva yataivia,
Yabadilika rangi tawini, na harufu yavutia

Yatapigwa na upepo, kuringisha doli doli,
Yakininginia kama popo, yapendeza kwelikweli,
Kisebu na kiroho papo, kitakupata kwa kweli
Maembe kweli matmu, yakidondoka yenyewe!
Subira yavuta kheri, yanapopoka yenyewe,
Wala hayataki shari, usiyarushie mawe,
Iwe shambani au pori, shika kikapu na wewe,

Anza kuyaokoteza, embe moja baada ya moja,
Ukipata la kupendeza, kwenye mamia ni moja,
Hilo siyo la kuuza, hilo ni embe la haja,

Nililosema nimesema, ya kwetu kweli matamu,
Hivyo kutama natama, nimezidiwa na hamu,
Moyo umeshanituma, nalila kama wazimu,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe
M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)