Maelfu ya wayahudi weusi waandamana Israel kupinga ubaguzi mmoja amiminiwa risasi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,438
Jamii ya wahajiri wa Ethiopia wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel, imeisababishia changamoto mpya serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo, kutokana na maandamano yake mapya mjini Haifa.
Hata kama sababu ya maandamano ya sasa ya wahajiri hao wa Ethiopia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu inatokana na kuuawa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 na polisi wa utawala haramu wa Israel, lakini maandamano ya wahajiri hao wanaoishi huko Israel sio suala jipya na lina sababu za msingi. Kwa mujibu wa takwimu, kwa uchache watu laki moja na elfu 30 ya watu wanaoishi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu ni Mayahudi wenye asili ya Ethiopia ambapo kwa mujibu wa tovuti ya Ethiopian National Project, elfu 82 kati yao walizaliwa nje ya Israel. Ukweli ni kwamba hali ya Mayahudi hao elfu 82 waliopelekwa katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu chini ya staratijia ya kuwahamishia wahajiri wa Kiyahudi huko Israel, inatofautiana sana na Mayahudi wengine wanaoishi ndani ya ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu (Israel). Baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni linawatazama Mayahudi wenye asili ya Ethiopia na ambao wanaitwa 'Mafalasha', kuwa ni watu wa darala la tatu. Ni kwa ajili hiyo ndio maana kunatekelezwa ukatili wa kimuundo dhidi ya Mayahudi hao wa Kifalasha, kukiwemo kuwabagua, kuwafanya kuwa masikini wa kutupwa na kuwafanyia ukatili wa kimwili. Utawala wa Kizayuni ambao uliwapa ahadi mbalimbali Mayahudi hao wa Ethiopia kwa ajili ya kuwashawishi wahamie katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, uliwaweka katika maeneo ya mashariki mwa Israel ambayo kwa kawaida huishi jamii za watu masikini.
Mayahudi wenye asili ya Ethiopia na Mayahudi wanaotoka Mashariki wote wanalalamikia ubaguzi wanaofanyiwa na utawala huo wa Kizayuni. Kwa mfano, Mayahudi hao hawapewi haki sawa na Mayahudi wanaotoka nchi za Magharibi. Moja ya sababu za kuendelea maandamano ya Mayahudi wenye asili ya Ethiopia dhidi ya serikali ya Tel Aviv ni ubaguzi huo. Ama sababu nyingine ni ongezeko la umasikini kati ya jamii ya Mayahudi wa Ethiopia. Hii ni kusema kuwa umasikini kati ya Mayahudi hao wa Falasha wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni wa kiwango cha 3.5 ikilinganishwa na umasikini wa maeneo mengine yote ya utawala huo ghasibu. Katika uwanja huo hivi karibuni mtandao mmoja wa habari nchini Misri uliandika kuhusiana na suala hilo kwamba: "Kiwango cha umasikini kati ya Mayahudi wenye asili ya Ethiopia kimefikia asilimia 51.7 katika hali ambayo kiwango cha umasikini katika maeneo yote ya utawala wa Kizayuni ni asilimia 15.8." Umasikini miongoni mwa jamii ya Mayahudi hao umefikia kiwango ambacho, watoto wao wanashindwa hata kwenda shule. Mashambulizi ya kimwili ya askari wa utawala wa Kizayuni ni sababu nyingine muhimu ya kufanyika maandamano ya Wayahudi wenye asili ya Ethiopia dhidi ya serikali ya Tel Aviv. Mayahudi hao wanasema kuwa polisi wa utawala huo khabithi wamekuwa wakiwatuhumu na kuwashambulia kwa kila jambo, hata bila ya kuwa na ushahidi wala uthibitisho wa kutosha wa kuhusika kwao na jambo wanalotuhumiwa kuhusika nalo.
Maandamano ya sasa ya Haifa yaliibuka katika kulalamikia mauaji dhidi ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 wa jamii ya Mayahudi hao. Jumapili iliyopita askari mmoja wa Israel alimshambulia na kumuua kijana huyo aliyekuwa anaitwa Solomon Teka mjini Haifa kwa kumpiga risasi. Hii ni katika hali ambayo kijana huyo wa jamii ya Mafalasha hakuhatarisha kivyo vyote maisha ya askari huyo. Itakumbukwa kuwa mwezi Januari mwaka huu, maelfu ya Mayahudi hao wenye asili ya Ethiopia pia walifanya maandamano makubwa mjini Tel Aviv baada ya askari mwingine wa Israel kummiminia risasi kijana mwingine mwenye asili ya Ethiopia. Nukta muhimu ni hii kwamba ubaguzi mkubwa wa rangi wa utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Mayahudi hao, kiasi cha kufikia kuwaua, ni jambo la kawaida kwa kuwa askari wanaohusika na mauaji hayo huwa wanafutiwa mashtaka kama ilivyoshuhudiwa katika tukio la hivi karibuni ambapo awali mtuhumiwa wa mauaji alishikiliwa na baada ya siku chache, akaachiliwa huru. Nukta ya kumalizia ni hii kwamba maandamano ya Mayahudi wenye asili ya Ethiopia wanaoishi ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Isreal yamebadilika na kuwa tatizo la usalama kwa Benjamin Netanyahu ambaye kwa sasa baada ya kushindwa kuunda serikali mpya, anaendelea kuongoza serikali isiyo kamilifu. Kwa upande mwingine anakabiliwa na kampeni za uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni uchaguzi wa pili kufanyika katika kipindi cha miezi sita.
Tags
ISRAEL Picha ya kijana aliyemiminiwa risasi bila hatia na askari wa Israel na kupelekea kuibuka maandamano 
Mayahudi wenye asili View attachment 1148401
4bsj6bb7662aa01ga0e_800C450.jpeg
4bsj9cb2fc15ed1ga0c_800C450.jpeg
 
R.i.p broo (pure jew) uliyeuawawa na wayahudi feki mazayuni wa israel kisa wewe eti ni mweusi daaah View attachment 1148406
Walimpinga Yesu,na hawamkubali mpaka leo,na ni ndugu yao wa damu,na wanajuwa kama katumwa na Muumba wa viumbe vyote,tunavyovijua na tusivyovijuwa,yaani ni Mtume wa Mungu,itakuwa wengine,wasiokuwa ndugu zao wa damu.
 
Walimpinga Yesu,na hawamkubali mpaka leo,na ni ndugu yao wa damu,na wanajuwa kama katumwa na Muumba wa viumbe vyote,tunavyovijua na tusivyovijuwa,yaani ni Mtume wa Mungu,itakuwa wengine,wasiokuwa ndugu zao wa damu.
Na hao hao Wayahudi ndio walioeneza ukristo.

Petro alikuwa nani? Yohana alikuwa nani eti baadaye miaka 600 kupita Mudi akampachika jina Yahya (pathetic) Stephano alikuwa nani? Paulo alikuwa nani wewee mbwiga?

Ndio maana tunawapenda wayahudi.

Better to worship a stone than being a Muslim. And better to go to hell than muslim paradise bcoz hell is much cooler than your paradise.

Jesus first Jesus Forever.

If you don't love Jesus who the hell will you love?

God bless Israel
 
Na hao hao Wayahudi ndio walioeneza ukristo.

Petro alikuwa nani? Yohana alikuwa nani eti baadaye miaka 600 kupita Mudi akampachika jina Yahya (pathetic) Stephano alikuwa nani? Paulo alikuwa nani wewee mbwiga?

Ndio maana tunawapenda wayahudi.

Better to worship a stone than being a Muslim. And better to go to hell than muslim paradise bcoz hell is much cooler than your paradise.

Jesus first Jesus Forever.

If you don't love Jesus who the hell will you love?

God bless Israel
It's better to let people think u are stupid than open ur mouth and prove u are stupid.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom