kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Maelfu ya Mayahudi wamefanya maandamano mjini Tel Aviv kuunga mkono kuundwa taifa huru la Palestina sambamba na kulaani miaka 50 ya utawala haramu wa Israel kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
Maandamano hayo yameitishwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Israel ya Peace Now kwa lengo la kukosoa kughusubiwa ardhi za Palestina, jinai na ubaguzi dhidi ya Wapalestina.
Avi Buskila, kiongozi wa asasi hiyo amesema wakati umefika kutuma ujumbe kwa walimwengu kwamba kuna baadhi ya Mayahudi wasiounga mkono kughusubiwa ardhi za Palestina.
Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera za Palestina, huku ujumbe wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas ukisomwa katika maandamano hayo.
Sehemu ya ujumbe huo inasema: 'Hakuna sauti yenye nguvu kushinda sauti ya haki, amani, haki ya watu ya kufanya maamuzi na uhuru wa kuondokana na mzigo wa kukaliwa kwa mabavu ardhi yenu.'
Siku chache zilizopita, Wapalestina kote duniani waliadhimisha Siku ya Nakaba, kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 69 tangu ulipoundwa utawala bandia na haramu wa Israel mwaka 1948.
Itakumbukwa kuwa, Wapalestina zaidi ya 750,000 walitimuliwa kutoka ardhi zao mwaka 1948 wakati wa kuundwa dola haramu la Israel na hivyo wakasambaratika katika kambi za wakimbizi huko Ghaza, Ukingo wa Magharibi, Syria, Jordan, Lebanon na maeneo mengine duniani. Hivi sasa kunakadiriwa kuwepo wakimbizi zaidi ya milioni tano Wapalestina duniani.
Chanzoarstoday.sw