Maelfu ya wasaka wahanga wa ajira kada mbalibali upinzani chukueni dola kupita hili

kofia ya plastiki

JF-Expert Member
Jun 9, 2019
416
404
Wakuu katika kutafakari, maelfu ya wasaka ajira toka 2014 so diploma si degree ngazi mbalimbali nchin huu ni udhaifu wa awamu ya 5..

2020 upinzani kazi kwenu fursa hiyo! Na ikumbukwe kua vijana wako wengi sana mtaani ya hubeba kariba nusu ya population
 
Sidhani km kusubiri mpaka serikali iliyopo itoke madarakani ndio wahitimu wapate ajira ndio solution, tuisaidie serikali iliyopo kwa mawazo nini kifanyike watu wapate ajira...lakini ni kweli serikali hii imewashughulikia wenye vyeti feki, imeanzisha miradi kibao and yet ajira hakuna, kuna tatizo mahali sio bure...
 
Watu wanaoingia kwenye soko la ajira kwa mwaka ni approximation ya laki 9 kwa miaka mitano maana yake kuna vijana milion 4.5 wako mtaani ukiongeza na wale wa kule nyuma unaweza kuta kama 10 mil jobles je upinzani wanakuja na mkakati gani wa kuwapa kazi population yote hii ? ni uongo hawa watu ni wengi.
 
Tuwasaidie upinzani,hii ni gap kwenye serikali ya Magufuli, kwengine barabara sijui ndege umeme anajitahidi ila swala la ajira anasua sua..wapinzani wanaweza kuchukua hii chance km fursa kwa kuja na mpango maalumu wa kutatua tatizo la ajira, I believe it can be done,,,
 
vijana wengi hawana ajira lakini hawana tumaini kwa upinzani hata ukichukua dola na bado tunaona chaguo letu namba moja ni CCM. Sababu kuu kwa nini Sisi vijana tunaiamini CCM:

1. Vijana katika nyakati tofauti kabla ya awamu ya tano walikuwa wanatumika katika kujenga upinzani hewa hususani kwa kufanya maandamano na migomo. Awamu hii ya tano tumeona umuhimu Wa kushiriki kujenga nchi kwa kufanya kazi HAPA KAZI TU.

2. Bado Sisi vijana tunaamini kuwa chama pekee kilichobeba maono na matarajio yetu ni CCM.

3. ushindi wetu Sisi vijana ni CCM , ni chama kilichotupa jeuri ya kuwa wazalendo na viburi Wa maendeleo katika ulimwengu Wa wababe na wenye nguvu kubwa kiuchumi
 
Swala la ajira sio Tanzania pekee
Hili ni janga la dunia nzima
Hapo ni serikali kutunga sera bora kuiwezesha sekta binafs ili kutengeneza nafasi nyingi za ajira.

Na pia swala la Kuanzisha vikund vya wahitimu na kuwapa elimu pamoja na mikopo isiyo na riba au riba nafuu ili waweze kujitegemea kwa kuanzisha miradi yao wenyew.

Serikali itafute masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo. Hapa tz tuna aidh yenye rutuba watu wanalima, wakija sokoni kila mkulima anarud nyumban analia faida hakuna.

Mwisho:Ila wadau mwanzo mgum pale unapotoka chuo na kusota miaka bila ajira ukikumbuka ulivokesha shule na stik +sup za hapa na pale lkn ukachomoka afu unakuja kuanza na zero bila ajira, asikwambie mtu.
 
Mimi naona pawepo na utaratibu kwa Serikali wakishirikiana na taasisi za kifedha mfano, mabenki ya kibiashara, BOT na vyuo vya taasisi za fedha.

Vijana wote Tanzania waingie katika mfumo wa teknolojia ili watambuliwe elimu zao, mahali wanapoishi na uhitaji wao.
Vijana wawe na uwezo wa kupata huduma ya mtandao (Software Application ) ambayo atajisajiri, ataweka taarifa zake zote zitakazo hitajika kwa Serikali na taasisi za kifedha.
Yafuatayo ni mawazo tu kama itafaa.
Maoni;
1. Watengeneze "software" nzuri ya kifedha itakayofanya kazi ndani ya Tanzania tu yaani wawe na uwezo wa kuidhibiti kiteknolojia.
2. Pia, wawe na uwezo wa kutoa elimu fupi ya kifedha na kiuwekezaji kwa kutumia taasisi tajwa.
3. Vijana wahitimu wa vyuo ngazi ya chini (under Veta), kati (College) na juu (University) kwa sifa stahiki wapewe vitambulisho vya Taifa (National ID).
4. Banks wawakopeshe vijana fedha wajiajiri wenyewe nashauri mkopo uwe wa mtu mmoja mmoja na sio kikundi.
5. Serikali kuu iwe mdhamini wa hiyo mikopo kwa vijana.
6. Halmashauri ziweke utaratibu wa kuwatambua vijana hao kwa kuwapa vyeti (certificate) ambayo kijana atachangia kiasi kidogo mfano Tsh.20,000/= ada kwa mwaka. Hapa nikimaanisha asisumbuliwe kwenye ushuru au kodi ya aina yoyote.
7. TRA iweke Tax holiday ya miaka 3 na itoe (Special Certificate) kwa kuwatambua vijana watakao wekeza katika miradi yenye kuhitajika kutolewa kodi.
8. Pesa zitumwe kwa simu au kupitia Banks itategemea na muhitaji mwenyewe njia aipendayo.
9. Mtaji uwe kuanzia Tsh.500,000/= mpaka Tsh.1Bilioni.
10. Kwenye hiyo Software Application iwe inauwezo wa kutambua aina za biashara kwa makundi, makadirio ya mitaji na maeneo ya uwekezaji utakapo fanyika ndani ya nchi.
11. Taasisi zote zinazohusika na uwekezaji mfano TIC, NIDA, BRELA, TZ CHAMBER OF COMMERCE nk wawe connected baada ya kijana kujisajiri na kupata mkopo wake.
12. Application fee kwa mwaka napendekeza iwe Tsh.20,000/= hii italipwa kabla ya huduma kwa njia ya simu au Bank.

NB
SIO RAHISI KUWAWEKA VIJANA PAMOJA KWENYE MAKUNDI WENYE MAWAZO TOFAUTI UKAWAPA PESA WAKAFANIKIWA KATIKA MRADI AU BIASHARA, HII IMESHAKUA CHANGAMOTO NA SIO NJIA NZURI NI BORA MUWAKOPESHE MMOJA MMOJA WAUNGANE WENYEWE WENYE MAWAZO YA KUFANANA KWA MANUFAA YA NCHI.

NINA IMANI TUTAPUNGUZA CHANGAMOTO NA UTEGEMEZI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA MPAKA TAIFA.
 
.
Sidhani km kusubiri mpaka serikali iliyopo itoke madarakani ndio wahitimu wapate ajira ndio solution, tuisaidie serikali iliyopo kwa mawazo nini kifanyike watu wapate ajira...lakini ni kweli serikali hii imewashughulikia wenye vyeti feki, imeanzisha miradi kibao and yet ajira hakuna, kuna tatizo mahali sio bure...
Tatizo serikali wamesema hawapangiwi.
 
Wapinzani gani? Hawa kina Zitto wanaomwombea Magufuli mabaya ndio tuwaamini?

Ccm bado ipo kwa miaka 100 mbele
Watu wanaoingia kwenye soko la ajira kwa mwaka ni approximation ya laki 9 kwa miaka mitano maana yake kuna vijana milion 4.5 wako mtaani ukiongeza na wale wa kule nyuma unaweza kuta kama 10 mil jobles je upinzani wanakuja na mkakati gani wa kuwapa kazi population yote hii ? ni uongo hawa watu ni wengi.
 
Nashauri tuanzishe kampeni rais ajiuzuru kashashindwa kuongoza nchi mpaka sasa nusu ya bajeti inatumika kulipa madeni miradi aliyokopea mkopo sio yakurudisha pesa leo wala kesho ni kama kutafuta sifa tu rais katuongopea sijui tanzania ya viwanda lakini vipaumbele tunavyoviona sasa ni vya kununua ndege ili kuongeza utalii
 
Mleta mada ungejua hawa vijana wakiwa mwaka wa mwisho wanavyogombea na kuhamasishana kuchukua kadi za UVCCM usingeleta hii mada.
Tunakuaga na presha za kitaa sana tukiwa last year, sijui kwa nini?
Watu walichukua kadi kibao, alaf waajiriwa wanawacheka tu hihihiii
 
Tatizo la ajira asilimia kubwa linasababishwa na watendaji wa chini Serikalini. Unakuta mtu akitaka kuanzisha kampuni ambayo itaajiri vijana wengi kunakuwa na urasimu wa kupata vibali mfano Ardhi, brela, nemc n.k.
Nakumbuka raia mmoja wa Mauritius alishalalamika jinsi alivyosotea zaidi ya mwaka kupata kibali idara ya ardhi kwa ajili ya kujenga kiwanda cha sukari, hapo bado hajaenda Nemc napo azungushwe. Kiwanda cha sukari hutoa ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya elfu10.
Viongozi wa juu serikalini wakisema wawajibishe watendaji wazembe unakuta wazee wa kupinga wanawatetea.
Kwa kifupi tatizo la ajira linasababishwa na ubibafsi wetu sisi wenyewe. Mtu kwa kuwa ameajiriwa hawawazii wengine ndio maana unakuta anachelewesha vibali vya kuanzisha kampuni flani.
Jambo la msingi ni viongozi wa juu Serikali kuendelea kuwashughulikia bila huruma wale wote wanaokwamisha uwekezaji nchini.
 
Nashauri tuanzishe kampeni rais ajiuzuru kashashindwa kuongoza nchi mpaka sasa nusu ya bajeti inatumika kulipa madeni miradi aliyokopea mkopo sio yakurudisha pesa leo wala kesho ni kama kutafuta sifa tu rais katuongopea sijui tanzania ya viwanda lakini vipaumbele tunavyoviona sasa ni vya kununua ndege ili kuongeza utalii
Mkuu uko iringa maeneo gani
 
Tatizo la ajira asilimia kubwa linasababishwa na watendaji wa chini Serikalini. Unakuta mtu akitaka kuanzisha kampuni ambayo itaajiri vijana wengi kunakuwa na urasimu wa kupata vibali mfano Ardhi, brela, nemc n.k.
Nakumbuka raia mmoja wa Mauritius alishalalamika jinsi alivyosotea zaidi ya mwaka kupata kibali idara ya ardhi kwa ajili ya kujenga kiwanda cha sukari, hapo bado hajaenda Nemc napo azungushwe. Kiwanda cha sukari hutoa ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya elfu10.
Viongozi wa juu serikalini wakisema wawajibishe watendaji wazembe unakuta wazee wa kupinga wanawatetea.
Kwa kifupi tatizo la ajira linasababishwa na ubibafsi wetu sisi wenyewe. Mtu kwa kuwa ameajiriwa hawawazii wengine ndio maana unakuta anachelewesha vibali vya kuanzisha kampuni flani.
Jambo la msingi ni viongozi wa juu Serikali kuendelea kuwashughulikia bila huruma wale wote wanaokwamisha uwekezaji nchini.
Uko sahihi mkuu
 
vijana wengi hawana ajira lakini hawana tumaini kwa upinzani hata ukichukua dola na bado tunaona chaguo letu namba moja ni CCM. Sababu kuu kwa nini Sisi vijana tunaiamini CCM:

1. Vijana katika nyakati tofauti kabla ya awamu ya tano walikuwa wanatumika katika kujenga upinzani hewa hususani kwa kufanya maandamano na migomo. Awamu hii ya tano tumeona umuhimu Wa kushiriki kujenga nchi kwa kufanya kazi HAPA KAZI TU.

2. Bado Sisi vijana tunaamini kuwa chama pekee kilichobeba maono na matarajio yetu ni CCM.

3. ushindi wetu Sisi vijana ni CCM , ni chama kilichotupa jeuri ya kuwa wazalendo na viburi Wa maendeleo katika ulimwengu Wa wababe na wenye nguvu kubwa kiuchumi
Buku7 kwa siku si habaa

Ova
 
Watu wanaoingia kwenye soko la ajira kwa mwaka ni approximation ya laki 9 kwa miaka mitano maana yake kuna vijana milion 4.5 wako mtaani ukiongeza na wale wa kule nyuma unaweza kuta kama 10 mil jobles je upinzani wanakuja na mkakati gani wa kuwapa kazi population yote hii ? ni uongo hawa watu ni wengi.
Wanatakiwa waajiriwe,wawekewe mazingira ya kujiajiri kwa kupewa vitendea kazi vya kupractice fani walizomea au mitaji nk.Tatizo letu kubwa ni Sera ya elimu ambayo haimfanyi mhitimu kuanzia wa darsa LA saba,Form four/six,vyuo kutokuwa na ujuzi kwa kiwango cha elimu aliyopata.
Tubadili mifumo yetu ya elimu na kutengeneza Sera wezeshi,sheria madhubuti na Katiba ya wananchi ili kuwezesha Watanzania wote kufaidi keki/kasungura kadogo kwa kila mmoja.
 
Tatizo si ajira Bali ni mfumo wa elimu hauwaandai wahitimu kujiajiri ,leo ukimuuliza mhitimu mtaji huu hapa hana cha kufanya,wengi wanaandaliwa kuwa mabosi na wafanyakazi tu.Na elimu inayotolewa haizingatii soko la ajira Na mahitaji halisi. Mfano unaandaa ma- IT 2000 wakati soko linahitaji 200 tu. Hata tuje utawala gani hautaweza kutatua hilo tatizo.
Vyama vyetu vya upinzani Tz bado ni kama wapiga dili tu,hawasimamii Sera za msingi kutatua matatizo ya watanzania kama ajira,haki za wakulima Na wafanyakazi . Hivi vyama vipiganie haya kwanza si kuwaza kuingia Ikulu au siasa za kutegemea matukio.
CHADEMA ilipata umaarufu ilipoweka vita vya ufisadi kama nguzo lakini kupokea wanao tuhimiwa mafisadi ndipo ilipopoteza mwelekeo.
Wanasiasa wengi hata ndani ya CCM ni wachumia tumbo ndio maana hata Mh anatumbua kila siku. Kinachoisaidia CCM ni kuwa chama ambacho ni taasisi sio cha MTU au kikundi.
Kuishinda itabidi vyama visimame kama taasisi inayosimamia mahitaji muhimu ya jamii kama ajira,mishara bora,maslahi ya wakulima Na uchumi utakao mwezesha kupata mahitaji muhimu.
Wanasiasa kulalamika kuwa wamenyimwa majukwaa isiwe kisingizio,kuna majukwaa ya mitandao ya kijamii Na vyombo vya hapari vina nguvu hata kuliko majukwaa ya mikutano maana asilimia kubwa ss ya watz vinawafikia.
Sera za kumponda au kumlaumu Mh zitawapoteza,watupe nondo Na Sera mbadala au masuluhisho mbadala hapo ndipo siasa za nchi yetu zitakuwa za maana Na zenye kujenga umoja..
Sera mbadala ndio maana ya upinzani Na kwa nchii hii Na karne hii tunauhitaji sanaaa
 
Mm ni mpinzani kindakindaki, lkn sitokubali na nitapinga kwa nguvu zangu zote kutumia ajenda ya wasaka ajira kama ngazi ya wapinzani kupata kura.

Tanzania hakuna tatizo la ajira. Tatizo tulilonalo ni kukosa wasomi. Wahitimu wengi siyo wasomi, maana hawana kitu kichwani. Huko vyuoni walijikita kujamiiana tu badala ya kutafuta maarifa.

Wanawezaje kulilia ajira ktk nchi kama Tanzania ambapo ardhi yenye rutuba imejaa tele? Narudia tena hawa graduates kamwe hawawezi kuwa ajenda ya wapinzani.
 
Back
Top Bottom