Maelfu ya wanachama wa CHADEMA wampokea Dr. Magufuli na kujiunga na CCM

Kwahiyo Leo lowasa siyo fisadi tena au unataka kusema nini.

CCM na ndani ya Serikali na katika vitengo nyeti Wapo mafisadi wangapi kumfananisha na Lowasa mnaemtuhumu tu ?.

Huyo Lowasa baada ya kujiuzulu ufisadi ulipungua au ndio uliongezeka?.

Msitafute sababu ya kujifichia kwa Lowasa ili mpate huruma kwa wananchi ,mmeshindwa kwa miaka 50 sasa kutoa matokeo tuliyoyatarajia kama wananchi so mnatakiwa mkae pembeni.

Madaraka yanatoka kwetu wananchi na sisi kwa wingi wetu na ulofa wetu na kwa ujinga wetu tumewakataa sababu bado adui 'Ujinga' yupo anarandaranda na sasa hivi mmepandisha cheo ili azidi kutupumbazia wanetu.na yule mwingine 'Maradhi' huyu ndio balaa kila siku anachukuwa watu wetu na kutuacha wakiwa...

Hawa jamaa mmewashindwa kabisa kuwaondoa ,hivyo sisi tutawaondoa ninyi na kuweka wapambanaji wengine maana hali tuliyofikia tunashindwa hata kufikiri kwa akili zetu ...
 
Dhamira ya mtu ndo umwongoza mtu ..tayari umeonesha msimamo wake na sie tumetambua msimamo wake hata kama atalazimishwa lakini tumeelewa ana msimamo fulani na leo anatafuta urais kwahiyo hawezi kuwa na makuu sana lakini akishaupata utasikia anakwambia urais wake si wa ubia ..tunachoweza kuchukua hapa ni kwamba kÃ-tika hari ya kawaida yeye binafsi ayuko tayari kushiriki na watu wenye kariba ya Chenge na hatashiriki nao kamwe

Hapana kama kashindwa kuonyesha msimamo ktk hili dofo la mtu mmoja je ataweza la taasisi nzima mi nasubili akifika kwa pesa za mboga atafanyeje. The problem that created by the same system can not be solved by the same system with same thinking capacity.
 
Nimeskia kuwa mh. Magufuli aligoma kumnadi chenge jukwaan kwenye kampeni bariadi ,hadi na chakula kilichoandaliwa nyumbani kwa chenge hakula sababu ni tuhuma za ufisadi unaomwandama chenge ila amekubali baada ya kulazimishwa na CCM kufanya hivyo kwa kuwa nilazima kutii kanuni na sheria za chama na hatimaye akakubali kulegeza msimamo. Kama taarifa hizi ni za kweli kulingana na mtoa taarifa humu JF swali langu ni je ataweza kweli kuubadili mfumo mbovu uliomuweka madarakani kama akishinda uchaguzi? Kama hapo tu kashindwa kuwa na msimamo, hili linanitia shaka sana

Nimeambiwa, nimesikia, nahisi, wanasema, Nadhani, pengine hizo ni kauli za ujanjaujanja
 
Hizo pesa zinazomzungusha yeye na wasaniii anajua zinakotoka! Atakaa tu wala hawezi kufulukuta.
 
Magufuli anao uwezo wa kujisimami kama Raisi. Huyu mwingine, Tuhuma za; Utajiri usiojulikana chanzo yeye, Ufisadi yeye, kukumbilia udini haraka ni yeye! Nani atamdhibiti?
 
Hii mtu katunga ili kukwepa Maswali hasa ya Kujitapa kwa Magufuri na uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi. Alafu mmemaliza kutungwa na kuanza kutumia ID feki mkaaza kujijibu.
Magufuli HAJAWAHI kuwa hata KATIBU WA KIJIJI au KATA WA CCM....!!!

Magufuli si Lolote au chochote mbele ya CCM.... ni kama DEREVA wa BOSS tu...!!

Anapewa masharti na kufuata, atake asitake...!!!

TUNAMWOMBA MAGUFULI AMUUNGE MKONO LOWASSA tumalize kazi...!!!

CCM ni janga kuu, kama hadi leo hamjui mtaja juta mara elfu ya hivi sasa...!!

Lowassa, Ukawa ndio chaguo la Mungu
 
Kwahiyo Leo lowasa siyo fisadi tena au unataka kusema nini.

ufisadi wa Lowasa ni upi? chamsingi hatukitaki hicho chama ambacho kinatambua lowasa ni fisadi na bado hakimchukulii hatua. .kinatulalamikia sisi wananchi kuhusu ufisadi wa lowasa wakatI ndio wenye serekali na mamlaka stahiki ?
 
nilishasema magufuli ajiandae kulia au kulizwa. chezea papa mtunga katiba ambayo warioba kalegea? ccm hamna kitu
 
ufisadi wa Lowasa ni upi? chamsingi hatukitaki hicho chama ambacho kinatambua lowasa ni fisadi na bado hakimchukulii hatua. .kinatulalamikia sisi wananchi kuhusu ufisadi wa lowasa wakatI ndio wenye serekali na mamlaka stahiki ?

Leo Hamuoni Ufisadi Wa Lowassa Kwel?Miaka 7 Yote Mlivokuwa Mnamwita Fisadi Papa Mlikua Hamjui Ufisad Wake?
 
Uraisi ni tasisi nchi bora inajengwa kwa katiba bora Mtanzania kuwa na akili usiendeshwe endeshewe

Usitumie njia moja kuzani utapata majibu tofauti
 
Lowasa kaisha safishika,heri mtu y

HERI MTU YULE ASIYEKWENDA KATIKA SHAURI LA WASIO HAKI WALA HAKUKETI BARAZANI PA WENYE MZAHA.LOWASA ni msafi ameshajitenga na wasioitendea haki tanzania
 
Leo Hamuoni Ufisadi Wa Lowassa Kwel?Miaka 7 Yote Mlivokuwa Mnamwita Fisadi Papa Mlikua Hamjui Ufisad Wake?

kipindi chote akishutumiwa na wapinzani hakuwahi kukiri kuwa mwenye zigo la Richmond ni nani, lakini baada yakukiri hilo ndio tukapata picha kamili ya mchezo mzima , na ndio maana huyu tuliye aminishwa ni fisadi papa mpaka leo anadunda uraiani na zaidi anagombea uraisi, na serikali ibebaki kupiga kelele kama raia au wapinzani badala yakuchukua hatua stahiki, mwenye upeo pekee anaweza kuelewa haya yanayo endelea ktk siasa majitaka za ccm
 
Kwa hili tunapaswa kujiuliza maswali kama haya;

Fisadi ni nani kwa mujibu wa CCM?

Je CCM inaweza kuwapitisha mafisadi kugombea uongozi?

Je chama kinafaidika kutokana na vitendo vyao vinavyotafsiriwa kuwa vya kifisadi?

Je mtu aliyepitishwa na chama ambacho hao wanaoitwa mafisadi wana nguvu kubwa kukiongoza anaweza kuwapinga?

..........................................................................?
 
Hivyo ndivyo atakavyofanya akiwa Rais. Ataongoza kwa shinikizo la chama
 
Umesikia, but huna uhakika. jamaa ana msimamo, na huwa hayumbishwi na kitu au mtu. ngoja aingie ikulu watu watashika adabu. mafisadi wezi na watendaji wa serikali wabovu na wazembe watakiona cha moto. Nyerere + Mkapa =Magufuli

Bahati mbaya urais una mwenyewe hivyo nafasi hiyo ya kumshughulikia master wake JK hawezi kuipata labda kwenye chama chao kitakapounda kambi rasmi ya upinzani bungeni.

#Mabadiliko Ni Lowassa
 
Magufuri atawanyoosha aisee ngoja kwa sasa awe mpole aingie IKULU.

Kabla ya kumnyoosha mwenzio wewe mwenyewe ni lazima uwe umenyooka vizuri. Magufuli si chochote si lolote kwa Chenge. Magufuli hata kama ingetokea akawa Rais hana uwezo wowote wa kushughulikia ufisadi kwani hata yeye ni fisadi. Hayupo kwenye System. Kila kitu kipo corrupted ndaniya serikali ya CCM kwa sasa. Huu ni ushabiki tu wa kampeni. Shughuli ipo ndani.
 
Magufuli hajashauliwa na hajalegeza msimamo wake kuhusu kutowanadi wale wana makandokando ya ufisadi.

Nadhani kuna watu wanatamani sana wamuone Magufuli akinadi wale wanaojulikana kama mafisadi ili wapate hoja.

Magufuli hana urafiki na mafisadi na pia anachukia ufisadi kwa vitendo.
 
alikuwa anajaribu kutengeneza liuongo likubwa kwa watanzania lakini hata hivyo kashindwa kwani kabla ya chakula alimnadi kwa kumshika mkono na kumtangaza kama ni mtu safi. Mtu makini haibiwi mwaka huu.
weka picha akionyesha anamnadi sio unaleta umbea umbea
 
Misimamo yoyote isiyoweza kubadilisha chochote katika mustakabali Wa nchi MISIMAMO MFU; haina tija na mtu Wa aina hiyo ni laghai asiye na mfano, ni Nyoka aliyavaa Ngozi ya Kondoo; hatufai, ni Wa kumuogopa Kama Ebola; Mtu mwenye dhamira Safi hutamka na kutenda bila kuyumba, Magufuli Is a weakling, hawezi kukabiliana na mahafidhina ndani ya mfumo Wa kifisadi Wa CCM.

Dhamira ya mtu ndo umwongoza mtu ..tayari umeonesha msimamo wake na sie tumetambua msimamo wake hata kama atalazimishwa lakini tumeelewa ana msimamo fulani na leo anatafuta urais kwahiyo hawezi kuwa na makuu sana lakini akishaupata utasikia anakwambia urais wake si wa ubia ..tunachoweza kuchukua hapa ni kwamba kÃ-tika hari ya kawaida yeye binafsi ayuko tayari kushiriki na watu wenye kariba ya Chenge na hatashiriki nao kamwe
 
Dhamira ya mtu ndo umwongoza mtu ..tayari umeonesha msimamo wake na sie tumetambua msimamo wake hata kama atalazimishwa lakini tumeelewa ana msimamo fulani na leo anatafuta urais kwahiyo hawezi kuwa na makuu sana lakini akishaupata utasikia anakwambia urais wake si wa ubia ..tunachoweza kuchukua hapa ni kwamba kÃ-tika hari ya kawaida yeye binafsi ayuko tayari kushiriki na watu wenye kariba ya Chenge na hatashiriki nao kamwe
Hakuna aliye juu ya Chama! Na chama si mwenyekiti au kiongozi mmoja?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom