Maelfu ya wanachama wa CHADEMA wampokea Dr. Magufuli na kujiunga na CCM

Robethn

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
2,103
352
Maelfu ya wakazi wa Bariadi wampokea Magufuli, wakiwemo wanachama wa chadema jimbo hilo ambao wameamua kujiunga na CCM.


Mgombea Urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Lamadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi hao wanaondokana na tatizo sugu la upatikanaji maji.



Mgombea Urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Lamadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi hao wanaondokana na tatizo sugu la upatikanaji maji.
Mgombea Ubunge jimbo la Busega Dk. Raphael chegeni akihutubia wakazi wa mji wa maji kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizoongozwa na mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani (kushoto) ,wakipena mikono na Mgombea ubunge wa jimbo la Busega kupitia CCM Dk. Raphael Chegeni wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika mji wa Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani akiteta jambo na mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano na wakazi wa mji wa Lamadi, Busega.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi Sapiwi wakati akiwa njiani kuelekea Meatu.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa bariadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa CCM Saba saba.
Wananchi wa Bariadi wakishangilia kwenye mkutano wa mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli




















5.jpg
1.jpg


Report photo



 
Mleta mada hapo sio bariadi!!!

Kama kweli ni.bariadi yuko wapi mbunge mtarajiwa???
 
Wapi joka la makengeza a.k.a Mzee wa Vijisenti? Siwezi kuamini pasipo kumuona mtu huyu!vinginevyo tumeliwa!
 
Jamani hali ni mbaya sana ccm...kwa mujibu wa kikao cha usalama ndani ya ccm kilichokaa jana kidogo kivunjike kutokana na watu kulaumiana na wengine kushikana mashati...baada ya ripot kutoka kuwa kwa miujibu wa takwimu uchaguzi ukifanyika leo lowassa lazima ashinde kwa asilimia 70 huku magufuli akiambulia 13...kikubwa kilichojadiliwa ni baadhi ya wanamipango kushindwa kutumia 150 billion zilizotengwa kuisambaratisha ukawa..huku kazi iliyokwisha fanyika kwa Lipumba..slaa..ray kagosi na aunt ezekiel zikilaumiwa kutumia zaidi ya bilion 20 bila kuzaa matunda yeyote..huku baadhi ya wajumbe wakishikana mashati kwa kutuhumiana kumuunga mkono lowassa chini chini..sasa mwisho ikaamuliwa hivi..katika hawa..MBOWE..MBATIA..MNYIKA..LISSU..MSIGWA..LEMA..BAREGU..PROF SAFARI.MZEE MAKIHIDI....mmoja ni lazima apatikane kwa gharama yoyote na aisaliti ukawa na kuhamia ccm kwa kishindo...ile timu ya kwanza iliyopewa kazi imeambiwa ikae pembeni..imechaguliwa timu mpya ikiongozwa na kinana na january makamba...na imepewa hadi tarehe 4/10 Iwe tayari imeshafanya kazi hiyo ya kuisambaratisha ukawa?? Na wakaja na mbinu mpya yaani PLAN A...NA PLAN B...NA PLAN C..ni kwamba endapo plan a itafeli basi itumike plan b ..ambayo ni kikwete na timu ya marais wote wastaafu kwenda kumuangukia lowassa arudi ccm na kuitekeleza ukawa..plan hii ikishindikana na lowasaa akikataa ni wamtume kikwete kwenda kuongea na lowasaa waweke makubaliano ya kwamba endapo atashinda urais kuwa akuna mambo ya kukamata mafisadi waliousika na wizi wa mali za umaa..na endapo plan zote hizo zikikataa watatumia plan ya mwisho ambayo ni General Dennis mwamunyange kuchukua nchi kwa kishindo....kwa hiyo timu imeanza rasmi kazi jana...tuweni makini jamani maana hizo 150 billion siyo mchezo...ukisikia kiongozi yeyote wa juu akiondoka ukawa na kufanya mambo ya hajabu ujue tayari...hali ni mbaya sana ndani ya ccm kiasi kwamba hata kikwete amuamini kinana anahisi pia anatumia na lowassa yaani sasa hivi ni kushikana mashati....wanajiuliza eti..endapo mikutano yetu ingekuwa aina Diamond..ali kiba..yamoto band..basi tungekuwa tumeshashindwa mapema maana hata mgombea wetu anaongea zaidi kama mpinzani na siyo mwana ccm...hotuba zote tulizomuandalia amekuwa akikataa kuzitumia huku akiibuka na hotuba zake za ajabu ambazoo zinakinzana na mwenyekiti wake kikwete....jamani makamanda kuweni makini pesa imetoka hiyo
 
sisi wanabaryati tunaogopa sana wezi wa ng'ombe kuliko kitu chochote na tumeshapigana nao vita vingi sana,,,,,hatuwezi kuchezea shilingi chooni bana
 
Back
Top Bottom