Maelfu ya raia waandamana Italia

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Maelfu ya raia wa Italia wameandamana katika mitaa mbalimbali ya mji wa Roma kupinga sera za kiuchumi za serikali ya nchi hiyo.

Waandamanaji hao wamedai kuwa serikali ya nchi hiyo iliyoingia madarakani mwaka 2018 imeshindwa kushughulikia tatizo la kukosekana kwa ajira pamoja na ubaguzi wa rangi.

Muungano wa vyama vya Wafanyakazi nchini Italia umesema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo umekua ukikua taratibu na pia hakuna ajira za kudumu hasa kwa kundi la vijana.

Muungano huo umefafanua kuwa kiwango cha watu wasio na ajira nchini Italia ni asilimia 9.7 na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ya tatu katika nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) baada ya Ugiriki na Hispania zenye kiwango kikubwa cha watu wasio na ajira.

Tbc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dunia kuna wakati huwa inanipa raha sana, hispania wanaandamana, ufaransa wanaandamana( maandamano yao wanayaita yellow vest) sasa italia nao wanaandamana...si muda uingereza nao wataandamana
 
Write your reply...
viongozi wanashindwa kukimbizana na wakati, wakati teknolojia inaongezeka ajira zinapungua na watu wanaongezeka, sasa hapo ndipo panapozuka songombingo la ajira
 
Hii dunia kuna wakati huwa inanipa raha sana, hispania wanaandamana, ufaransa wanaandamana( maandamano yao wanayaita yellow vest) sasa italia nao wanaandamana...si muda uingereza nao wataandamana
Urusi ya puttin na Washington ya Trump raia zao wanaponda Raha ndo Raha ya ubabe duniani, unaiba Syria unalisha wananchi wako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom