Maelfu ya maafisa wa polisi wametawanywa Paris kukabiliana na waandamanaji wanaopinga kuanzishwa pasi maalumu ya afya kwa waliochanjwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Maelfu ya maafisa wa polisi wametawanywa kote mjini Paris kukabiliana na waandamanaji wanaopinga kuanzishwa pasi maalumu ya afya kwa wale waliochanjwa dhidi ya virusi vya corona.

Zaidi ya polisi 3,000 na maafisa wa usalama wameuzunguka mji mkuu wa Ufaransa Paris Jumamosi wakati maelfu ya waandamanaji wakiwa wamekasirishwa na mpango wa serikali wa kuanzisha pasi maalumu kwa waliopigwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Nchini kote, watu wapatao 204,000 wameshiriki maandamano hayo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani. Idadi hiyo ya watu imeongezeka ikilinganishwa na ile ya wikiendi iliyopita.

Katika jiji la Paris, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika mikusanyiko minne tofauti mjini humo.

Polisi hao walikuwa wanajaribu kuwazuia waandamanaji kuingia katika barabara maarufu ya Champs-Elysee, ambayo ilitawaliwa na maandamano ya "vizibao vya manjano" yaliyokuwa na vurugu mnamo mwaka 2018.
Msemaji wa polisi amesema maafisa watatu wa polisi wamejeruhiwa na waandamanaji wakati wa makabiliano hayo ya siku nzima.

Kuanzia Agosti 9, pasi mpya za afya zitahitajika kwa raia kuweza kusafiri na kuingia kwenye maeneo ya biashara, kama vile migahawa, vinyozi, pamoja na kupanda kwenye treni au kushiriki kwenye maonyesho tofauti, pendekezo hilo bado linasubiri idhini ya Baraza la Katiba. Aidha upigaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona itakuwa lazima kwa baadhi ya wafanyakazi.

Maandamano hayo yamekuwa yakiendelea kwa Jumamosi ya tatu mfululizo. Na hayafanyiki tu mjini Paris, lakini pia kwenye miji mingine ipatayo 100 nchini kote, ikiwa ni pamoja na Montpellier, Bordeaux, Marseille na Nice. Afisa wa wizara ya mambo ya ndani amesema zaidi ya watu 200,000 wameandamana kote Ufaransa.
 
Bunge lilishapitisha ,imebaki mahakama kuikubali, na mtu ambaye hajachanjwa atafukuzwa kazi iwe serekalini au kampuni binafsi, na hayo yote mleta uzi alioongea. Jamaa mmoja akasema Kwa nn nchi kubwa kama u Faransa iendeshwe Kwa matakwa ya watengeneza chanjo (Pfizer), so alisema wapewe chanjo ya 3 itabidi wakubali, ikibidi wawekewe tatoo au kitu mwilini serekali itapitisha. Kuanzia mwezi wa kumi wa 10 mtu atakua analipia chanjo hiyo
 
Back
Top Bottom