field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,730
Ni mara nyingi sana inatokea kuona polisi wetu wakisimama kwenye podium kuzungumza na waandishi wa habari, wanachozungumza mara nyingi ni "watuhumiwa walipigwa risasi na wakafa wakikimbizwa hospitali" Wakati huo huo hakuna ushahidi wa polisi kushambuliana na hao wanaowaita wahalifu, wananchi hawaoni na kuhakikisha kuwa kulikuwa na milio ya risasi.
Miaka ya nyuma, Zombe na wenzake walileta hadithi inayofanana na haya yanayoendelea....Kirahisi rahisi wafanyabiashara wakauawa, huku wakisingiziwa ni majambazi, hadi tume ilivyoundwa ikathibitisha kuwa wale ni wafanyabiashara waliopelekwa Mabwe pande na kuuliwa huko.
Sasa haya leo yameshamiri, polisi wanatatua matatizo yao kwa kuua, kwa nini wasiwashike? Kweli kuna asiye na akili akataka kupigana na panga na polisi walio na silaha kali? Katika kipindi cha wiki 3, watu/wananchi 19 wameshapoteza maisha mikononi mwa polisi. Maelezo yao polisi wetu hayaeleweki. Yaani ya kuunga unga tu!
Nani leo hii atawaamini polisi wanaoua watu wasio na makosa? Kwanini wasiwakamate washukiwa wa ujambazi ili waweze kuwataja wauaji wengine? Na mbona hawaonyeshi sehemu kulipokuwepo hayo mapambano? Wanaonyesha mapanga yenye damu (Polisi wanajua ukweli kuwa wanadanganya)
Polisi wetu hamna credibility, mnaua, mnatesa na kuumiza wananchi wasio na hatia. Hakuna anayewaamini kwa matendo yenu.