Maelezo ya Naibu Spika kuhusu tozo na makato ya benki na makampuni ya simu ni upotoshaji?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
851
1,077
Naibu spika amenukuliwa akilaumu wananchi kuwa malalamiko ya tozo ni makubwa wakati taasisi husika makato yake ni makubwa zaidi na kwamba huenda kuna njama tu za kukwamisha mambo ya serikali. Je, naibu spika hana taarifa kuwa:

1. Serikali kupititia hayo makato ya makampuni inapata kodi kubwa kama 30% corporate tax,income tax nk?

2. Makato hayo ni sehemu inayotumika kama mishahara hivyo kupatia serikali kodi PAYE?

3. Hana habari kuwa baada ya kuweka tozo mauzo ya makampuni yalishuka na hivyo corporate na income tax zilipungua sana?

Na iwapo mapato yakipungua zaidi upo uwezekano wa wafanyakazi kupoteza ajira hivyo kukosa PAYE? Achilia mbali ajira za vijana zilizopotea kutokana na kufungwa kwa maduka ya biashara ya fedha?kufungwa kwa maduka haya kumepoteza mapato kiasi gani kutokana na malipo ya leseni?

Viongozi waache kupokea maelezo ambayo yanazidi kupotosha mambo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom