SolarPower
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 223
- 27
Wakuu,
Natumaini wote jana mlifanikiwa kusikiliza hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa jana usiku. Kati ya mambo ambayo Rais Kikwete aliyoongelea jana ni pamoja na namna ambavyo serikali hutoa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na wale wa kutoka nje ya nchi yetu.
Katika hili Mheshimiwa Rais alilieleza taifa kuwa Wawekezaji hupatiwa ardhi ya Uwekezaji Kupitia Kituo chetu cha Uwekezaji TANZANIA INVESTMENT CENTRE (TIC). Katika ufafanuzi wake alilieleza taifa kuwa Kila wilaya imetenga maeneo maalum ya ardhi ya uwekezaji ambapo ardhi hizo ziko chini ya Benki ya Ardhi inayosimamiwa na TIC.
Katika kipindi cha TUAMBIE kilichorushwa na TBC kama wiki moja na nusu iliyopita, maafisa wa TIC walilieza taifa kuwa toka TIC ianzishwe ardhi ambayo TIC wameishaitoa kwa wawekezaji wa ndani na nje mpaka sasa haifiki Hekta 17,000. Lakini gazeti la The East African la tarehe 14-20 Mei 2012 katika ukurasa wake wa mbele lilitoa taarifa kuwa nchi yetu inaongoza katika kutoa ardhi kubwa kwa wageni ambapo mpaka sasa tumeishatoa kiasi cha Hekta 2,200,000 (kiasi cha kama ekari mil 5.6---mpaka sasa taarifa ya gazeti hilo bado haijakanushwa na Serikali yetu).
Je ni kwanini ardhi hii (Hekta mil 2.2) TIC hawakuhusika katika kuitoa kama ambavyo Mheshimiwa Rais alivyoeleza jana katika hotuba yake kuwa TIC wao ndiyo wahusika wakuu katika kutoa ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Taarifa hiyo ya Gazeti la The East African inaonyesha pia kuwa kampuni moja tu ya Sweden imepewa Hekta 797,000 ( kama ekari mil 2.02438).
Naomba kuwasilisha