Dkt. Mollel: CHADEMA walipanga njama za kumpiga risasi Lissu

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,707
15,163
Aliyekuwa mbunge wa CHADEMA kutoka jimbo la Siha jana ametema nyongo bungeni baada ya kuelezea namna viongozi wa CHADEMA walivyopanga njama za kumuuwa Lisu kwa kumpiga risasi na amesema kama wanabisha siku ikifika ataweka ushahidi wote hadharani!

Report ya Dkt Mollel sasa inaweza kujibu swali la kwa nini pamoja na kufyatuliwa risasi nyingi lakini hamna hata moja iliyompata dereva wa Lisu kwa sababu alikuwa anajua mchongo mzima na namna gani ya kujificha wakati risasi zikimiminwa.

========

Mbunge Dkt. Mollel akiwa Bungeni amesema fedha zinazopatikana kwenye rasilimali ambazo si endelevu(Mf. Madini) zinapaswa kuwekezwa kwenye maeneo ambayo yataendelea kulipa taifa pato hata zikiisha.

Nayo ni

1. Rasilimali watu
2. Miundombinu
3. Ugunduzi na Teknolojia

Pia ameeleza kuwa wakati sisi tunawekeza huko, kuna baadhi ya nchi ambazo rasilimali zao zimekwisha hivyo wanatafuta maeneo katika nchi zetu ili waweze kuwekeza kwenye rasilimali zetu na kuzipa nchi zao nguvu.

Katika kutoa mfano wa hilo, Dkt. Mollel anadai kuwa akiwa CHADEMA chini ya Mbunge Selasini, walikuwa wakipanga mikakati ya kuzuia Serikali isiwekeze maeneo hayo.

Katika mkakati huo ikaonekana kuwa Tundu Lissu anajipatia umaarufu binafsi hivyo wakampiga risasi na kumuumiza.

Anasema mkakati huo ndio unaendelea hadi sasa Ulaya ukifadhiliwa na watu wachafu wenye nia ya kuiba rasilimali za Watanzania. Anasema suala la Lissu liko wazi sababu hata Chacha Wangwe alipotaka Uenyekiti nini kilimpata?

Mabomu ya Arusha

Akizidi kukandamizia point yake, Mollel amesema alikuwa Daktari mwakilishi wa CHADEMA kipindi cha Mabomu ya Arusha na alipotoka kwenye chumba cha uchunguzi(post mortem) aliwaeleza viongozi wake kuwa ameiba vitu kadhaa toka kwenye chumba hicho hivyo wavipeleke Afrika ya Kusini kwa ajili ya uchunguzi lakini walikataa licha ya kuwa na Ruzuku.
 
Basi jamani utata umeisha,bwana mollel unaambiwa anao ushahid wooooteeeeee, ila atautoa tu pale chadema itakapoeleza matumizi ya ruzuku
Kwa hiyo tusubiri jeshi la polisi waongee na msajili wa vyama na CAG kuhusu ruzuku ili kumlainisha bwana mollel atoe ushahidi wake huo
**Halii hii inaonyesha wazi kwamba ukihama cdm kwenda ccm akili zako zinaongezeka sana, Dr Mollel katisha vibaya mno.


mollel.PNG


Kwa ufupi
Mbunge huyo wa Siha aliyehama Chadema na kujiunga CCM amesema tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 ni mpango uliosukwa na Chadema ingawa hakuwa tayari kuthibitisha madai yake.


Dodoma. Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel amesema tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 jijini Dodoma ni mpango uliosukwa na Chadema na kutoa sharti kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kuwa wakilitimiza atakuwa tayari kuthibitisha.

Dk Mollel, mbunge wa zamani wa Siha kwa tiketi ya Chadema aliyejiunga CCM mwaka 2018 na kupitishwa kuwania ubunge na kuibuka na ushindi, ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Februari 8, 2019 bungeni jijini Dodoma.

Amesema hata siku ya kufanya uchunguzi baada ya Lissu kupigwa risasi, kuna baadhi ya sampuli aliziiba lakini uongozi wa Chadema ulikataa pendekezo lake la kupeleka sampuli hiyo Afrika Kusini kufanya uchunguzi kwani walikuwa na hofu ya kuumbuliwa.

“Mimi nilikuwa huko lakini nilikimbia kwa mipango yao, hata katika tukio la kushambuliwa Lissu mimi niliingia ndani kwenye uchunguzi na niliiba baadhi ya vitu lakini wakakataa mapendekezo yangu," amesema Mollel.

Hata hivyo, mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka aliomba taarifa akimtaka Dk Mollel kueleza ni kwa nini alikuwa anakiuka kiapo cha udaktari, na mbunge huyo wa Siha kujibu kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa kada mwaminifu wa Chadema.

Wakati Mwakajoka akieleza hayo, mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alimtaka Dk Mollel kuthibitisha madai yake kuhusu Lissu.

Katika majibu yake Dk Mollel amesema hawezi kuthibitisha hadi Chadema watakapomueleza fedha za ruzuku zinakwenda wapi na mpango waliotaka kuufanya kwa Zitto Kabwe (mbunge wa Kigoma Mjini) na marehemu Chacha Wangwe, walipotaka kugombea uenyekiti wa Chadema.

Soma Zaidi: Alichokisema dereva wa Lissu katika mahojiano Ujerumani
 
Basi jamani utata umeisha,bwana mollel unaambiwa anao ushahid wooooteeeeee, ila atautoa tu pale chadema itakapoeleza matumizi ya ruzuku
Kwa hiyo tusubiri jeshi la polisi waongee na msajili wa vyama na CAG kuhusu ruzuku ili kumlainisha bwana mollel atoe ushahidi wake huo
**Halii hii inaonyesha wazi kwamba ukihama cdm kwenda ccm akili zako zinaongezeka sana, Dr Mollel katisha vibaya mno.


View attachment 1017124

He is retarded. CHADEMA ndio walioondoa walinzi na kamera? Si awape huo ushahidi wanaohangaika kujisafisha? Kweli kuwa ccm ni lazima uache kufikiri kabla hujaongea au kutenda.
 
Basi jamani utata umeisha,bwana mollel unaambiwa anao ushahid wooooteeeeee, ila atautoa tu pale chadema itakapoeleza matumizi ya ruzuku
Kwa hiyo tusubiri jeshi la polisi waongee na msajili wa vyama na CAG kuhusu ruzuku ili kumlainisha bwana mollel atoe ushahidi wake huo
**Halii hii inaonyesha wazi kwamba ukihama cdm kwenda ccm akili zako zinaongezeka sana, Dr Mollel katisha vibaya mno.


View attachment 1017124
Ntajitahidi kufunika pembe la ng'ombe Lakin hafichiki
Mbona mnaruka ruka tulieni mliyataka wenyewe
Anawaanika Kwel Kwel hadi naona aibu mimi huku Germany had tunaona aibu kutoka street

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe chadema ni balaa mpk waliweza kuwaondoa maaskari pale getini wakaweza kuondoa na CCTV aisee,ni makomandoo hawa.

Ujinga mwingine kuujadili ni upuuzi wa daraja la kwanza tu,dokta sindano za ng'ombe zimeshamchanganya huyo.
 
Namwomba afande Siro amwite Mollel akasaidie upelelezi. Haiwezekani mpaka leo kitendawili cha nani alitaka kumwua Lissu hakijateguliwa wakati key witness kajitokeza mwenyewe kwa hiari yake bila kualzimishwa na mtu.

Imani yangu kesho asubuhi Mollel atakuwa ameripoti polisi!
 
Kwa serikali hii ya Magufuli, kama wangekuwa na ushahidi wa shambulio la Lissu wangeutoa siku hiyo hiyo na wahusika wangekamatwa.


Lakini cha ajabu wamebaki kusema leteni dereva ahojiwe.

Mara tunamfutia Lissu ubunge, mara mshahara unasitishwa, mara blaa blaa gani.....

Haya leteni huo ushahidi tena wa CCTV camera mlizozificha
 
Back
Top Bottom