Maelezo juu ya dawa Abacavir inayotibu Vijidudu vya Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo juu ya dawa Abacavir inayotibu Vijidudu vya Ukimwi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 13, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Maamuzi juu ya matibabu ya aina mbalimbali
  yanahitajika kufanywa kwa kushauriana na mtaalamu
  aliyehitimu kwenye mambo ya afya na mwenye ujuzi
  juu ya magonjwa yanayoendana na maambukizi ya
  vijidudu vya ukimwi na matibabu atakayoamuliwa
  kutumiwa
  www.catie.ca www.apaa.ca
  Abacavir (ABC, Ziagen)
  Maelezo juu ya dawa
  Kwa Nini Nimepewa Dawa Ya Abacavir? Abacavir (kwa jina lingine Ziagen) ni dawa inayotumika pamoja na mchanganyiko wa dawa nyingine kutibu maambukizi ya vijidudu vya ukimwi. Abacavir pia hupatikana kwenye dawa nyingine ya kupigana na maambukizi ya vijidudu vya ukimwi inayoitwa Trizivir. Abacavir husaidia kuzuia protini inayoitwa “reverse transcriptase.” Kutokana na kazi hii, dawa hii huwekwa kwenye kundi la dawa zinazoitwa Reverse Transcriptase Inhibitors (RTIs). Vijidudu vya maambukizi ya ukimwi huhitaji protini hii ili kuzaliana, kwa hiyo kwa kuwa dawa hii huzuia protini hii inasaidia kupunguza nguvu za ugonjwa wa maambukizi ya vijidudu vya ukimwi. Matumizi ya dawa hii huweza kupunguza wingi wa vijidudu vya maambukizi mwilini mwako. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa yanayoendana na ukimwi, na kukuwezesha kuwa na afya njema kwa muda mrefu au kukurudishia afya yako kabisa. Vilevile dawa hii husaidia kupunguza uharibifu wa mfumo wako wa kupigana na magonjwa.
  Nitatumiaje Dawa Hii? Abacavir huja kwenye mfumo wa vidonge vya miligramu 300 na vile vile kama dawa ya kunywa (20 miligramu/cc). Kiwango cha kawaida cha matumizi cha Maamuzi juu ya matibabu ya aina mbalimbali
  yanahitajika kufanywa kwa kushauriana na mtaalamu
  aliyehitimu kwenye mambo ya afya na mwenye ujuzi
  juu ya magonjwa yanayoendana na maambukizi ya
  vijidudu vya ukimwi na matibabu atakayoamuliwa
  kutumiwa

  abacavir (ABC, Ziagen)
  Abacavir ni miligramu 300 mara mbili kwa siku. Abacavir huweza tumika kabla au baada ya chakula. Ni muhimu kuhifadhi abacavir kwenye joto la kawaida kwenye sehemu kavu. Epukana na kuhifadhi dawa hii bafuni au jikoni, kwani unyevunyevu huweza ipotezea dawa hii nguvu yake. Hifadhi dawa hii mbali na watoto.
  Nifanye Nini Nikisahau Kunywa Vidonge Vyangu? Meza dawa zako ulizosahau mapema iwezekanavyo. Ikiwa ni karibu na saa mbili kabla ya muda wa kumeza dawa nyingine, endelea na ratiba yako ya kawaida. Usimeze dawa zako mara mbili ya kiwango utakiwacho ili kulipizia ile uliyosahau. Tafiti za kisanyansi zilizofanyika karibuni zimegundua kuwa ili dawa za kupigana na maambukizi ya vijidudu vya ukimwi ziweze kufanya kazi vizuri, dawa zote hazina budi kutumiwa mara kwa mara na kwa mfululuzo ilivyoelekezwa. Kuacha au kuruka kumeza dawa zako kunasababisha kupungua kwa nguvu za dawa hizi na kuvifanya vijidudu vya maambukizi kubadilika na kuwa sugu kwa dawa.
  Madhara Ya Yaletwayo Na Matumizi Abacavir Ni Yepi? Madhara makuu ya kutumia abacavir ni kusisimka kwa mwili kutokama na viamsho vya allergies kama vile kupiga chafya, upele mwilini n.k (hypersensitivity reaction – allergies) ambayo huwa na dalili za magonjwa ya mafua. Hii hutokea kwa asilimia 3 ya watu wanaotumia abacavir na huweza sababisha hatari kubwa. Dalili hizi huweza kuambatana na homa na kujisikia baridi, maumivu ya misuli na mifupa, kuchoka kwa kila mara na kujisikia mnyonge, kichefuchefu na kutapika, kupatwa na upele mwilini au kupumuwa kwa shida. Ukiwa na dalili mbili au zaidi zilizotajwa hapo juu, tafadhali kamuone daktari wako mara moja bila kuchelewa. Usiache kutumia dawa hii kabla ya kuonana na watu wa afya wanaokuhudumia.
  Swahili:

  Shirika la kubadilishana maelezo juu matibabu ya ukimwi Kanada (The Canadian AIDS Treatment Information Exchange – CATIE) na Shirikisho la waafrika katika kupigana na ukimwi (Africans in Partnership Against AIDS - APAA) kwa nia nzuri kabisa wanatoa maelezo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya vijidudu vya ukimwi/Ukimwi ambao wangependa kutawala afya zao wenyewe kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wanaowapatia matibabu. Hata hivyo, maelezo haya yanayochapishwa au kutolewa na CATIE au APAA hayawezi kuchukuliwa kama ushauri wa kiafya. Hatushauri au kusisitiza juu ya tiba moja juu ya nyingine. Hivyo tunawashauri watumiaji ya maelezo yetu kupitia maelezo ya matibabu mengine yanayotolewa na vyanzo mbalimbali kwa upeo mkubwa iwezekanavyo. Tunawashauri watumiaji wa maelezo haya na kusisitiza kuwa ni muhimu kushauriana na wataalamu ya afya na tiba waliohitimu mafunzo yao kabla ya kuamua, kutumia au kuanza jambo lolote juu ya matibabu.
  Vile vile, hatuthibitishi au kudhamini ukweli au ufarisi na ujuzi wa maelezo yanayochapishwa au kupatikana kutoka CATIE au APAA. Watumiaji wanaotumia au kutegemea maelezo haya wanafanya hivyo kwa kuthubutu wenyewe na matokeo yake yakiwa mabaya yatakuwa juu yao. Si CATIE wala APAA, au Wizara ya Afya Kanada, au wafanyakazi wao, wakurugenzi, maafisa au watu wanaojitolea wataweza kuhusishwa na uharibifu wa aina yeyote unaoweza kutokea kwa kutumia vizuri au vibaya maelezo haya. Mawazo na maelezo yaliyotolewa hapa au kwenye nakala yeyote au ilani/tangazo lolote
  Copyright: This Fact Sheet is made available through a collaboration between Africans in Partnership Against AIDS (APAA), Asian Community AIDS Services (ACAS) and the Canadian AIDS Treatment Information Exchange (CATIE). Original content developed by ACAS, 2001. Translation into Swahili and Hausa by APAA, 2004.
  Funding has been provided by Health Canada, under the Canadian Strategy on HIV/AIDS
  Supported by an unrestricted educational grant from
  GlaxoSmithKline in partnership with Shire BioChem
  Swahili: Abacavir languages.catie.ca 4
  This information is also available in Chinese, Tagalog and Vietnamese http://www.treathivglobally.ca/african/pdfs/Swahili/Abacavir.pdf
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kutibu?

  For real for real? Ukimwi ushapata tiba?
   
 3. M

  Mbelakisa Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtaalam huyu hajajibu matakwa ya wahitaji, kwani bado hajaeleweka kama hiyo ni tiba au dawa ya kurefusha maisha. Kwa maana kama ilikuwa inatibu hajasema ni dozi ya muda gani? na hizi dwa zinapatikana wapi? naomba anitoe kimasomaso.
   
 4. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
 5. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kama dawa nyingine tu za kurefusha maisha and it has to be used in combination.
   
Loading...