Maelezo Jinsi ya kushughulikia vifaa vya kinga ya kibinafsi

Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,405
6,281
Disclaimer: Kutokana na katazo lililo tolewa na wizara ya Afya juu ya utolewaji wa Elimu kuhusu Virus vya Corona ( Covid-19) napenda kuchukua muda huu kukanusha kua huu uzi hauna lengo la kukiuka hilo agizo na halitaongelea Virusi tajwa hapo juu. Hivyo mods naombeni msifute uzi wangu.

Habarini wana jamvi. Natumai mko salama na mnachukua tahadhari zote kujikinga.

Lengo la huu uzi ni kutoa elimu juu ya uvaaji, uvuaji na kutupa vifaa vya kinga ya kibinafsi (personal protective equipments) kama glavu na mask etc.

Shirika la afya duniani halishauri mtu ambae hajapata maambukizi kuvaa glavu na mask lakini kwa kua mmepanick na kila mtu kaamua kujivalia tu anavyojiskia na elimu ya kuvaa hivi vitu hamna hivyo kupelekea kutuweka sisi ambao hatuvai hvyo vifaa kua kwenye Risk. Acha tu niwape elimu


Glavu
1. Anza kwa kunawa mikono vizuri na sabuni, kausha mikono vizuri kisha vaa glavu kama inavyoonekana kwa picha hapo chini.

2. Kwa watumishi wa afya wanaashauriwa kutumia glavu moja kwa mgonjwa mmoja. Hivyo jitahidi kubadilisha kwa mara nyingi kadri uwezavyo.

3. Vua glavu kwa jinsi inavyoonyeshwa hapo pichani. Ukivua weka kwenye dust bin maalum. Usichanganye glavu na taka zingine. Usitupe glavu kiholela ili kuepusha usambaaji wa magonjwa mengine.

4. Angalizo
● Usishike simu yako, usile chakula, kunywa maji huku umevaa glavu.

● Usimshike mwenzako na glavu

● Vaa glavu ukiwa nje (in public) usivae nyumbani kwako.

● Nawa mikono yako mara kwa mara

● Usijishike uso wako na glavu

Mask

1. Vaa mask kwa kufata maelekezo pichani

2. Badili mask kila baada ya masaa manne au kila ikiwa na ubichi

3. Vua mask kwa kufata maelekezo

4. Tupa mask kama ilivyoelekezwa hapo juu

Angalizo

● Usiishike mask hapo katikati

● Usiwe unaitoa na kurudisha kila ukitaka kuzungumza. Unazidi kujisambazia vijidudu.

● Jua aina sahihi ya mask inayotakiwa kuivaa.

● Usichangie mask na mtu mwingine yeyote.

Njia sahihi ya kujikinga ni kunawa mikono vizuri kadri uwezavyo na kutojishika macho, pua au mdomo. Na kukaa mbali japo mita 1 kutoka kwa mtu mwingine ( distancing)


disposable-glove-donning.jpeg
Screenshot_20200324-232722_Chrome.jpeg
Screenshot_20200325-110733_WhatsApp.jpeg
GettyImages-175511668-1445x962.jpeg
mask-wearing-guide-e1580353261286.jpeg


Wearing gloves can actually increase your risk of catching coronavirus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu, ikiwa umevaa mask & Gloves je kuna utaratibu kifaa kipi kianze kuvuliwa kabla ya kingine?
 
Back
Top Bottom