Maelezo jinsi Mke wa Bilionea Msuya alivyomuua wifi yake yasomwa mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,439
Mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Mrita ameeleza sababu na namna alivyohusika na mauaji ya wifi yake, Aneth Msuya.

Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji hayo ya wifi yake huyo Aneth aliyeuawa Mei 25, 2016 kwa kuchinjwa shingoni nyumbani kwake, Kibada Kigamboni , jijini Dar es Salaam, amekiri kuhusika na mauaji hayo, katika maelezo yake ya onyo.

Katika maelezo hayo, Miriam anaeleza kuwa aliamua kumuua wifi yake kwa sababu alikuwa anamfuata fuata katika suala la usimamizi wa mirathi ya mumewe, marehemu bilionea Msuya na kwamba katika kutekeleza mauaji hayo alimkodi mtu aliyemlipa Sh20 milioni.

Mbali na Miriam mshtakiwa mwingine katika keso hiyo namba 103 ya mwaka 2018 inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ni mfanyabiashara Revocatus Myella.

Maelezo hayo ya Miriam yalisomwa mahakamani hapo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, WP Sajenti Mwajuma, aliyemhoji mshtakiwa huyo na kuandika maelezo yake alipotiwa mbaroni, baada ya kupokewa mahakamani hapo kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kwa mujibu wa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe, Bilionea Msuya ambaye aliacha wosia kuwa asilimia 40 ya fedha alizoacha benki wapewe wazazi na dada zake na asilimia 60 iliyobaki apewe mkewe na watoto wake.

Pia marehemu bilionea Msuya alieleza katika wosia huo kuwa mali nyingine zikiwemo magari, mgodi na hoteli zinapaswa kugawanywa kwa utaratibu wa mirathi.

Mshtakiwa huyo alieleza kuwa alifungua shauri la mirathi katika Mahakama Kuu Arusha kwa kumtumia wakili aliyechaguliwa na familia.

Hata hivyo baadaye aliliondoa shauri hilo mahakamani bila ya kumweleza wakili aliyechaguliwa na familia sababu za kufanya hivyo na kutafuta wakili mwingine bila ya kukaa kikao na wanafamilia.

Miriam aligawa fedha hizo za benki bila ya kuwa na mgogoro wowote asilimia 40 ilienda kwa wazazi na ndugu wa marehemu na asilimia 60 ilienda kwake na kwa watoto.

Kwa mujibu wa maelezo hayo baadhi ya mali za marehemu mshtakiwa huyo aliziorodhesha kwa jina lake jambo lililosababisha kutokuwa na maelewano mazuri na ndugu wa marehemu mume wake.

Mshtakiwa huyo alipata taarifa kuwa kuna ndugu wa mume wake jijini Dar es Salaam walipigwa risasi walikuwa wamelazwa lakini hakuwahi kuonana nao kwa sababu hawakuwa na mahusiano mazuri.

Baada ya tukio hilo la kupigwa risasi dada wa marehemu Bilionea Msuya ndipo likafuatia tukio la mauaji ya Aneth.

Katika maelezo hayo mshtakiwa huyo alikiri kuwa ndiye aliyehusika na mauaji hayo baada ya ya kuona kuwa alikuwa anamfuata fuata sana.

Katika kutekeleza mpango wa mauaji hayo mshtakiwa huyo alieleza kuwa alimpa kazi hiyo mtu anayeitwa Ray kwa makubaliano ya malipo ya Sh20 milioni.

Mshtakiwa huyo alieleza kuwa alimpigia simu Ray na kumuuliza kama anafahamu anapoishi marehemu Aneth lakini alimjibu kuwa hafahamu ila anajua anaishi Kibada.

Miriam alieleza kuwai Mei 15,2016 Ray alimpitia yeye mshtakiwa na wakaelekea Kigamboni eneo la Kibada wakiwa na gari lao aina ya Range Rover ili kutafuta nyumba aliyokuwa anaishi marehemu Aneth na walipofika eneo hilo walikutana na binti wa kazi wa Aneth.

Walimuuliza binti huyo kama anapajua nyumbani kwa Aneth naye akawajibu ni pale na yeye anaishi kwenye nyumba hiyo.

Walimuuliza binti huyo kama ana simu akawajibu hana hivyo walimuahidi kumnunulia na wakakubaliana kuwa Mei 18.2016 na wamkute nje ya nyumba hiyo na siku hiyo.

Siku hiyo, Mei 18 walikwenda na kumkuta binti huyo nje ya nyumba hiyo kama walivyokuwa wamekubaliana, hivyo wakampatia simu kwa ajili ya mawasiliano binafsi.

Wakati huo Ray alikuwa amebeba briefcase nyeusi ndani kulikuwa na sh10 milioni lengo lao kumuonyesha binti huyo akubali ombi lao ili siku ya tukio asiwepo nyumbani badala yake alitakiwa kuondoka.

Mei 23,2016 asubuhi Miriam alimpitia Ray na jamaa zake ambapo walikutana Magomeni kwa ajili ya kazi hiyo na ilipofika Mei 25, 2016 Miriam alipelekwa mkoani Arusha.

Mei 26,2016 Miriam akiwa Arusha alipata taarifa kwamba Aneth ameuawa kwa kuchinjwa na yeye, lakini hakwenda kwenye mazishi kwa sababu mama mkwe wake alikuwa amemwambia kuwa ikitokea yeye amekufa au familia ya mume wake asiende kwenye mazishi.

Mei 27,2016 Ray alisafiri na kuelekea jijini Arusha hadi kwenye hoteli ya mshtakiwa huyo ili akamaliziwe fedha zake zilizobaki kiasi cha Sh 10 milioni ambazo alipewa.

Baada ya kumaliza kusoma maelezo ya mshtakiwa huyo, shahidi huyo wa kwanza alieleza kuwa baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe Agosti 7,2016 alifanyiwa gwaride la utambuzi pamoja na watuhumiwa wengine kina mama na alitambuliwa na binti huyo.

Source: Mwananchi
 
Yaani hawa huwa hawaangalii movie kabisa.....mbona walipanga mchezo kizembe hvyo? Walimuongeza huyo binti wa kazi kwenye cycle kwa ajili ya nini? Kesi ipo wazi sana...lazima mtu ale mvua za kutosha.......kuna zile ambazo mtu anapotezwa bila hata kujua kama kuna foul play
 
Yaani hawa huwa hawaangalii movie kabisa.....mbona walipanga mchezo kizembe hvyo? Walimuongeza hyo binti wa kazi kwenye cycle kwa ajili ya nn? Kesi ipo wazi sana...lazima mtu ale mvua za kutosha.......kuna zile ambazo mtu anapotezwa bila hata kujua kama kuna foul play
Cycle tena?? Hakuna damu inapotea bure hata siku moja!

Hata asingekuwa connected nao ...wangedakwa tu
 
An
Wachaga kwenye wanaweza uwa kila mtu
Angalia nasaba au asili ya ukoo unapotaka kuoa au kuolewa hayo ndo matokeo ya yake ukiona kweny asili ya kabila la mtu au anapotokea wana tabia ya ukatili ,ukorofi, ukarimu, wasomi na nyingine basi na yeye atakuwa nazo kwa asilimia fulani

Kwa imani yangu hili swala la nasaba au asili ya ukoo fulani tunaangalia sana unapotaka kuoa wapo makabili ni wakatili hata iweje ndo asili na yao
 
Elimu inahitajika sana kwenye maisha ya kila Siku...huwezi kuua kijinga hivo halafu usikamatwe.

Wachawi ndo wauaji bora Sana kuwahi kutokea kwani hawaaji alama yoyote na wala hakuna kesi wala ushahidi..kwa utajiri aliokuwa nao huyu mama ilibidi aende kwa wachawi magwiji nchini kongo.
So ulitaka aue kitaalam zaidi sio?

Shabaaash

Terrible being you are
 
Mtu anachinjwa kama Mbuzi , halafu inategemea usikamatwe , Plan za mauaji za kishamba kabisa hizo , Yaani na simu walimnunulia Binti wa Kazi Ina maana walikuwa hawajui kuwa Wana acha alama ya ushahidi endapo wakifuatiliwa mitandaoni, Mijinga kabisaaa roho mbaya na choyo ime waponza wanastahiki kunyongwa na wao
 
Elimu inahitajika sana kwenye maisha ya kila Siku...huwezi kuua kijinga hivo halafu usikamatwe.

Wachawi ndo wauaji bora Sana kuwahi kutokea kwani hawaaji alama yoyote na wala hakuna kesi wala ushahidi..kwa utajiri aliokuwa nao huyu mama ilibidi aende kwa wachawi magwiji nchini kongo.

Uchawi ni imani. Mtu ambaye haamini uchawi huwezi kumdhuru kwa uchawi . Jiulize usa anavyowabonda waarabu why wanashindwa mroga usa kwa uchawi?

Bongo mauaji mengi ya kizembe sana. Evidence na traces zinaachwa nyingi sana kwenye crime scene.

Killers wa bongo wengi ni vilaza sana . Polisi wetu hawapati shida wala changamoto kumpata muuaji wakiamua tu. Maana kwenye crime scene wanakuta traces kibao.

Mfano hao wauaji kuweka urafiki na housegal mpaka wa kumnunulia simu kabisa na kumwambia aondoke siku ya tukio ni ujinga

Wataalamu wanasemaga hakunaga perfect murder crime. Ila kuna watu wanazifanya huko huko majuu na hawakamatwi milele
 
Back
Top Bottom