Maelekezo ya Baraza la maaskofu Tanzania kuhusu korona Virus.

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,033
23,873
*Maelekezo ya Baraza la maaskofu Tanzania kuhusu korona Virus*

1. *Sala*: Waamini wote wasali sala maalumu ya kumwomba Mungu atukinge na kutuepusha na maambukizi ya virusi vya korona

2. *Ibada* Ibada zote ziendeshwe kwa kuzingatia taratibu za kujikinga.

Waamini waelekezwe kuosha mikono kwa maji safi na sabuni

Maji ya baraka ya kuchovya yatasitishwa kwa muda(utumike utaratibu ufaao)

Hakuna kupeana mkono wakati wa kutakiana amani, waamini wafunge mikono na kuinamiana

Waamini watakomunika kwenye mikono na siyo mdomoni

Usishiriki kwenye jumuia ndogondogo kama unajisikia vibaya na ukishiriki jumuia usiazime kitabu, kila muumini atumie kitabu chake mwenyewe!

Wahesabu fedha wavar gloves na kutumia saniters

Mapadre wanapoadhimisha misa zaidi ya mmoja watachovya mwili na damu(maumbo)

3. *Sakrament*
Padre atatumia pamba kuwapaka wagonjwa mafuta na mapadre wanashauriwa kuambatana na wataalam wa afya

Katika kuungama padre asiangaliane moja kwa moja na muungamaji, kiti cha kitubio hakitatumika litumike eneo la wazi

4. *Ijumaa kuu*
Ibada ya ijumaa kuu waamini watainamia msalaba (hawatabusu au kushika)


5. *Mikutano ya vyama vya kitume*
Mikutano yote ya vyama vya kitume imesitishwa hadi hapo baadaye!

*Tusali na kuomba tuvuke katika hili*
 
Back
Top Bottom