Maelekezo: Jinsi ya kupanda na kushuka kwenye basi la Mwendo kasi (DART)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Karibu wageni katika Jiji la Dar es Salaam

Kama Siku nyingi hujaja Dar, safari hii ukija lazima ushangae na kutalii kidogo kwani tuna Daraja amizing, tuna barabara za mwendo kasi. So watu wa Mkoa karibuni sana.

Huo ulikua ni utangulizi tu, turudi kwenye Mada yetu sasa. Kwa wale wageni au wale ambao hawajawahi kutumia Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi(DART). Nmeanzisha huu uzi ili kutoa mwanga au ramani kwa ufupi ili kuwasaidia wale wanaotegemea kutumia huu usafiri ili ukifika usionekane mgeni sababu watoto wa mjini wanaweza kukuibia. Vilevile itapunguza usumbufu.

1.Tuanze na vile vituo ambavyo vinasumbua kutumia kama kituo cha Moroco Kinondoni, Ubungo na Kimara Mwisho.
DSCF8277-FILEminimizer.jpg

Daraja la Ubungo

Ili uweze Kupanda basi la Mwendo kasi kwa kutumia vituo hivi, Lazima Upitie kwenye Daraja la Watembea kwa Miguu, bila hivyo hutaweza kupanda hili basi sababu hakuna njia ya kuingilia tofauti na hii. Wapo walinzi watakuzuia kupita sehemu isiyo ruhusiwa, lakini Vituo vingine unaingia kama kawaida tu japo napo kuna wtu wa kukuelekeza cha kufanya.
tiketi.jpg

Sehemu ya kukatia tiketi

2. Ukishangia kwenye kituo cha kupandika gari, itabidi uende sehemu ya kukatia tiketi kama utakuta watu wengine panga foleni hadi zamu yako ifike, ni vizuri ukawa na hela isiyosumbua chenji ili kutokupoteza muda kusubili chenji sababu saa nyingine wale wanaotoza nauli wanaishiwa chenji. Ukishalipa nauli, utapewa tiketi yenye tarehe ya siku hiyo na muda na kiasi cha hela uloitoa, tatizo la hii ticket haioneshi unatoka wapi au unaenda wapi. (Usiitupe tiketi yako kwani utaonesha wakati wa kushuka pia)
tiketi2.jpg

Tiketi ukatayopewa baada ya kulipia, hiyo bacode nyeusi ndo utaiweka kwenye mashine ili iscaniwe

3.Ukishapewa Tiketi usiikunje, nenda nayo hadi sehemu ya kuhakiki kama kweli ni ya leo na haijatumika. Utakuta mashine maalum ya kuscan, utaisican bacode ya hiyo tiketi, kama inafaa mlango utajifungua, saa nyingine inagoma, lakini ikigoma subiri dakika moja urudie tena, kama itagoma itabidi umurudishie aliyekutatia ticket na umueleze tatizo, ataweza kukubadilishia.
90f56cd2-42e0-453e-b3a3-72b988bdc086.jpg

Mashine za kukagulia tiketi wakati wa kuingia na kutoka
scan1.jpg

Abiria wakiwa foleni ya kukagua tiketi ili waweze kuingia sehemu ya kusubiria basi
scan2.jpg

Mashine ya kukagua tiketi, tiketi yako inakaigusisha hapa iskaniwe ili mlango ujifungue

4. Ukishapita sehemu ya kukagua tiketi, utakuta viti utakaa, kama vimejaa utasimama kusubiri Basi la sehemu unapoenda, ikibidi uliza wahudumu kama basi lako lipo. kama halipo, subiri muda kidogo litafi.
kupanda.jpg

Abiria waliokuwa wamesubiria mabasi wakienda kupanda baada ya mabasi kufika

5. Gari likifa mtatngaziwa, Subiri wanaoshuka wakiisha ndo upande, kama hakuna anayeshuka panda na tafuta Kiti uketi(Kama ni mtoto kumbuka kuwapisha wakubwa kwako wakae), kama hakuna kiti simama na ushikilie vifaa vilivyowekwa kujishikiza kama mfupi shikilia nguzo au kiti cha abiria mwenzako alokaa.
kaa.jpg

Abiria wakiwa watulivu ndani ya basi

Unapokuwa ndani ya Basi la Mwendo kasi utulie, usiwasumbue abiria wenzio, Usichafue ndani ya gari wala kuharibu chochote ndani ya gari.
stop.jpg

kitufe kilichoandikwa STOP, kinabonyezwa unapofika mwisho wa safari yako ili dereva asimamishe basi

6.Kila kituo wanatangaza basi likikaribia kufika, au ukiona umekaribia kituo chako, kuna kitufe chekundu mbele ya kiti chako au pembeni, kimeandikwa STOP, basi kibonyeze ili basi ikifika isimame. Dereva anaweza akauliza kuna anayeshuka magomeni au Ubungo na usibonyeze au kusema kama unashuka basi utapitilizwa, gari ikishajaa hasimami kila kituo hadi kuwe na mtu wa kushuka. Hivyo ni vyema ukabonyeza ukikaribia kufika sio ukifika ndo ubonyeze kwani utapitilizwa, dereva anatakiwa apate nafasi ya kujiandaa kusimama.(Hakikisha mizigo ulopanda nayo unaiandaa kabla ya basi kusimama kwani muda ukiisha inaondoka na haina nisubiri)
IMG_8794.jpg

Abiri wakisubiriana wakati wa kupanda na kushuka
dd10f27c-c89f-4dc3-81d1-aa93c4950e0e.jpg

Abiria wakikaguliwa tiketi zao na kuchanwa baada ya kushuka ndani ya basi

Gari ikisimama, subiri Mlango ujifungue ndo ushuke. Ukishashuka, utaonesha tiketi yako na itachanwa ndipo utaruhusiwa kutoka. Utakoea ulipoingilia(Ubungo, Kimara mwisho na Moroco, itakulazimu upite juu ya daraja wakati wa kutoka)
darajani2.jpg

Abiri wakipita juu ya daraja la Kimara mwisho baada ya kushuka

Kwa leo ni hayo tu. Naamini itakusaidia hii japo kwa uchache tu. Mia
 
Hizi huduma bado Ni Za kizamani sana, labda uwajulishe hao wa mkoa, habari Za tiket kukaguliwa Na kuchanwa inapoteza muda wa abiria. Hapa walitakiwa waweke scan mashine ndani ya mabasi iwe unaweza kuilipia kwa ukubwa wa safari. Ukiingia Na kutoka iwe unascan.
 
Hizi huduma bado Ni Za kizamani sana, labda uwajulishe hao wa mkoa, habari Za tiket kukaguliwa Na kuchanwa inapoteza muda wa abiria. Hapa walitakiwa waweke scan mashine ndani ya mabasi iwe unaweza kuilipia kwa ukubwa wa safari. Ukiingia Na kutoka iwe unascan.
Wewe acha kujichanganya, Huduma gani tanzania tunatumia ambayo sio ya kizamani? Huu ujumbe nmekwandikia wewe kwa taarifa yako.
 
Wewe acha kujichanganya, Huduma gani tanzania tunatumia ambayo sio ya kizamani? Ondoa mishauo yako wewe. Huu ujumbe nmekwandikia wewe kwa taarifa yako.
ndugu si unajua watanzania much know hutakuta hajawahi hata kuutumia huo usafiri ambao anasema wa kizamani.
 
Hizi huduma bado Ni Za kizamani sana, labda uwajulishe hao wa mkoa, habari Za tiket kukaguliwa Na kuchanwa inapoteza muda wa abiria. Hapa walitakiwa waweke scan mashine ndani ya mabasi iwe unaweza kuilipia kwa ukubwa wa safari. Ukiingia Na kutoka iwe unascan.

We indian kwenu mnayo hayo?? Tuache kubeza kula kitu
 
Hizi huduma bado Ni Za kizamani sana, labda uwajulishe hao wa mkoa, habari Za tiket kukaguliwa Na kuchanwa inapoteza muda wa abiria. Hapa walitakiwa waweke scan mashine ndani ya mabasi iwe unaweza kuilipia kwa ukubwa wa safari. Ukiingia Na kutoka iwe unascan.

Wew mshamba acha usasa sisi tuache na uzamani wetu...hata jina lako tu linaonyesha namna gani unarukia vitu
 
Figfa upo? Dar kama ulaya sio, nakuja kushangaa mkuu, uje unipokee ubungo
 
Wasiwasi ni je hii changamoto ya mashine wakati flani kushindwa kuscan barcode za ticket, baada ya mda flan kuna uwezekano mashine nyingi zikashindwa kufanya kazi..inabidi uandaliwe utaratibu mwingine utakaokuwa mbadala wa hizo mashine zilizopo hivi sasa...
 
Mtu katoa somo zuri watu mnamponda . Duh we have a long journey to go .
 
Huu uzamani ndiyo mzuri kwa watu kama wewe, vinginevyo mkipewa nafasi kwa usasa unaotaka mtapola sana na kupunguza mapato!!
Hizi huduma bado Ni Za kizamani sana, labda uwajulishe hao wa mkoa, habari Za tiket kukaguliwa Na kuchanwa inapoteza muda wa abiria. Hapa walitakiwa waweke scan mashine ndani ya mabasi iwe unaweza kuilipia kwa ukubwa wa safari. Ukiingia Na kutoka iwe unascan.
 
Back
Top Bottom