Sikubaliani asilani na maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji wake akizindua kituo cha mabasi huko nyumbani, Mbezi Louis lililopewa jina lake.
Kwanza Magufuli amesema Stendi hiyo ni ya Kimataifa (International Bus Stop) ambapo mabasi yatafika hapo na abiria kutoka mataifa mbalimbali.
Magufuli amedai (na mimi nakubaliana naye) kwamba ni Stendi nzuri na ya kisasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa imegharimu zaidi ya Sh 50 bilioni licha kwamba zabuni yake ilijaa utata mtupu. Potelea mbali sasa kimekamilika.
Rais amesema atasikitika sana akijakuona Stendi hiyo imeandikwa na kuchorwa uchafu wao wakiita "kupiga chata" tena wengine wakitumia kinyesi chao. Itakuwa ni aibu.
Rais wa wanyonge akasema Machinga nao waingie humo, mamalishe wapike uji humo, boda-boda wapaki pikipiki humo, mshindi ya kuchoma na mitumba iuzwe madirishani kwa abiria nk. Ukweli ni kwamba kama haya yataachwa yafanyike tusahau hadhi ya Stendi hiyo kuwa ya Kimataifa. Haitokuwa tofauti na Manzese.
Kwanini Julius Nyerere International Airport (JNIA) hawaruhusiwi wamachinga kufanya biashara au tunaogopa wazungu? Kwa nini Magufuli Bus Terminal na si viwanja vya ndege kama kweli tuna mahaba na wanyonge?
Hatuwezi kuruhusu hali hiyo then tukose chata za vinyesi maukutani na kila aina ya uchafu. Otherwise niamini yalikuwa ni porojo za siasa kumfurahisha hadhira na kushangiliwa. Kuna namna ya kusaidia wafanyabiashara ndogo ndogo kote duniani hata huku tuliko.
Si nasema ukweli ndugu zangu!