Maelekezo aliyotoa Rais Magufuli Mbezi Louis ni porojo za siasa, nashusha hoja

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,528
2,000
Akili za ubongo kipimo Cha uzito wa gram 3.01 hizi. unafananisha airport na stendi !!!???.
 

NORTHERNIST

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
236
250
Lengo ni kuwa stand isiwe inabagua watu inapaswa iwe ni matumaini kwa wote bila kujali classes za watu
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,680
2,000
Hao machinga, bodaboda, mama lishe na wachoma mishikaki ndio wanaotoa huduma kwa mtanzania wa kawaida atakayetumia stendi hiyo.

Huko JNIA unakotolea mfano hakuwahudumii watanzania wa kawaida. Acha wanyonge wafanye kazi.
USIJITIE HAMNAZO.

Keshoo utakuja na kero/malalamiko oooh, majinga, wapiga debe kero stand ya mbezi.

Yote kwa yote stendi ya dodoma ni mfano, hao wapiga bebe wapo ila wanakuwa trick sana na machinga wana vizimba vyao ndani, pembeni ya stendi.

NOTE: Vaa barakoa na unawe mikono kwa sabuni na maji tiririka pia ukae mbali na mikusanyiko.
 

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,201
2,000
Inawezekana bro,kwani wamachinga na mama ntilie watawekwa kwenye zone yao na watakatazwa uchafu,uchafu ni tabia inayoweza kudhibitiwa
 

mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,561
2,000
USIJITIE HAMNAZO.

Keshoo utakuja na kero/malalamiko oooh, majinga, wapiga debe kero stand ya mbezi.

Yote kwa yote stendi ya dodoma ni mfano, hao wapiga bebe wapo ila wanakuwa trick sana na machinga wana vizimba vyao ndani, pembeni ya stendi.

NOTE: Vaa barakoa na unawe mikono kwa sabuni na maji tiririka pia ukae mbali na mikusanyiko.
Ni kweli wapiga debe na wamachinga wanakera, lakini siku zote hua najizuia kuwalaumu. Hawa watu ni watanzania wenzangu, tena wenye vipato duni, na wameamua kujitafutia mkate wao kwa njia halali.
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,899
2,000
Rais wa wanyonge akasema Machinga nao waingie humo, mamalishe wapike uji humo, boda-boda wapaki pikipiki humo, mshindi ya kuchoma na mitumba iuzwe madirishani kwa abiria nk. Ukweli ni kwamba kama haya yataachwa yafanyike tusahau hadhi ya Stendi hiyo kuwa ya Kimataifa. Haitokuwa tofauti na Manzese.
Lugha hii imenishangaza sana, hasa ukizingatia amesema ni stand ya kimataifa!
Tuna safari ndefu mnomno nchi hii naapa!
Pia data za kuwa ndio stand kubwa E&C Africa napata kigugumizi.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,753
2,000
Mchezo unaochezwa hapa ni kuwa na wanaoitwa WANYONGE,
Sinema kamili kwenye kuongezewa muhula mwingine,2025-2030,
Hiyo wanyonge haitumiki Bahati mbaya,ndio FIMBO Yenyewe hiyo,tulieni mtaniambia
Exactly!
Siyo mi5 tena ni mi50 tena!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,590
2,000
Serikali inakwepa lawama ya kwanini jobless wameongezeka kiwango cha juu sana.
Haijatafuta mu arobaini wa kumaliza tatizo la ajira.
Ila wanafanya maigizo.
Kuna haja gani ya kuwa na wizara ya kazi isiojua hata namna ya kuajiri wafanyakazi?
Kuna haja gani ya kuwa na Tanzania Investment Center isiotilia maslahi ya kuajiri wafanyakazi wazalendo.
Kuna haja gani ya kuwa na vyama vya wafanyakazi visivyotambua maslahi ya mfanyakazi.
Mwisho ni kutumia mabavu kwa kukosa busara na hekima.
 

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,195
2,000
Hivi hakuna uwezekano huko mbeleni kubadilisha hayo majina?

Siyo siri mimi huwa naona hayapendezi hata labda baadhi ya yale ya zamani mfano

1.Daraja la Mkapa imekaa poa naona

2.Uwanja wa Mkapa Stadium haijakaa poa bora ingebaki tu uwanja wa taifa

3.Daraja la Nyerere wala haileti tija bora ingekaa vilevile daraja la kigamboni Nyerere amekumbukwa/anakumbukwa kwa mengi wala hakukuwa na haja ya kumwingiza kila kakitu

4.Soko lile la Morogoro kuitwa Kingalu ndo kabisaa baadae italeta impact ya ukabila... muda!

5.airport ya JKNIA ingeitwa tu DIA kama ilivyo KIA

6.stendi hiyo ndo kabisaa hata haileti mtiririko kwenye kutamka badala yake MBEZI BUS TERMINAL ingetosha na kufaa zaidi

7.ndoo ndogo kule ukanda wa nyumbani zinaitwa Mkapa mpaka leo imezoeleka na naona imekaa fresh pia (ndoo za ujazo wa wa lita 10)

8.mwaka wa uongozi wa kikwete wakatoa vindoo vidogo kama mkapa ila vyenyewe vyembamba zaidi wakaviita Kikwete wala haikukaa poa na wala havikudumu vikapotea

9.M4C ile ya Magufuli For Change tu ndo niliona inafit na jina hilo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom