Maelekezo aliyotoa Rais Magufuli Mbezi Louis ni porojo za siasa, nashusha hoja

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
373
1,000
Sikubaliani asilani na maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji wake akizindua kituo cha mabasi huko nyumbani, Mbezi Louis lililopewa jina lake.

Kwanza Magufuli amesema Stendi hiyo ni ya Kimataifa (International Bus Stop) ambapo mabasi yatafika hapo na abiria kutoka mataifa mbalimbali.

Magufuli amedai (na mimi nakubaliana naye) kwamba ni Stendi nzuri na ya kisasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa imegharimu zaidi ya Sh 50 bilioni licha kwamba zabuni yake ilijaa utata mtupu. Potelea mbali sasa kimekamilika.

Rais amesema atasikitika sana akijakuona Stendi hiyo imeandikwa na kuchorwa uchafu wao wakiita "kupiga chata" tena wengine wakitumia kinyesi chao. Itakuwa ni aibu.

Rais wa wanyonge akasema Machinga nao waingie humo, mamalishe wapike uji humo, boda-boda wapaki pikipiki humo, mshindi ya kuchoma na mitumba iuzwe madirishani kwa abiria nk. Ukweli ni kwamba kama haya yataachwa yafanyike tusahau hadhi ya Stendi hiyo kuwa ya Kimataifa. Haitokuwa tofauti na Manzese.

Kwanini Julius Nyerere International Airport (JNIA) hawaruhusiwi wamachinga kufanya biashara au tunaogopa wazungu? Kwa nini Magufuli Bus Terminal na si viwanja vya ndege kama kweli tuna mahaba na wanyonge?

Hatuwezi kuruhusu hali hiyo then tukose chata za vinyesi maukutani na kila aina ya uchafu. Otherwise niamini yalikuwa ni porojo za siasa kumfurahisha hadhira na kushangiliwa. Kuna namna ya kusaidia wafanyabiashara ndogo ndogo kote duniani hata huku tuliko.

Si nasema ukweli ndugu zangu!
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,207
2,000
Watendaji wanapata wakati mgumu sana kusimamia mpangilio wa mambo, leo majiji makubwa mitaa imejaa wamachinga ni kero na hasara kubwa.

Angesema waweke setup ya vizimba groups vyao planned sambamba sio free range hata kuku hufungwa kwa mpangilio.
 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,523
2,000
Ile stendi nafananisha na hazina iliyopatikana kwa ajili ya familia,Sasa huwezi ukawa selective nani ashiriki kwenye hazina hiyo ,na Nani asishiriki.

Kama hazina niya familia yote basi,rais yuko correct ,machinga,bodaboda,mama ntilie n.k wote ni watanzania ,ile stendi ni kitega uchumi, hivyo kila mmoja anahaki ya kuitumia kiuchumi kupata riziki.

Haikujengwa kwa ajili ya wanaochomekea,au wavaa suti,au wenye mitaji mikubwa n.k ,ni ya watanzania wote.kuhusu usafi ametoa hiyo mifano kusisitiza wahusika watakao kabidhiwa jukumu la kuhakikisha stendi haipotezi muonekano wake,Basi wawe wawajibikaji vilivyo.
 

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
373
1,000
ile stendi nafananisha na hazina iliyopatikana kwa ajili ya familia,Sasa huwezi ukawa selective nani ashiriki kwenye hazina hiyo ,na Nani asishiriki.kama hazina niya familia yote basi,rais yuko correct ,machinga,bodaboda,mama ntilie n.k wote ni watanzania ,ile stendi ni kitega uchumi ,hivyo kila mmoja anahaki ya kuitumia kiuchumi kupata riziki.haikujengwa kwa ajili ya wanaochomekea,au wavaa suti,au wenye mitaji mikubwa n.k ,ni ya watanzania wote.kuhusu usafi ametoa hiyo mifano kusisitiza wahusika watakao kabidhiwa jukumu la kuhakikisha stendi haipotezi muonekano wake,Basi wawe wawajibikaji vilivyo.
JNIA si kitega uchumi? Au unakariri
 

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
472
1,000
Ukweli ni kwamba serikali inawajibu wa kuwatafutia wafanyabiashara wadogo maeneo na mazingira mazuri ya wao kufanya shuguli zao bila kubuguziwa na mtu.

Kitendo cha serikali kuruhusu wafanybiashara wadogo kufanya biashara sehemu yoyote ile Kama vile kando ya barabara inaweza kuleta hatari kwa wafanyabiara au watumiaji wa barabara kama itatokea Ajai.

Jambo jingine ni ukweli usiofichika vibanda vya wamachinga kando ya barabara na maeneo yote ambayo sio maalumu kwa biashara yanachafua mandhari ya miji yetu.

Binafsi sipingi hoja ya watu hususani wamachiga kufanya biashara zao, ila ninachokiona hapa ni kua serikali inajaribu kukimbia wajibu wake wa kuwaandalia mazingira na maeneo maalumu ambayo hawa wafanyabiashara watafanya shuguli zao bila buguza, matokeo yake serilikali inawapa uhuru wa kufanya biashara sehemu yoyote ile kwa mgongo wa wananchi wanyonge na raia wenyewe pasipo kujua kitu wanafurai na kuona serikali inawapenda
 

Mwanga Mkali

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
545
1,000
Ukweli ni kwamba serikali inawajibu wa kuwatafutia wafanyabiashara wadogo maeneo na mazingira mazuri ya wao kufanya shuguli zao bila kubuguziwa na mtu.
Kitendo cha serikali kuruhusu wafanybiashara wadogo kufanya biashara sehemu yoyote ile Kama vile kando ya barabara inaweza kuleta hatari kwa wafanyabiara au watumiaji wa barabara kama itatokea Ajai.
Jambo jingine ni ukweli usiofichika vibanda vya wamachinga kando ya barabara na maeneo yote ambayo sio maalumu kwa biashara yanachafua mandhari ya miji yetu.

Binafsi sipingi hoja ya watu hususani wamachiga kufanya biashara zao, ila ninachokiona hapa ni kua serikali inajaribu kukimbia wajibu wake wa kuwaandalia mazingira na maeneo maalumu ambayo hawa wafanyabiashara watafanya shuguli zao bila buguza, matokeo yake serilikali inawapa uhuru wa kufanya biashara sehemu yoyote ile kwa mgongo wa wananchi wanyonge na raia wenyewe pasipo kujua kitu wanafurai na kuona serikali inawapenda
Maeneo hutengwa ila wanunuzi sir ndio hatutoi ushirikiano...fikiria ukiwa kwenye ka vitz kako kushuka dukani kwa mangi hushuki unapiga horn kuagizia unachotaka...sembuse stand
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,000
Mkubwa kuna kitu kizuri sana hapa umekiongoea. Zabuni ilikuwa na mauzauza, lakini sasa tuna stendi imesimama. Cha muhimu hapa ni kuwa tulitaka stendi ya kisasa, and that is what we got. It is there, it is tangible and we can see it. And we probably got more than what we expected, given the history ya stendi ya ubungo na usanii uliofanyika kwenye UDA. Ukilinganisha na hili ya Mbezi unaona kabisa hapa kuna mabadiliko ya nyuzi 360.

Haya maswala ya majina, masuala ya usafi, na maswala ya wamachinga...all these can be contested. Kulinganisha JKNA na Stendi ya JPM si haki ni vitu viwili tofauti. Hata London kwa mfano angalia biashara zinazofanyika Victoria station na zile zinazofanyika Heathrow na Gatwick, unaweza kuona ni tofauti kabisa. Na hii sio kwa sababu watu weusi wanainga kwenye viwanja hivyo, au kwa sababu wazuungu wenyeji ndio watumiaji zaidi wa Victoria station. Ukiangalia kwa undani utajua kuwa ni zaidi ya hapo.
 

mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,560
2,000
Hao machinga, bodaboda, mama lishe na wachoma mishikaki ndio wanaotoa huduma kwa mtanzania wa kawaida atakayetumia stendi hiyo.

Huko JNIA unakotolea mfano hakuwahudumii watanzania wa kawaida. Acha wanyonge wafanye kazi.
 

jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
430
1,000
Aaaahhh...koo lako ni zito ndio maana unatema makohozii tuu..huna hoja mzee..twwnde stand mpya ya magu..
 

jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
430
1,000
JNIA si kitega uchumi? Au unakariri
Mkuu ni hivi..jaribu kutofautisha level za watu wanaotumia JNIA na stand za mabasi.

Moja..uwanja wa ndege ni sehem ya watu wenye uchumi mkubwa (namanisha wasafir) ..ukisema umuweke cjui mama ntilie hakuna biashara pale..lakin huku kwenye mabasi wapo watu wa kila aina..uchumi mdogo..mkubwaa..na wakati..uchumi mdogo watu watahitaji huduma za bei chee..wa kati vile vile na wa juu watapata huduma za juu mana kuna hotel pia..nazani koo lako sasa litakuwa chepesi na umeelewaa mjuu wa tindulasu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom