Maegesho ya magari katikati ya jiji la Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maegesho ya magari katikati ya jiji la Dar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mutensa, May 5, 2009.

 1. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wana-JF
  heshima mbele,
  mimi nitatatizwa na kitu kimoja ambacho nimeona ni vema tukijadili. Kila siku ukienda mitaa ya kati (City centre) utaona kuwa si rahisi kupata maegesho ya gari. Sasa mimi nilikuwa najiuliza tatizo hili litakwisha lini. Upande mwingine wa shilingi nikaona kuwa inaelekea wale wanawekeza katikati ya mji labda kuna mawazo hawajayapata ambayo yanalipa na yanaweza kuwasaidia watanzania. Kila mtu anafikiria kuinua jengo kwa ajili ya biashara (ofisi, hotels, etc). sasa mimi nauliza ... je mtu akiinua jengo la ghorofa kadhaa kwa ajili ya parking peke yake, si atakusanya hela kama mchanga jamani? Uwezekano wa kuwekeza katika miundo mbinu hiyo haupo?
  Secondly,
  je serikali haiwezi kuweka sheria/utaratibu ya kuwabana wanaojenga majengo marefu waoneshe namna gani wateja wao watakavyopaki magari? Ninachokiona haswa posta na kariakoo ni majengo marefu sana yakiibuka lakini nje ya majengo hayo, ukibahatika kupata parking itakuwa ya magari si zaidi ya 5 au hamna kabisa kwa majengo yaliyo mengi.
  Hili mnalionaje wadau.
  Tujenge taifa kwa pamoja, mawazo ya kila mtanzania yatasaidia...
   
 2. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani Mabasi ya abiria hasa makubwa yangeboreshwa na yawe mengi ili watu wengi watumie badala ya kila mtu kuwa na gari yake kwenda mjini, na Vipanya viishie nje ya mji tu. Pia magari madogo ushuru wa kupaki uwe mkubwa say, 5,000 kwa saa ukipaki maeneo ya city centre! Hii nadhani itasaidia kidogo kwa kuanzia nadhani hatutaweza kujenga majengo ya kutosha kuegeshe utitiri wa magari yaliyopo mjini.

  Haya ni mawazo yangu tu Mkuu Mutensa
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mawazo mazuri, lakini tutayapeleka wapi for implementations? Wakuu wa nchi sasa hivi wanawaza uchaguzi 2010 na si kitu kingine kwa sasa. Ukitaka kuamini hilo.. last week kamati kuu ya CCM imekutana pale patakatifu (Ikulu) na moja kati ya maazimio ama kilichojadiliwa ni "kikwete kuwa mgombea pekee 2010". Swali kamati kuu haina vitu vya msingi vya kujadili na kumsaidia rais na serikali yake (hata chama chao pia) hadi wakapata muda wa kujadili kitu ambacho hakina TIJA kwa sasa. Taifa linapita katika wakati mgumu, ningetegemea kikao kingekuja walau na madhimio ya maana kama vile;

  1. Vita dhidi ya ufisadi (je hatua zinazochukuliwa zinatosha?)
  2. Janga la njaa ambalo taifa linaelekea kukumbwa
  3.GFC
  4. Kuporomoka kwa ubora wa elimu (nini kifanyike)
  5.Uwajibikaji kwa watumishi wa umma (angalia kilichotokea mbagala)
  6. na mengi mengineyo

  Ndugu zangu tuko tayari nchi iendeshwe kama DECI??
   
 4. f

  fkabete Member

  #4
  May 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo Mpango uko siku nyuma ulikuwepo, lakini nasikia wakubwa/mafisadi wengi ndio wenye vipanya hapa mjini, inakuwa ngumu kuzuia vipanya vyao visifanye kazi.
   
 5. P

  Preacher JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imagine unaondoka nyumbani kwako saa 11.00 asubuhi - kutembea hadi kufika main road ili kupanda bus - usafiri kuja mjini sio kwa wafanya kazi tu - ila kuna all sort of groups of people - wafanyakazi, wagonjwa, walemavu, wafanyabiashara - etc. USAFIRI ukiwa wa BIG BUSES TU inakuwa ngumu. Issue ingine ni kuwa BIG BUSES have very low speed - ukilinganisha na barabara zetu finyu - que itakuwa pale pale njiani - na kwa vile TIME FACTOR kwa sisi watanzania ni 0 - usumbufu utajitokeza - unless ROADMAP ifanyike kwa undani jinisi zoezi zima litakavyokuwa - Parking mjini - ni kweli ni shida sana - hasa kwa mwananchi wa kawaida - na inasikitisha kuwa Manispaa inafanya biashara ila haina JIPYA inachofanya kuacha kukusanya fee za parking - HIYO NI IDEA ULIYOKUJA NAYO YA BIASHARA - TAKE A STEP - TAFUTA OPEN SPACE - RENT IT - HALAFU WATU WATAPARK NA KUKULIPA WEWE - HII INAFANYIKA KWENYE OPEN SPACE YA POST OFFICE (NEW) NA JAMAA WENGINE WENYE NAFASI KWENYE NYUMBA ZAO HAPA TOWN - ILA PARKING SYSTEM ILIYOKO INAPIGA SANA KELELE KWANI WANATAKA HELA ZOTE WACHUKUE WAO - just remember that viongozi wa nchi yetu wao hawana shida na kamwe hawatakaa wafikirie kufanya kitu cha kumsaidia mnyonge -
   
Loading...