Maduka ya watu wa Bara yachomwa Zanzibar; yadaiwa ni kampeni dhidi ya Muungano!

source. radio tbc at 4PM Kwa kile kinachoonekana kama chuki dhidi ya watanganyika vijana wa kizanzibari wamechoa maduka huko unguja ya wafanyabiashara wenye asili ya bara na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni 400. hawa wameuchoka muungano. hivi nasisi tukiamua kwenda hapo kariakoo itakuwaje?
"Haya ni mazao ya chama Tawala CCM kufanyia utani mambo yanayohitaji umakini, tunaelekea pabaya"
 
Hawa ni wahalifu tu na wala si wana harakati wa siasa. Hili ni kosa la jinai na wakikamatwa wafikishwe mahakamani. Kama ni kuuchoka muungano wajikusanye wapeleke malalamishi yao kwa viongozi wao kwanza, pili wampelekee risala rais wa jamhuri ya muungano. Hakuna cha muungano wa kulazimishwa hapa.

Jasusi, usishangae kuona kimya. kuna mambo lukuki yanawapata watu wa bara Zanzibar lakini hakuna chochote kimefanyika. Mwaka huu tu peke yake zimechomwa bar zaidi ya tatu. Kisingizio ni kwamba hawataki watu wauze pombe lakini cha ajabu ziko bar nyingi zinamilikiwa na wanzazibari na hazijachomwa!

Nadhani muda umefika sasa kwa Rais wa Zanzibar na makamu wake wawili (maana ni serikali ya umoja wa kitaifa) kuwaambia watanzania toka bara kama wanaruhusiwa kuishi na kufanya biashara Zanzibar na pia awahakikishie usalama wao. Ninaposema kuhakikisha usalama naamania kama matatizo yanatokea kama yaliyotekea sasa basi serikali ionekane kukereka na kuwashughulikia wahusika. Haiwezekani haya mambo yakaendelea hivi hivi maana nionavyo mimi hatua inayofuata ni mtu wa bara kuuliwa. Tusifike huko.
 
Mh! Wanatupeleka kubaya hawa. hakuna haja ya kulipa kisasi, utoto unawasumbua, wakikua wataacha. Hata kama hawautaki Muungano sidhani kama hii ndio njiia muafaka yab kueleza hisia zao

wewe una uzembe wa kufikiri, kama viongozi wanaziba masikio hawataki muungano ujadiliwe wanauona Muungano ni Mtakatifu kuliko Mungu.

Kila Jambo lililoko chini ya Jua lazima kulijadili hasa pale jamii inaona kuna matatizo. Panua mawazo usiwe mwepesi wa kulaumu Muungano una kasoro kubwa.
 
Leo katika Taarifa ya habari ITV kumeonyeshwa habari ya kusikitisha ambapo Wazanzibar wamechoma maduka ya Wabara wanaofanya biashara visiwani humo. Cha kusikitisha zaidi imeelezwa kuwa wachomaji hao waliwatisha hao wabara kwa siku kadhaa kabla ya kutimiza azma yao bila polisi kuchukua hatua yeyote!!

Je, serikali ya akina Seif and Shein iliridhia kadhia hiyo maana hakuna cha zima moto wala polisi haikujishughulisha kuzuia tukio hilo!!!!
 
Hafanywi mtu kitu Zanzibar, hivi kumbe hamuijui kweli, akamatwe mzanzibari kwa sababu kafanya chochote kwa mtu wa bara? hata siku moja msijidanganye, tena huyo wa bara akienda ripoti atachekwa na Polisi hao hao wa Muungano.
 
Bara tunapewa umeme kwa mgao, wao wanapewa full, halafu faida ni hii?
 
Nadhani umekusudia kusema ya akina Shein na Seif Mkuu.

Kwanini usiseme ya SMZ tu?
 
ishu siyo muungano wala watanganyika. Ishu ni kwamba kila binadamu anapo kuwa na matatizo lazima watafute scape goat. Zanzibar umasikini mwingini na wananchi hawajui nani wa kumlaumu. Sasa frustrations zao wana zitoa kwa watanganyika. Ni kama wasouth afrika wanao ua wageni kisa hawana kazi wakati wanajua fika chanzo cha umasikini wao sio hao wageni. Zanzibaris are frustrated people.

i concur!!
 
Nafikiri watanganyika hawautaki muungano kabisa, viongozi ndo wanang'ang'ania kwa maslahi yao binafsi

Mfano ni RAISI;hatakuwa raisi wa nchi yoyopte hapa duniani.Ndiyo maana viongozi wanaung'ang'ania,eti kwa sababu za kiusalama
 
Bara tunapewa umeme kwa mgao, wao wanapewa full, halafu faida ni hii?

Hata Zanzibar mgao upo Mkuu ingawa silo nnalotaka kusema hili.

Hio ni isolated case kama ya kuchoma baa na kwa kweli wala kama mimi sifurahii vitendo kama hivi/

Naomba msi jump into conclusions kwani Mkuu nakujua wewe huko Polisi.
 
Hafanywi mtu kitu Zanzibar, hivi kumbe hamuijui kweli, akamatwe mzanzibari kwa sababu kafanya chochote kwa mtu wa bara? hata siku moja msijidanganye, tena huyo wa bara akienda ripoti atachekwa na Polisi hao hao wa Muungano.

Uchunguzi kwani umekwisha wazee wangu?
 
Kwanini tusiuvunje tu huu mnaouita muungano, honestly sioni haja ya kuendelea kukaa na hawa mamwinyi!
 
Kuna mwanafunzi toka bara aliwahi kubakwa na kuchanwa pande zote na wazanzibari wawili kisha wakamtupa, hata hospitali hajapelekwa ilibidi atoke bara baba yake na kuja kumchukua, wote walimcheka tu, huu wa maduka ni moja ya mifano ya unyanyasaji wa wabara wachache Zanzibar, huku wao wakiwa na kila uhuru, sasa dawa ya moto?

Nipo gym, ngoja waguse anga zangu hao wala ukwaju; vita ni vita muraa! Kama serikali haipo ama ipo likizo,basi wananchi tutakuwepo kwa niaba yao!

Hawa ni wauza mbao na maduka huku bara,waanze kufunga virago tartibu.

Hali sasa sio salama kwa mbara kuwa znz kwa sasa, take care wabara!
 
Mbona Wazanzibari kila mara wanauwawa huko bara, mbona haijawa issue Mkuu?
 
Hao si waharifu, waharifu gani wa namna hiyo. Tatizo wa afrika sijui tuko je mpaka mambo yawe kama ya Gbagbo ndo mijitu inasituka. Muungano si lazima kulazimisha watu ambao hawautaki wanataka mpaka rebels watokee ndo waelewe hawa jamaa?

Hawa waliochoma wakitokea wahuni wa ulaya wakawapa silahaa wanakuwa rebel hawa na watapigana.
 
Inasikitisha sana kuona watu wazima wanazama kwenye ubaguzi namna hiyo, hakuna haja ya kufikiri kufanya kama wao K'koo umefika wakati tuuangalie muungano wetu kama hatuutaki basi tuachane nao, siyo kama Kombani na Werema wanavyotaka usijadiliwe haiwezekani tuujadili na tuamue utaratibu wetu wasitulazimishe na muungano ambao mwisho wa siku utaleta maafa.
 
Back
Top Bottom