Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,851
- 15,265
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Rais Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za Serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali.
Wengi tulishuhudia huduma nzuri pamoja na upatikanaji wa dawa ndani ya hospitali lakini leo mambo yamejirudia pale pale.
Leo hii Mwananchi wa kawaida anaona ni bora akapate huduma katika Hospitali binafsi kuliko ya Serikali kutokana na huduma mbovu zitolewazo katika Hospitali za umma.
Ndani ya hospitali za Serikali mara nyingi utapimwa vipimo lakini baada ya majibu kuja utaandikiwa paracetamol na dawa nyingine utaambiwa kanunue duka lililopo nje ya geti.
Kwa upande wa kina mama wanaojifungua tunaambiwa ni bure lakini Hospital nyingi za umma huwa wanalipishwa, huku wajawazito wakiamriwa waje na vifaa vya kujifungulia kama vile pamba. Gloves nk.
Wizara ya afya wafuatilie na pia wawe wakali maana Hospitali za umma zimekuwa changamoto sana kwa wananchi wa kawaida.
Kwenye nchi yoyote ile huduma bora za afya ndio kipaumbele cha kwanza kwani afya ndo kila kitu kwenye maisha ya binadamu,
Hizi hizi huduma mbovu pamoja na Ukosefu wa madawa hospitalini ndio chanzo cha vifo vingi ambavyo vingeweza kuepukika, serikali iweke sera nzuri kupitia wizara ya afya ili kuondoa hili tatizo.
Mbona suala la tozo limewezekana nchi nzima