Maduka ya Dawa yaliyo nje ya mageti ya Hospitali za Serikali huwa na dawa muda wote lakini ndani ya Hospitali husika hamna dawa

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,219
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Rais Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za Serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali.

Wengi tulishuhudia huduma nzuri pamoja na upatikanaji wa dawa ndani ya hospitali lakini leo mambo yamejirudia pale pale.

Leo hii Mwananchi wa kawaida anaona ni bora akapate huduma katika Hospitali binafsi kuliko ya Serikali kutokana na huduma mbovu zitolewazo katika Hospitali za umma.

Ndani ya hospitali za Serikali mara nyingi utapimwa vipimo lakini baada ya majibu kuja utaandikiwa paracetamol na dawa nyingine utaambiwa kanunue duka lililopo nje ya geti.

Kwa upande wa kina mama wanaojifungua tunaambiwa ni bure lakini Hospital nyingi za umma huwa wanalipishwa, huku wajawazito wakiamriwa waje na vifaa vya kujifungulia kama vile pamba. Gloves nk.

Wizara ya afya wafuatilie na pia wawe wakali maana Hospitali za umma zimekuwa changamoto sana kwa wananchi wa kawaida.

Kwenye nchi yoyote ile huduma bora za afya ndio kipaumbele cha kwanza kwani afya ndo kila kitu kwenye maisha ya binadamu,
Hizi hizi huduma mbovu pamoja na Ukosefu wa madawa hospitalini ndio chanzo cha vifo vingi ambavyo vingeweza kuepukika, serikali iweke sera nzuri kupitia wizara ya afya ili kuondoa hili tatizo.

Mbona suala la tozo limewezekana nchi nzima
 
Umedanganya , Sheria ilimzuia Magufuli kufunga maduka ya dawa karibu na Hospitali , akaamua kuanzisha maduka ya MSD ili kuyashinda maduka binafsi , huku akisahau kwamba kila wodi ya Wagonjwa kule ndani , sewahaji , Mwaisela nk zinayo maduka humo humo vyumbani , kifupi alichemsha vibaya .

Maduka ya dawa hukaguliwa na Mamlaka ya chakula na dawa , hakuna dawa ya serikali inaweza kuuzwa mle , maana dawa zao zina nembo
 
Nje ya hospital lazima kuwe na duka la dawa kihosptal kidogo chenye vipimo vikubwa os imetawala pharmacy msaada unaupata maduka ya nje ya kutumia bima
 
Umedanganya , Sheria ilimzuia Magufuli kufunga maduka ya dawa karibu na Hospitali , akaamua kuanzisha maduka ya MSD ili kuyashinda maduka binafsi , huku akisahau kwba kila wodi ya Wagonjwa kule ndani , sewahaji , Mwaisela nk zinayo maduka humo humo vyumbani , kifupi alichemsha vibaya .

Maduka ya dawa hukaguliwa na Mamlaka ya chakula na dawa , hakuna dawabya serikali inaweza kuuzwa mle .
Wewe ndio mwongo, unazifahamu taratibu za baraza la famasia? Pia maduka ya MSD yapo na dawa zina bei nafuu sana.
 
Umedanganya , Sheria ilimzuia Magufuli kufunga maduka ya dawa karibu na Hospitali , akaamua kuanzisha maduka ya MSD ili kuyashinda maduka binafsi , huku akisahau kwba kila wodi ya Wagonjwa kule ndani , sewahaji , Mwaisela nk zinayo maduka humo humo vyumbani , kifupi alichemsha vibaya .

Maduka ya dawa hukaguliwa na Mamlaka ya chakula na dawa , hakuna dawabya serikali inaweza kuuzwa mle .
Mada ni kuwa inakuweje maduka nje ya hospitali yawe na dawa lakini ndani ya hospitali hakuna dawa wala gloves?

We umeangalia hospitali moja mi nimefanya mzunguko wa hospitali nyingi za serikali.
Isitoshe pia kusema sisi ambao tunakaa na manesi jirani wanavyowauzia dawa majirani wanawazunguka, kila aina ya dawa wanazo na nyingi za watoto,.
 
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Raisi Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali...
Hebu ileza maduka ya nje yanakuwaje chanzo cha ukozefu wa dawa hospitali. Serikalo inasema mama ni bure Lakini hivyo vitu vya bure huwa serikali yenyewe haivileti sasa kosa la nani kwa mfano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani dawa zinatolewa bure! ndugu yangu kata bima ya afya ndipo kwenye unafuu
Kulipia kwa cash ni gharama haswa kama unamagonjwa endelevu

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Sio wote wenye bima, na hata itoshe kusema kuwa uwe na bima au usiwe na bima changamoto ni nyingi sana ndani ya hospitali za serikali kubwa ikiwa ni ukosefu wa Dawa ndani ya hospitali.
 
Kilimani Pharmacy pale Mawenzi Hospital Moshi. Nilizungushwa sana wakati nauguza. Kila kitu kuanzia mionzi hadi dawa nililazimika kwenda pale sababu hapo hospital wameshatengeneza network ya kupiga pesa.

Utasubirishwa pasipo sababu ya msingi huku ukiambiwa kama unaweza nenda kapige hapo kilimani uje doctor akupe huduma. Dawa zote unazoandikiwa hazipo, ila utaambiwa nenda hapo kilimani wanazo
 
Magufuli aliharibu akili za vijana wengi.

Hata mwenyewe alimind then akajiona lofa tu.

Unamzuia mtu kuweka duka la dawa karibu na hospital kwa sheria ipi?

Yeye akiishiwa dawa anapanda daladala anafuata Kariakoo faster ila serikali mpaka ipeleke dawa kwenye zahanati au hospital lazima mchakato uchukue zaidi ya mwezi mmoja.
 
Hii nchi ina Wapumbavu wengi mtoa mada akiwa mmojawapo

Upatikanaji wa dawa ndani ya Hospitali hauna uhusiano na uwepo wa dawa katika maduka yaliyoko nje ya Hospitali. Dhana hiyo ni moya ya akili fupi alizopata kuwa nazo yeyote aliyefikiria.

Serikali iboreshe mifumo yake ya upatikanaji wa dawa kupitia MSD, Wazabuni binafsi na taratibu zingine ili Vituo vyake viwe na dawa.

Unapoanza kushangaa kwa nini Maduka ya nje ya Hospitali yana dawa na na Zahanati au Hospitali hakuna kwani chanzo chao ni kimoja? Taratibu za manunuzi kwa Hospitali zinafanana na taratibu za manunuzi za mtu binafsi?

Famasi Binafsi wanaweza at any time t wakaenda Kariakoo au kwenye Duka lolote la Jumla wakanunua mzigo aidha kwa Cash au Mali kauli wakaweka dukani, je taratibu za manunuzi ya Umma yanaruhusu hilo?

Hii nchi Wapumbavu ni wengi sana kuliko tunavyodhania.
 
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Raisi Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali...
Watu wanakula kwa urefu wa kamba,ni kama uhamiaji,Kuna viofisi vingi vya stationary,kila copy unaelekezwa katolee pale.
 
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Raisi Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali...
Acha kupotosha wewe, lini maduka binafsi yaliyoko nje ya hospital yalifungwa?

Yaani alikuja na mbwembwe nyingi eti maduka yote yaliyopo nje ya hospital yafungwe, wakamtazama tu, hakuna aliyefunga , na hakuna kilichofuata!

Suluhisho ni kuweka dawa hospitalini tu, sasa ukiyafunga halafu bado dawa kwenye hizo hospital hakuna, kuna nini?ule ulikuwa ni UKURUPUKAJI TU, na jiwe na diblo waliangukia pua.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom