Maduka na Siasa: Zamani tuliita Kwa Mpemba, Kwa Mchaga, Kwa Muha, Kwa Msambaa hao siku hizi ndio vinara wa siasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,430
Hii ya " kwa mangi" ilikuja baadae zamani tuliita " pale kwa mchagga".
Maduka mengine masrufu ukiondoa yale ya Ushirika ilikuwa " Kwa mpemba" au " kwa msambaa" na " kwa Muha"

Hawa hawa siku hizi ndio maarufu kwenye vyama vya siasa, angalia Chadema, Cuf, ACT wazalendo, Nccr mageuzi, TLP, Sau, Chaumma na kadhalika na kadhalika.

Wale wa maduka ya Ushirika ndio sawa na hawa CCM.

Sijaelewa sawasawa hii connection ya maduka na vyama vya siasa, ngoja nichimbue historia zaidi.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Hahahaaaa........ "...kanunue mkate wa siha pale kwa mchagga"

Unakimbie kwenye kiduka cha Ndesamburo......utoto raha sana bwashee!
Pamoja na kulitambulisha duka au muuza duka kwa njia ya kabila lake lkn ukabila haukuwa na nguvu. Wengi tuliishi kama ndugu tunaotoka mkoa mmoja.

Siasa zilivyo ingia ndo zikaanza kutugawa kwa makabila, dini, ukanda na wengine mpaka rangi. Utasikia "mi siwezi kwenda kununua chumvi kwa mpemba maake jamaa ni mfadhili mkubwa wa chama cha cuf nk"
 
Pamoja na kulitambulisha duka au muuza duka kwa njia ya kabila lake lkn ukabila haukuwa na nguvu. Wengi tuliishi kama ndugu tunaotoka mkoa mmoja. Siasa zilivyo ingia ndo zikaanza kutugawa kwa makabila, dini, ukanda na wengine mpaka rangi. Utasikia "mi siwezi kwenda kununua chumvi kwa mpemba maake jamaa ni mfadhili mkubwa wa chama cha cuf nk"
Kweli kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom