Maduka kubadilisha fedha kufutiwa leseni Sept. 2

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa waraka kwa wafanyabiashara wa maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni kuomba upya leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Leseni zote za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni zitafutwa ifikapo Septemba 2, mwaka huu ili wamiliki waombe upya.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Msimamizi Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za Kigeni wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanuti Mosha kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mosha alisema kwa sheria ya sasa, mfanyabiashara atatakiwa kumiliki duka moja tu tofauti na ilivyokuwa awali mtu mmoja anaweza kumiliki maduka hata matano. Alisema sambamba na kutoa leseni upya, BoT imeweka viwango vipya vya mtaji ambavyo vinaanzia Sh milioni 100 hadi 300 kwa daraja A, na kuanzia Sh milioni 250 hadi Sh bilioni moja kwa daraja B na Amana ya Thamani kuanzia Dola za Marekani milioni 50 hadi milioni 100.

Aidha, alisema wafanyabiashara wa Daraja B watafanya miamala ya papo kwa hapo pamoja na miamala ya nje ya nchi. Hata hivyo, Mosha alisema mbali na masharti ya mtaji, watahitajika pia kufunga kamera tatu ‘CCTV‘ kwa ajili ya usalama.

Alieleza kuwa lengo ni kudhibiti ubadilishaji wa fedha na utoaji wa stakabadhi, kamera zinatakiwa kufungwa kaunta, kwenye kabati la kuhifadhia fedha na eneo la kuhudumia wateja.

Alisema watakaokamilisha masharti hayo ndio watakuwa wanaendesha biashara hiyo kuanzia Septemba mwaka huu Wafanyabiashara hao wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wamepewa miezi mitatu kuanzia Juni 2, 2017 hadi Septemba mosi, mwaka huu wakamilishe usajili na kumiliki duka moja tu. Mosha alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma maombi BoT.

Chanzo: HabariLeo
 
Huruhusiwi kuwa na katawi? Hata kama usajili uliofanya ni wa duka moja? Au kisichoruhusiwa kufungua maduka ya kubadirishia fedha kwa majina tofauti na yote yakawa ni ya mmiliki mmoja? Ufafanuzi please wadau
 
Number bado zinasomeka

2020 toa ccm nje

Swissme
Sawa, lakini itakuwa 2020 ingiza CCM ndani. Huoni hili la maduka ya kubadilisha fedha kuzagaa kiholela ilikuwa ni chaka fulani la kutakatisha fedha? Serikali ilikosa mapato? Udhibiti ulikuwa mdogo kuendana na sera ya kifedha inayoambatana na mambo ya uchumi? Je,uholela huu ilikuwa sio sababu ya fedha yetu kushuka thamani? Faida iliyokuwa inapatikana haikuwa inapelekwa nje kama fedha za kigeni sio kwa tshs? Je, huoni hii biashara ilishikiliwa na wajanja fulani wakiwa na mikakati mahususi na iliyojificha? Kwanini kama ni biashara rahisi hukuti mmatumbi, mkurya, mgogo, mnyambwa, mmatengo, msonjo wa kule vijijini wakiifanya bali ni tabaka fulani?Tufikiri nje ya box, nadhani na ni mtizamo wangu hii yote inafanyika ili kuleta udhibiti wa biashara hii na wala si NUMBER BADO ZINASOMEKA.
 
Huruhusiwi kuwa na katawi? Hata kama usajili uliofanya ni wa duka moja? Au kisichoruhusiwa kufungua maduka ya kubadirishia fedha kwa majina tofauti na yote yakawa ni ya mmiliki mmoja? Ufafanuzi please wadau

Mosha alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma maombi BoT.
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa waraka kwa wafanyabiashara wa maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni kuomba upya leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Leseni zote za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni zitafutwa ifikapo Septemba 2, mwaka huu ili wamiliki waombe upya.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Msimamizi Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za Kigeni wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanuti Mosha kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mosha alisema kwa sheria ya sasa, mfanyabiashara atatakiwa kumiliki duka moja tu tofauti na ilivyokuwa awali mtu mmoja anaweza kumiliki maduka hata matano. Alisema sambamba na kutoa leseni upya, BoT imeweka viwango vipya vya mtaji ambavyo vinaanzia Sh milioni 100 hadi 300 kwa daraja A, na kuanzia Sh milioni 250 hadi Sh bilioni moja kwa daraja B na Amana ya Thamani kuanzia Dola za Marekani milioni 50 hadi milioni 100.

Aidha, alisema wafanyabiashara wa Daraja B watafanya miamala ya papo kwa hapo pamoja na miamala ya nje ya nchi. Hata hivyo, Mosha alisema mbali na masharti ya mtaji, watahitajika pia kufunga kamera tatu ‘CCTV‘ kwa ajili ya usalama.

Alieleza kuwa lengo ni kudhibiti ubadilishaji wa fedha na utoaji wa stakabadhi, kamera zinatakiwa kufungwa kaunta, kwenye kabati la kuhifadhia fedha na eneo la kuhudumia wateja.

Alisema watakaokamilisha masharti hayo ndio watakuwa wanaendesha biashara hiyo kuanzia Septemba mwaka huu Wafanyabiashara hao wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wamepewa miezi mitatu kuanzia Juni 2, 2017 hadi Septemba mosi, mwaka huu wakamilishe usajili na kumiliki duka moja tu. Mosha alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma maombi BoT.

Chanzo: HabariLeo
Hizo CCTV Camera zingesaidia sana kama nchi ingekuwa na Bank Surveillance System

BOT na Financial Intelligent Unit wangekuwa na uwezo wakuziona mubashara benki na bureau de change zote kila wanapotaka

Cc: Minister of finance & Central bank governor
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa waraka kwa wafanyabiashara wa maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni kuomba upya leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Leseni zote za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni zitafutwa ifikapo Septemba 2, mwaka huu ili wamiliki waombe upya.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Msimamizi Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za Kigeni wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanuti Mosha kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mosha alisema kwa sheria ya sasa, mfanyabiashara atatakiwa kumiliki duka moja tu tofauti na ilivyokuwa awali mtu mmoja anaweza kumiliki maduka hata matano. Alisema sambamba na kutoa leseni upya, BoT imeweka viwango vipya vya mtaji ambavyo vinaanzia Sh milioni 100 hadi 300 kwa daraja A, na kuanzia Sh milioni 250 hadi Sh bilioni moja kwa daraja B na Amana ya Thamani kuanzia Dola za Marekani milioni 50 hadi milioni 100.

Aidha, alisema wafanyabiashara wa Daraja B watafanya miamala ya papo kwa hapo pamoja na miamala ya nje ya nchi. Hata hivyo, Mosha alisema mbali na masharti ya mtaji, watahitajika pia kufunga kamera tatu ‘CCTV‘ kwa ajili ya usalama.

Alieleza kuwa lengo ni kudhibiti ubadilishaji wa fedha na utoaji wa stakabadhi, kamera zinatakiwa kufungwa kaunta, kwenye kabati la kuhifadhia fedha na eneo la kuhudumia wateja.

Alisema watakaokamilisha masharti hayo ndio watakuwa wanaendesha biashara hiyo kuanzia Septemba mwaka huu Wafanyabiashara hao wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wamepewa miezi mitatu kuanzia Juni 2, 2017 hadi Septemba mosi, mwaka huu wakamilishe usajili na kumiliki duka moja tu. Mosha alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma maombi BoT.

Chanzo: HabariLeo
Hii ni sawa,lakini kigezo cha ziada ni muhimu.Ihakikishwe pasi shaka yeyote kwamba fedha anazotumia mfanyibiashara hazikupatikana kwa njia haramu.Kigezo hiki kitumike pia kwenye uanzishwaji wa Bank za kawaida.Kumekuwa na utitiri mkubwa mno wa Bank nchini ambao sidhani kama una tija yeyote kwenye uchumi wa nchi yetu.

Kiukweli utitiri wa Bureau de Change na Banks inaonekana kama ni njia ya kutakatisha fedha haramu, kwa hiyo tight control ni muhimu.
 
Back
Top Bottom