Maduka gani wanauza Nigerian foods Dar

Jan 12, 2015
67
59
Habari wanajamii forum, naomba msaada wa kujua ni wapi naweza kununua vyakula vya kinigeria. Nina rafiki yangu nilisoma nae huko nchi za watu,amekuja kikazi TZ sasa angependa kujua kwa Dar hivyo vyakula vinauzwa wapi ili awe anajipikia mwenyewe. Ninaomba msaada kama kuna watu wanajua vinapouzwa.
 
Mpaka nimeandika hii thread I know that kuna utofauti kwasababu niliishi nao huko ulaya na vyakula vyao vilikuwa vinauzwa kwenye hiyo nchi, wali wanakula lakini mchele wao nitofauti na wakwetu, ugali hawali kwasababu sisi tunatumia unga wa mahindi na vyakula vingine vya kikwao vinavyoandikwa kikwao wenyewe wakiviona wanajua.
 
Ni bora umtembeze sokoni , ataona mwenyewe vyakula gani ghafi vipo ambavyo anavijua na anaweza kupika mwenyewe - nadhani atakidhi mahitaji yake
 
kwa kweli mimi pia nilizsoma habar za mgahawa mmoja nigeria kupika nyama za watu. ilinishangaza sana
 
Tofauti kubwa sana. Wa Nigeria wanakula nyama za watu. Huku bongo sidhani kama binadamu wanaliwa
mzee, nyama za watu zinaliwa sana hata hapa tz na watu hawajui kama ni nyama za watu. only those wenye macho ya kiroho ndio wanaweza wasile nyama. kuna nyama zingine zinauzwa wewe unafikiri ni za ng'ombe lakini wengine wanajua za watu. wakati mwingine wachawi wanaingia buchani wanaweka tako la mtu ninyi mnaopita mnaona ni mguu wa ng'ombe ila kuna watu wanauona kabisa sio wa ng'ombe. hiyo mishikaki inayouzwa kwenye machips zinachanganywa sana huko. izo nyama zisizo na mifupa hizo wanaweka walau kipande kimoja ndani ya vipande vingine vya ng'ombe, na ni makafara wanaambiwa wafanye hivyo kwaajili ya biashara zao. wengine mnalishwa nyama za watu usiku na wachawi bila ninyi kujua. in short kama hauko ndani ya Yesu, wewe ni boga ambalo shetani na wachawi wanaweza kukufanya chochote.

kuna wadada wengi sana wanafanywa ngono usiku wakiamka wanaona wamechafuliwa na wachawi bila wao kujua. wachawi wengi tu wanatembelea watu usiku na kuwafanya vibaya.

kuna mbibi mmoja alishawahi kukamatwa, yeye kazi yake ilikuwa kuwalambisha uchii wake watu usiku. mnalishwa sana nyama kichawi, mnauziwa sana nyama kichawi bila kujua. tafuteni Mungu mpate macho ya kiroho.
 
TChai!! Chinekeee na God forbid ooo, they eat nyama za watu?! Basi itabidi nimpeleke kwenye mgahawa wao akifika huko atawauliza wanzake ghafi huwa zinauzwa wapi ili awe ananunua mwenyewe na kujipikilisha
 
Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.na usituletee!!

Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!

Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.

Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.

Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.

Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .

Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.

Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.

Chanzo: BBC Swahili
 
TChai!! Chinekeee na God forbid ooo, they eat nyama za watu?! Basi itabidi nimpeleke kwenye mgahawa wao akifika huko atawauliza wanzake ghafi huwa zinauzwa wapi ili awe ananunua mwenyewe na kujipikilisha

Anataka hii?
 

Attachments

  • 1431749769466.jpg
    1431749769466.jpg
    18.6 KB · Views: 211
Mpaka nimeandika hii thread I know that kuna utofauti kwasababu niliishi nao huko ulaya na vyakula vyao vilikuwa vinauzwa kwenye hiyo nchi, wali wanakula lakini mchele wao nitofauti na wakwetu, ugali hawali kwasababu sisi tunatumia unga wa mahindi na vyakula vingine vya kikwao vinavyoandikwa kikwao wenyewe wakiviona wanajua.

Ambavyo havijapikwa sijui, vilivyopikwa mlete kkoo likoma street kuna restaurant inaitwa WAZOBIA atakula kila chakula cha kinigeria na wanapika wanigeria wenzake
 
Back
Top Bottom