Maduka 70 ya wafanyabiashara waliokwepa kodi jijini Mwanza yafungwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Halmashauri ya jiji la Mwanza imeyafunga maduka 70 ya wafanyabiashara yaliyopo kandokando ya shule ya sekondari Pamba, ambayo yanadaiwa kukwepa kulipa kodi ya pango na kuisababishia halmashauri ya jiji hilo kupoteza mapato ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa mwaka.

Hatua ya mkurugenzi wa jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba, kuamua kuyafunga maduka hayo inalenga kukusanya shilingi bilioni 2 kwa mwaka katika vyumba vya biashara vinavyomilikiwa na halmashauri ya jiji hili, zoezi hilo linafanyika sambamba na kuivunja mikataba inayohujumu mapato ya halmashauri ya jiji la Mwanza.

Hata hivyo zoezi hilo limebaini kuwepo kwa mikataba ya makampuni hewa yanayokusanya kodi kutoka kwa wafanyabishara hao.

Kibamba ameapa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waliohusika kuhujumu mapato ya serikali.

Halmashauri ya jiji la Mwanza ina miliki jumla ya vyumba vya maduka 1024 ambapo kwa hii leo imefungia vyumba 70 vya wakwepa kodi na oparesheni hiyo inatarajiwa kufanyika ndani ya siku tatu ili kuyafikia maduka yote.

Chanzo: ITV
 
1476862772612.jpg
Hawana direct debit na kulipa moja kwa moja Bank?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom