Madudu ya vigogo hadharani, VIONGOZI WA WIZARA WADAIWA KUPORA MRADI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madudu ya vigogo hadharani, VIONGOZI WA WIZARA WADAIWA KUPORA MRADI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VIKWAZO, Jun 17, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  • VIONGOZI WA WIZARA WADAIWA KUPORA MRADI

  SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeingizwa katika mvutano wa kibiashara ambao unahusisha taasisi ya nchini Ubelgiji inayoidhinisha kutumia mifumo ya biashara ya utambuzi wa bidhaa za kimataifa GSI, kwa kutumia nembo za mistari inayojulikana kama ‘bar codes'.

  Habari zilizolifikia gazeti hili kwa siku kadhaa sasa zimebaini kuwa mzozo huo unatokana na kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za
  viongozi wa ngazi za juu wa wizara hiyo kudaiwa kutumia jina la serikali ya Rais Kikwete kutimiza haja binafsi za kibiashara.
  Tukio hili ambalo linaweza kuchafua taswira ya Serikali ya Tanzania, limeibuliwa na Mtanzania mjasiriamali Ole Koimere, anayeinyooshea kidole serikali ya Rais Kikwete hususan Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo, kwa kile alichodai njama za kumpora mradi wake wa kutaka kuanzisha huduma ya kutoa ‘bar codes' hapa nchini, ambayo kwa sasa haipatikani hadi nchi jirani.
  Mjasiriamali huyo, Ole Koimere anasisitiza kuwa mradi huo aliporwa, kwa madai kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo la kuuanzisha hapa nchini akiwa amefuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kupata hati ya usajili kutoka Brela.
  Akizungumza na Tanzania Daima juu ya kisa hicho, mjasiriamali huyo, alidai kuwa mwaka 2010 akiwa katika semina moja iliyohusisha wajasiriamali pamoja na maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara, aliibua wazo hilo la Tanzania kushindwa kutoa huduma ya ‘bar codes'.
  Alisema kuwa baada ya kuibua wazo hilo ndani ya chumba cha mkutano, wakati wa mapumziko, aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, D. Massawe, alimfuata na kumweleza kuwa ni wazo zuri na kumwambia aandike maombi wizarani kuomba kuwa wakala wa kazi hiyo hapa nchini. Kila nchi haitakiwi kuwa na wakala zaidi ya mmoja.
  Ole Koimere alisema kuwa, aliandika barua hiyo Februari 10, mwaka jana (tunayo) akiomba kuwa wakala kwa hapa nchini.
  Alisema katika hali ya kushangaza baada ya siku mbili tu, wizara iliijibu barua yake (nakala tunayo) ikiwa imesainiwa na Massawe ikimjulisha kuwa kuna jitihada zilizoanzishwa hapa nchini kwa lengo la kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma hiyo, akieleza kuwa kwa wakati huo TPSF na TIRDO walikuwa wakikusanya maoni ya wadau kabla ya kuitisha kikao cha pamoja kupanga mkakati wa kufanikisha azima hiyo.
  Alisema kuwa wakati huo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajili Kampuni ya GS1 Tanzania, ambapo waliandika barua Brela Februari 26,2010 kuomba usajili na Machi 18, mwaka huo huo walipata hati ya usajili nambari 75537.
  "Kwa kuwa maombi ya leseni hutumwa Ubelgiji yalipo makao makuu ya GS1 na mwisho wa kupeleka nyaraka za maombi kila mwaka ni Machi 31, tuliona tumechelewa hivyo tukaamua tujiandae kwa mwaka huu wa 2011…lakini maombi yetu tulikuwa tumeishatuma Ubelgiji Desemba 18, 2010 wakati tukisubiri barua za kuungwa mkono na kampuni 250 kama tulivyoagizwa na Brela."
  "Tuliandika barua SIDO, Desemba 2010 tukiomba kupitia kwao watuunge mkono katika kuzipata hizo kampuni lakini tulikwama kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi," alisema.
  Alisema Januari 19 mwaka huu walipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo (nakala ya barua tunayo), akitaka kuonana na wakurugenzi wa kampuni hiyo ya GS1 Tanzania Ltd.
  Kwa mujibu wa Ole Koimere, waliitikia wito huo lakini cha ajabu,
  katibu mkuu huyo aliwajulisha kuwa alikuwa amewaita kuwaomba wamuachie jina la kampuni yao hiyo lakini hata hivyo walimkatalia.
  Alisema baada ya siku kadhaa ilisajiliwa kampuni nyingine Brela,
  inayotambulika kwa jina la GS1 (TZ) National Ltd ambayo ilipata hati ya usajili Januari 28, mwaka huu na siku hiyo hiyo walipokea barua pepe kutoka Ubelgiji kwa Meneja Mkuu wa huduma, Monica Walsh, akimtaarifu kuwa tayari wamepokea maombi kutoka kwa kampuni ya hiyo ambayo alidai kwamba inaungwa mkono na Serikali ya Tanzania na kwamba mchana wa siku hiyo hiyo alikuwa akienda kukutana na mwakilishi wa kampuni hiyo kutoka Tanzania.
  Kwa kuwa utoaji wa ‘bar codes' hufanywa na kampuni moja tu kwa kila nchi, lakini Brela inashutumiwa kwa kuzisajili kampuni mbili kwa shughuli moja.
  Habari zaidi zinaeleza kuwa Kampuni ya GS1 (TZ) Ltd inadaiwa kuundwa na watu walio karibu na wizara hiyo, kadhalika ikidaiwa kutumia rasilimali za serikali ikiwamo Brela (
  ushahidi wa hilo upo katika barua iliyoandikwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami, nakala tunayo).
  Kadhalika zipo nyaraka za vikao vya maandalizi ya uanzishwaji wa kampuni hiyo, zikionyesha gharama kubwa zilizotumika ambazo inasemekana zimekuwa zikitolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.
  Moja ya vikao kilichofanyika Ubungo Plaza, kati ya Januari 24 au Machi 5, mwaka huu nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kiasi cha zaidi ya sh milioni 46 zilitumika.
  Mbali na mjasiriamali huyo kuzungumza na gazeti hili, pia amepata kukutana na Waziri Chami na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumueleza juu ya hujuma hiyo inayodaiwa kufanywa na viongozi wa wizara dhidi yake.
  Alisema mara ya kwanza mbali na kukutana na Katibu Mkuu huyo, Mapunjo pia aliwahi kukutana na baadhi ya viongozi walioko Ikulu lakini hadi sasa hakuna alichojibiwa, hatua ambayo ilimfanya atafute nafasi ya kukutana na Rais Kikwete lakini bila mafanikio, ambapo sasa ameamua kumwandikia barua.
  Wakati Ole Koimere akilalamikia kupokwa mradi huo, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mapunjo, ambaye sasa anahudhuria mkutano wa Agoa nchini Zambia, hivi karibuni alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu madai hayo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa watu hao.
  Katikati ya wiki hii Mapunjo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuutaarifu umma kuwa Tanzania imefanikiwa kuidhinishwa kutumia ‘bar code'.
  Katika mkutano huo ambao pia aliongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Esterian Mahingila, naye alipoulizwa kama
  kuna kampuni nyingine ilisajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo alikana madai hayo na kusema kuwa kampuni iliyosajiliwa ni moja tu.

  tANZANIA DAIMA   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  It happens in every industry in the country and outside Tanzania, kabla ya ku-trumpet ni muhimu kumaliza homework yako

  to do business, you have to be greed hata kama ni ya makaburi
   
 3. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tanzania nchi inayowafaa wazi tu! Hakuna kitu cha halali nchi hii. Nchi hii asilimia kubwa ya successful business man ni either ni jambazi au ofisa wa serikali.
  Kufanyabiashara kubwa katika hii nchi ni heri ukalimee!
  Huyu jamaa alikuwa amepata deal zuri na pengine angeifanya kazi hii kwa ufanisi maana alikuwa na malengo.

  Sasa hawa walionynaga'anya hawajui hata kinachotakiwa kifanyike. Wanachokiona mbele yao ni mkataba mnono na serikali ya kifisadi.

  Kampuni hii haitafanya vizuri hat siku moja maana wenyewe hawajui wamedandia behewa wasilojua linaenda wapi!

  Hili ni sakata zuri naona hapa jamaa akiendelea kuwavua nguo hii wizara tutaona mengi.

  Kkwani sheria zinasemaje juu ya hili!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  yale yale kama walivyopora mradi wa kusafirisha mafuta kwa bomba kwenda mwanza!matokeo yake mpaka leo hakuna kilicho fanyika.nchi hii ubunifu ni kazi bure!bongo ni ufisadi tuu uta win life
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii nchi inakwenda wapi?
   
Loading...