Luushu
JF-Expert Member
- Apr 8, 2012
- 816
- 477
Shule ya msingi diamond kuna madudu yanafanyika pale walimu wamefanya ile shule kama yao na sii ya serikali.
Kuna vijimiradi vinaendelea pale vya kujipatia kipato kwa kila mwalimu mmoja mmoja kuingia vimikataba na wazazi eti kuwafundisha watoto nje ya masomo ya kawaida na kuna mkakati wa kishule unaitwa remedio ambao wanafunzi wanalipa pesa kwa ajili ya masomo ya ziada.
Muda wa masomo huanza saa moja na nusu asubuhi mpaka saa saba na dakika arobaini na tano kisha watoto huingia tena darasani mpaka saa kumi eti remedio, walimu wamekuwa wakijitetea kwamba kuna idadi kubwa ya wanafunzi hivyo sio rahisi kuwafikia kila mmoja katika vipindi vya kawaida hivyo muda wa ziada unatakiwa.
Swali langu kwa Ndalichako waziri wa elimu inawezekanaje huyu mwalimu ambaye hawezi kufundisha katika muda wa kawaida kwa kisingizio cha wanafunzi wengi atawezaje darasa hilo hilo katika muda wa ziada akalifundisha bila malalamiko.
Je huu sio wizi wa kiana, shule ina walimu zaidi ya 40 wa kiume wawili hili sio tatizo, shule hii ya serikali inayofundisha mchepuo wa kingereza watoto wanafika darasa la saba kingereza hawajui kwa mitihani hii ya kuchagua hata mimi naweza kubahatisha ila na uhakika multiple choice ikifutwa hakuna atae faulu.
Wazazi tumeimba watoto watoke saa saba na dakika arobaini na tano ili na sisi wazazi tuweze kukaa nao na kusaidia nyumbani uongozi wa shule umekataa ili waendelee kula hela ya remedio
Mwisho nakuomba waziri wa elimu fika Diamond primary school kajionee kushuka kwa elimu na nakushauri sambaza walimu wote leta wapya na vunja kamati ya shule tuunde upya kwa maendeleo ya shule.