Madudu ya TFF kuishusha madaraja Kimondo FC

Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,584
6,694
Tarehe 21 Jan, Kimondo iliiandikia TFF barua kuomba pesa zao za FA ili zitumike kusafirisha timu kwenda Ruvuma kucheza na JKT Mlale.

Kimondo.jpg

Feb 4, Kamati ya TPLB ikakaa na kuishusha Kimondo FC madaraja mawili na kuipiga faini ya Tsh 2M kwa kutoonekana uwanjani. Timu hiyo pia ikafutiwa matokeo ya mechi zake zote ilizocheza katika kundi B ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yamefutwa kwa kushindwa kufika uwanjani kucheza mechi dhidi ya JKT Mlale bila sababu za msingi.

TFF wanasema mechi hiyo namba 47 ilitakiwa kuchezwa Januari 28 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea lakini Kimondo haikutokea uwanjani wala kutoa taarifa yoyote hadi Februari 1 ilipotuma taarifa Bodi ya Ligi (TPLB) na kutoa sababu ambazo hazikukubaliwa na Kamati. (Barua inaonesha kuandika tarehe 24.01.2017 kwenda TFF na Bodi ya Ligi.

TFF.jpg

Kwa madudu haya, tukisema Jamal Malinzi ameshindwa kuiendesha TFF tutakuwa tunakosea?
 
Hii Kimondo bora ishushwe tu ili ikajipange kwanza, hebu angali hawawezi kuandika hata barua vizuri!
 
Kwa TFF ya Malinzi haya yanayotokea ni ya kawaida,tumeshayazoea
 
Tarehe 21 Jan, Kimondo iliiandikia TFF barua kuomba pesa zao za FA ili zitumike kusafirisha timu kwenda Ruvuma kucheza na JKT Mlale.

View attachment 469441

Feb 4, Kamati ya TPLB ikakaa na kuishusha Kimondo FC madaraja mawili na kuipiga faini ya Tsh 2M kwa kutoonekana uwanjani. Timu hiyo pia ikafutiwa matokeo ya mechi zake zote ilizocheza katika kundi B ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yamefutwa kwa kushindwa kufika uwanjani kucheza mechi dhidi ya JKT Mlale bila sababu za msingi.

TFF wanasema mechi hiyo namba 47 ilitakiwa kuchezwa Januari 28 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea lakini Kimondo haikutokea uwanjani wala kutoa taarifa yoyote hadi Februari 1 ilipotuma taarifa Bodi ya Ligi (TPLB) na kutoa sababu ambazo hazikukubaliwa na Kamati. (Barua inaonesha kuandika tarehe 24.01.2017 kwenda TFF na Bodi ya Ligi.

View attachment 469442

Kwa madudu haya, tukisema Jamal Malinzi ameshindwa kuiendesha TFF tutakuwa tunakosea?
Huu upuuzi wa klabu kuvunja kanuni tunazicheke ni tz safi sana Malinzi kwa hili, yaani bajeti ambayo mmetumia kutoka Mbozi kwenda Mbeya mjini mnatuaminisha ndio hiyo ambayo mngetumia kutoka Mbozi mpaka Songea yaani hata umbali wa km hamuuoni ni uongo dhahiri??then kutolipwa fedha za FA sio sababu ya kuvunja kanuni, ligi daraja la kwanza inajulikana haina udhamini mmeshindwa ku organise fund ya kutosha, timu za tz kutafuta wadhamini zinataka mpaka TFF wawatafutie khaa, yaani imefika mahali mpaka jezi mnataka mpewe na TFF kila kitu tegemezi, mpira wa sasa ni uchumi fungueni macho wapeni timu wawekezaji wenye pesa timu ziwe na mipango sahihi ya pesa,mkacheze daraja la nne huko hakuna gharama
 
Kwahiyo TFF kuwacheleweshea malipo yao sio kosa mkuu?
 
kama Bunge la limeingilia kati katika ligi ya Epl kuhusu maendeleo ya soka la England. na kutowa maamuzi magumu ambayo Chama cha soka cha England FA wanatakiwa watekeleze.

Sasa ufike wakati Hapa napo Bongo BUNGE na Serikali ingilie kati juu ya uwendeshwaji wa soka la bongo.

Inavyo onekana sasa TFF imeachiwa majukumu yote ya mpira yani ni kama mtoto yatima. Na ndiyo mana sahizi TFF imekuwa sehemu ya kupiga dili na sio kuendeleza soka la Tanzania.
TFF kwa sasa haina msaada kwa soka la Tanzania na ndiyo maana hamna Timu Katika VPL inayo jiendesha kwa faidA

Kwa ukubwa wa VPL na timu tulizo nazo Tanzania na ukubwa wake eti leo timu zinagombea Ml 80 kweli ina maana TFF wanashidwa kutafuta njia za kupandisha dau kweli hata ikifika ml 200 itakuwa sio mbaya...

TFF ili ikopo kimondo fedha da kweli hii Tanzania hapa ni sawa tajiri aka ombe mkopo kwa maskini alafu unategemea huyu maskini aje kuwa mkubwa kama sio kumdidimiza kiuchumi.

SERIKALI iivunje TFF na kamati zake ili zisukwe tena upya. kwa TFF hii tusitegemee kama tuta kuja kupeleka timu kwenye mashindano ya Africa ..

dhamani ya kodi ya mtanzania iyendane na soka. sio thamani ya pesa haiyendani na soka huo unaitwa uhujumu

TANZANIA HATUNA CHAMA CHA MPIRA.
CHAMA CHA MPIRA HAKINA MAHUSIANO NA TIMU NDOGO BALI KINA MAHUSIANO NA YANGA NA SIMBA TU. NDIZO TIMU WANAZO ZIANGALIA NA WANAZO FANYA NAZO KAZI
 
Kwahiyo walitegemea hela za FA ndo wazitumie kwenye FDL, tusiwe tunawahukumu TFF kwenye mambo mengine ya kijinga.
Kwahiyo ulitaka wafanyeje kama timu haijafika uwanjani
 
Lakini kama mdhamini wa kombe la shirikisho (FA) ambaye ni Azam alishatoa hela kwa nin TFF wasizilipe timu shiriki fedha zao ontime??? Kimondo wana makosa na TFF wana makosa lkn makosa ya TFF ni makubwa zaidi ya Kimondo, TFF na Bodi ya ligi kwa ujumla they need to relook hili suala la kuishusha Kimondo, that is absolutely a capital punishment for Kimondo jamani.
 
Back
Top Bottom