Madudu serikalini:Spika Mstaafu,Mama Makinda na Bunge la 10 nao ni wa kulaumiwa pia

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Hivi sasa lawama nyingi zinaelekezwa kwa serikali iliyopita lakini tunasahau kuwa hata Bunge la 10 chini ya Mama Makinda lilishindwa kuisimamia vizuri serikali na lilifanya kazi kisiasa zaidi.

Inasikitisha kuona wabunge wa CCM waliona kazi ya kukosoa serikali ilikuwa ni kazi ya wapinzani na wao waliokuwa wengi kazi yao ilikuwa ni kutetea serikali tu.Hawa nao wametuponza sana kwani wamechangia hali hii kwa kiasi kikubwa tu.

Kwa mfano,katika Bunge la 10 kueleza tu mapungufu ya raisi/taasisi ya uraisi ilikuwa ni tatizo hata pale ilipostahili wapinzani kuhoji maana waliishia kukatishwa kwa maelezo huwezi kumsema mtu ambae hayuko Bungeni kwani hawezi kujitetea-kanuni za ajabu kabisa hizi!!

Wapinzani walikemea matumizi mabaya ya fedha kama vile ununuzi wa magari ya kifahari,safari za viongozi lakini walibezwa na wabunge wa CCM.

Spika Makinda na wabunge wako wote wakiwemo wapinzani mlishindwa kuonyesha mfano wa kupunguza matumizi ya serikali kwa kukataa kupokea sitting allowance.Makinda na wabunge wako mlishindwa kujiongeza katika hili na linawapunguzi uhalali wa kuhoji matumizi mabaya ya serikali.
 
Back
Top Bottom