The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 15,394
- 12,978
Itakufaje?
Duh.................!!! Kweli watu wameichoka CCM!!
Itakufaje?
kuan tatizo gani kuweka kituo cha kukagulia hapo nyumbani tanzania ya kwamba magari yote kabla hayjapewa plate numbers yakaguliwe hapo nyumbani kwa kulipia gharama ya USD 200 kwa gari. Hii itawezesha serikali kuingiza mapato mengi zaidi kuliko kungojea mawakala wa nchi za nje waliowaweka. Machine zenyewe zinagharimu Usd kama 50,000 hivi, ambazo zitaleta ajira nyumbani. Wataalam kila siku tunazalisha hasa vijana wa Technical colledges.Madudu ndani ya mashirika ya umma yamezidi kuibuka ambapo jana Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (POC), ilibaini kuwa Shirika la Viwango nchini (TBS), limedanganya taifa kwa kutumia makampuni hewa ya kukagua magari nje nchi. Utapeli huo ulibainika baada ya timu ya wabunge kufanya ziara katika nchi za Singapore, China na Japan kwa ajili ya kutembelea makampuni yanayoelezwa na TBS kwamba yanahusika na ukaguzi wa magari kabla ya hayajaingia hapa nchini.
Hata hivyo, wabunge hao walijionea vituko baada ya kufika huko nje ya nchi ambapo walibaini hapakuwa na kampuni wala ofisi yoyote inayofanya kazi hiyo ya ukaguzi wa magari. Mmoja wa wabunge hao, Deo Filikunjombe, alisema jana kuwa baada ya kufika walipata aibu mpaka wakafikia hatua ya kukimbilia ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo katika nchi hizo kwa ajili ya kujihifadhi. "Huko nje, hakuna ofisi, makampuni wala ofisi ambazo zimekuwa zikidaiwa na TBS zipo huko kwa ajili ya kukagua magari kabla hayajaingia nchini ili kujua ubora wake," alisema Filkunjombe.
Kutokana na utapeli huo kuwa mkubwa, Kamati imemuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutaka suala hilo litinge bungeni likajadiliwe na wabunge wote. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa POC, John Cheyo, alisema licha ya wabunge kukosa ofisi za makampuni hayo huko nje ya nchi, lakini pia hakuna mchanganuo wa fedha zilizopatikana kutokana na ukaguzi huo wa magari nje ya nchi.
Alisema TBS kwa miaka 10 mfululizo imekuwa ikifanya vibaya katika mahesabu yake na kueleza kuwa hakuna shirika bovu la serikali kama hilo hapa nchini. Imedaiwa kuwa baadhi ya wabunge waliokwenda nje ya nchi kuangalia makampuni hayo walitaka kumpiga ngumi, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, ambaye aliwaongoza baada ya kubaini kwamba walikuwa wanatapeliwa.
Kamati za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali (POC), jana zilisema ukaguzi wa magari unaingiza fedha nyingi lakini TBS imeshindwa kueleza mahali zilipo wala mchanganuo wake. "Huko nje ya nchi hatukukuta ofisi wala wakala wa ukaguzi wa magari baada ya kufanya ziara nje ya nchi, alisisitiza Makamu Mwenyekiti wa POAC, Filikunjombe.
Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati hizo, walisema kutokana na utendaji mbovu wa TBS, kwa sasa haijulikani magari mangapi yanayokaguliwa ubora wake kabla ya kuingia nchini na ukaguzi huo unaingiza kiasi gani cha fedha.
Kutokana na utata huo, kamati hizo zimeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na TBS wiki ijayo kufika mjini Dodoma ili kutoa maelezo ya kina.
SOURCE: NIPASHE
Kamati za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali (POC), jana zilisema ukaguzi wa magari unaingiza fedha nyingi lakini TBS imeshindwa kueleza mahali zilipo wala mchanganuo wake. "Huko nje ya nchi hatukukuta ofisi wala wakala wa ukaguzi wa magari baada ya kufanya ziara nje ya nchi, alisisitiza Makamu Mwenyekiti wa POAC, Filikunjombe.
SOURCE: NIPASHE
Kwani Nyerere alikuwa mwadilifu? Tuambie uadilifu wake ni upi.
Warioba namkumbuka alikuwa afisi ya mwanasharia mkuu. Sina kumukumbu nae.
Lakini nimefanya na watu zaidi ya 50 kutoka Mara akina Nyirabu na wengine wengi kutokea nikiwa wizara ya fedha muungano na mkoa wa Mwanza lakin sijapatapo kumuona mtu wa huko Mwadilifu. Labda nitajie wengine kama wapo waadilifu tuwaone.
Huu ndio upimbi yaani wewe kufanya kazi na watu 50 wa mkoa wa Mara umeshajiona ni mtaalamu wa tabia za zaidi ya watu milioni moja wa mkoa huo!
Sitarajii hata siku moja umkubali Nyerere kama kiongozi bora katika nchi hii. Kuanzia kwenye masimulizi ya historia ya wazee wenu wa gerezani, nilikuona rangi zako halisi tunapomzungumzia Nyerere.
Ukweli ni kwamba wenye akili zao timamu na wanaozitumia vizuri wanajua na kukubali kwamba Nyerere alikuwa ni kiongozi muadilifu. Hakuna mtu amewahi kulalamika kwamba Nyerere katumia madaraka yake kumpora shamba, nyumba ama kampuni. Sasa hivi tunashuhudia maraisi wenu bora wanavyokimbizana kufanya biashara wakiwa ikulu. Wanaanzisha makampuni ya kuwaibia watanzania, wanajaza watoto wao, wake zao, wajomba, mashangazi na mabinamu zao serikalini na kwenye mashirika ya umma.
Nyerere kwa uadilifu wake hata siku moja hakuwahi kumbeba mwanaye yeyote, kumuingiza katika serikali ama mashirika ya umma.
Kwa mfano tumeambiwa watumishi wa ofisi za makao makuu ya cuf upande wa bara imejaa wapemba watupu, wenzake na maalim seif lakini upande wa zanzibar watumishi wote ni wapemba. Huo ndio uhuni mnaofanya huko kwenu na ambao mwalimu hakuufanya na asingethubutu kumvumilia mtu aufanye. Je ni sawa kusema kwamba chama chote cha cuf si waadilifu ama huo ni mzigo wa maalim na washikaji zake wachache wanaoshiriki kuchakachua ajira ktk chama?