Madudu ndani ya Shirika la Viwango (TBS) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madudu ndani ya Shirika la Viwango (TBS)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jan 31, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Madudu ndani ya mashirika ya umma yamezidi kuibuka ambapo jana Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (POC), ilibaini kuwa Shirika la Viwango nchini (TBS), limedanganya taifa kwa kutumia makampuni hewa ya kukagua magari nje nchi. Utapeli huo ulibainika baada ya timu ya wabunge kufanya ziara katika nchi za Singapore, China na Japan kwa ajili ya kutembelea makampuni yanayoelezwa na TBS kwamba yanahusika na ukaguzi wa magari kabla ya hayajaingia hapa nchini.

  Hata hivyo, wabunge hao walijionea vituko baada ya kufika huko nje ya nchi ambapo walibaini hapakuwa na kampuni wala ofisi yoyote inayofanya kazi hiyo ya ukaguzi wa magari. Mmoja wa wabunge hao, Deo Filikunjombe, alisema jana kuwa baada ya kufika walipata aibu mpaka wakafikia hatua ya kukimbilia ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo katika nchi hizo kwa ajili ya kujihifadhi. "Huko nje, hakuna ofisi, makampuni wala ofisi ambazo zimekuwa zikidaiwa na TBS zipo huko kwa ajili ya kukagua magari kabla hayajaingia nchini ili kujua ubora wake," alisema Filkunjombe.

  Kutokana na utapeli huo kuwa mkubwa, Kamati imemuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutaka suala hilo litinge bungeni likajadiliwe na wabunge wote. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa POC, John Cheyo, alisema licha ya wabunge kukosa ofisi za makampuni hayo huko nje ya nchi, lakini pia hakuna mchanganuo wa fedha zilizopatikana kutokana na ukaguzi huo wa magari nje ya nchi.

  Alisema TBS kwa miaka 10 mfululizo imekuwa ikifanya vibaya katika mahesabu yake na kueleza kuwa hakuna shirika bovu la serikali kama hilo hapa nchini. Imedaiwa kuwa baadhi ya wabunge waliokwenda nje ya nchi kuangalia makampuni hayo walitaka kumpiga ngumi, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, ambaye aliwaongoza baada ya kubaini kwamba walikuwa wanatapeliwa.

  Kamati za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali (POC), jana zilisema ukaguzi wa magari unaingiza fedha nyingi lakini TBS imeshindwa kueleza mahali zilipo wala mchanganuo wake. "Huko nje ya nchi hatukukuta ofisi wala wakala wa ukaguzi wa magari baada ya kufanya ziara nje ya nchi," alisisitiza Makamu Mwenyekiti wa POAC, Filikunjombe.

  Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati hizo, walisema kutokana na utendaji mbovu wa TBS, kwa sasa haijulikani magari mangapi yanayokaguliwa ubora wake kabla ya kuingia nchini na ukaguzi huo unaingiza kiasi gani cha fedha.
  Kutokana na utata huo, kamati hizo zimeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na TBS wiki ijayo kufika mjini Dodoma ili kutoa maelezo ya kina.


  SOURCE: NIPASHE
   
 2. zululima

  zululima Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hasira yao hao wabunge ni kukosa takrima huko. wamezoea kuchukua allowance huku then wakifika huko wakirimiwe tena posho wanatia kibindoni. jiulizeni wana jf nini kilichowafanya kina filikunjombe kutaka kumchapa makonde ekerege? na nini kilichowafanya wakimbilie kujihifadhi ubalozini? wamezoea kulipwa mara mbili mbili. wao na ekerege wota mafisadi. inaudhi sana aggrhhh!!!!!
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hebu tuwekeeni list za hao wahusika tuwajadili.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika hapa ndipo ninaposema WaTz ni lini mtafikia kuamini vitu vyenu? Kwanini wasitumike mabalozi kulisimamia hili kwa niaba ya Serikali yenu. Kwanini aachiwe TBS pekee na balozi yupo.

  Kwa uzoefu wangu wa kufanyakazi Serikalini JMTz kwa miaka 12. Sijapata kuona kati ya niliofanya nao kazi Watu kutoka mkoa Mara kuwa muadilifu. Wengi wao niliwahi kufanya nao kazi walikuwa very corrupt. Na nimefanya na wengi.

  Mkurugenzi wa TBs ni wa huko pia.

   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Quality motors ya Hongkong ndo imeleta shida zote hizi,ni ya wakubwa wa Wizara
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wizara ipi?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Dah..."theory" zingine ni kabambe kweli!
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  wewe kwa akili zako finyu na zilizojaa udini ndiyo maana unatoa shutuma kama hii ukigeneralize mkoa mzima wenye makabila zaidi ya kumi. Unaweza ukatuthibitishia kauli zako hapa kwamba ni nani hao wa mkoa mara ambao si waadilifu kwa kauli zako za kibaguzi kama huko pemba kwenu. Ni mkoa upi uliotoa watendaji waaminifu serikalini kama siyo uelewa wako mdogo wa mambo. Ni watu wa mkoa mara ndiyo walikuwa bot, epa, richmond, ppf, wizara ya afya, bandarini, tra, n.k?


  Je waziri mkuu mstaafu jaji joseph waryoba anatoka pemba kwenu? Na rais aliyestaafu akiwa maskini japo alifanya kazi kipindi kirefu kuliko wengine nyerere naye anatoka kwenu pemba?

  Je yanayofanyika sasa hivi kwenye jeshi la wananchi napo ni watu wa mkoa mara ndiyo wako kwenye management? Jaribu kufikiri bila kuhusisha elimu yako ya madrasa kabla hujaleta hoja hapa. Wewe ni uaminifu unaouongelea kwa kuhusisha mkoa mzima badala ya kuulezea ukimlenga muhusika bila kujali sehemu anakotoka. Kwahiyo, kwa akili zako za madrasa unaamini kwamba huo ubabaishaji uliofanyika tbs ni kwasababu anatoka mkoa mara? Jaribu kutumia akili ktk kufikiri na si kuleta shutuma kwa watu wote wkt watu wa mkoa wapo wengi tu ambao wameendelea kuwa watumishi wema na waaminifu ktk nafasi mbalimbali.

  Nina wasiwasi na hata hapo unakofanyia kazi kama kuna mafanikio, kwani umetawaliwa na habari za kwenye vikao vya wanywa kahawa.
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Waende pia NSSF wakajionee sumu kali ya udini iliyopandwa hapo na R. Dau.
   
 10. T

  Tom JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuambie kama kweli kiongozi wa TBS si mla rushwa.
  Ukweli mwingine haujifichi: kwa mfano ni sahihi kugeneralise na kusema CCM (na mstaafu JOSEPH WARYOBA akiwemo) kuwa imeshindwa ama na inaendelea kushindwa kuongoza nchi na ni wala rushwa. Ushahidi wa kushindwa kuongoza nchi ni maisha ya dhiki ya kila MTANZANIA na pia rushwa imetapakaa sehemu zote hadi Mhimbili hospitaini. Kina Joseph Waryoba wa CCM wanaokaa kuliko bora na kupewa fursa ya matibabu kwenye hospitali yao India wakati ndugu zao wakiugua wanaishia MUHIMBILI wala si mali kitu.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwani Nyerere alikuwa mwadilifu? Tuambie uadilifu wake ni upi.

  Warioba namkumbuka alikuwa afisi ya mwanasharia mkuu. Sina kumukumbu nae.

  Lakin nimefanya na watu zaidi ya 50 kutoka Mara akina Nyirabu na wengine wengi kutokea nikiwa wizara ya fedha muungano na mkoa wa Mwanza lakin sijapatapo kumuona mtu wa huko Mwadilifu. Labda nitajie wengine kama wapo waadilifu tuwaone.

   
 12. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  nafikiri wewe hujaelewa hoja linaloongelewa hapa. Nimemfahamisha barubaru kwamba siyo jambo jema kuhusisha mkoa mzima kwa uwizi ambao umefanywa na mtu mmoja, kwani kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wale wanaofanya kazi zao za kwa uadilifu ktk taasisi mbalimbali hapa ndani na nje ya nchi. Suala la viongozi kwenda kutibiwa na nje ya nchi kwani iliasisiwa na watu wa mara au na serikali? Ni ktk mazingira gani unaweza ukahusisha tuhuma za mtu mmoja na mkoa mzima kama unafikiria sawasawa? Jaribu kusoma upya ili uweze kuona madhumuni hasa ya hiyo thread.
   
 13. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  WEWE UNA MATATIZO KTK KUWEKA HAYO MAMBO UNAYOYAONGELEA; UNATAKA KUNIFAHAMISHA KWAMBA KAMA NYIRABU HAKUWA MWAMINIFU NDIYO MKOA MZIMA UNA WATUMISHI WASIO WAAMINIFU? JE KATIKA WATU WALIOFANYA UWIZI WA MALI ZA UMMA HAPA TZ WOTE WANATOKA MKOA MARA? LEO HII WATU KAMA CHENGE, LOWASSA, ROSTAM, BALALI, LIYUMBA, N.K WOTE WANATOKA MARA? JE UWIZI/UFISADI/UDANGANYIFU UNAFANYIKA KWENYE TAASISI ZA SERIKALI UNAFANYWA NA WATU WA MARA? JE NI WATU WA MARA NDIYO WANAONGOZA HALMASHAURI ZINAZOONGOZA NCHINI KWA HATI CHAFU (UBADHIRIFU)? JE NI WATU WA MARA NDIYO WAKO KWENYE MANAGEMENT YA TAASISI KAMA PPF, NSSF, TANESCO, MIKATABA YA KWENYE MIGODI, NK.?

  UNAPOONGELEA NYERERE, HATA KAMA HAKUWA MWAMINIFU KWA JINSI UNAVYOJUA WEWE LKN NI RAIS GANI ALIYEFUATIA AMBAYE AMEISHI MAISHA YA KAWAIDA NA FAMILIA YAKE KULIKO NYERERE? NI NANI HUYO? NI MWINYI, MKAPA AU KIKWETE? JE MAISHA ALIYOISHI NYERERE NA WANAYOISHI FAMILIA YAKE UTAMLINGANISHA NA NANI SASA HIVI? KAMA UNATAKA KUJUA KTK HILI EBU ANGALIA HATA WALE AMBAO SI WATANZANIA WANAVYOUCHUKULIA UONGOZI WETU KWA SASA. KIPINDI CHA NYERER TZ ILIHESHIMIKA NDANI NA NJE YA NCHI LKN SIYO KTK HALI YA SASA. JARIBU KUZINDUKA NA UACHE CHUKI ZAKO ZENYE MSINGI WA KIDINI UNAPOONGELEA KUHUSU UAMINIFU WA VIONGOZI WETU. ANGALIA COMMENT HII HAPA;
  ona na hii comment nyingine ya mmarekani mmoja..

  Nepotism has risen; those in power ensures they slot in their children in sensitive positions before they retire. Currently, 15% of Tanzania government leadership is made of sons and daughters of those that once ruled or still in power.

  I see Tanzania in the line of Tunisia and Egypt very soon, and won't lose sleep if this man is ousted, we just don't want him in America. UK, you can have him.
  Our cabinet secretaries take subway, their ministers in expensive land cruisers. Not with our tax dollars. I learnt through secret channels that one of his associates transported a Range rover in a cargo plane to Tanzania


  Habari zaidi unaweza kuingia hapa chini;

  Davos 2012: Day two, as it happened | Business | guardian.co.uk

  KUMBUKA UNAPOONGELEA UAMINIFU NI DHANA PANA SANA; KWANI HATA KTK SUALA LA AJIRA LIKO HAPO NA HATA SUALA LA UTEUZI KWENYE VYEO MBALIMBALI NALO LIPO PIA; JE NI WATU WA MARA NDIYO WANAOTUMIA NAFASI ZAO KUPENDELEA WATU KWENYE AJIRA NA TEUZI MBALIMBALI KWA MISINGI YA DINI/KABILA N.K?

  HUWEZI KUSEMA NA KUTHIBITISHA KWAMBA UMEWAHI KUFANYA NAO KAZI ZAIDI YA 50 NA WOTE HAWAKUWA WAAMINIFU; JE WEWE ULIHUSIKA VIPI KTK KUSAIDIA KUONDOA HIYO HALI AU NA WEWE ULIKUWA SEHEMU YA HUO UKOSEFU WA UAMINIFU?

  KWA MTU AMBAYE ANGALAO ANA UELEWA MZURI NA EXPOSURE HUWEZI KUCHUKUA MAKOSA YA MTU MMOJA KAMA MKURUGENZI WA TBS NA KUHUKUMU MKOA MZIMA KWAMBA SIYO WAAMINIFU. HII SIYO SAHIHI HATA KIDOGO LABDA KAMA UNA CHUKI ZAKO BINAFSI NDIYO UAMUE KUSEMA HIVYO LKN HIYO SIYO SAHIHI. KWANI KUNA WATU WENGI SANA NA WANATOKA SEHEMU TOFAUTI NA MIKOA TOFAUTI KTK NCHI HII NA WAMEFANYA MAMBO TOFAUTI NA MAADILI YA KAZI LKN HATUWEZI KUHUKUMU MIKOA YOTE WANAYOTOKA NA WATU WA HUKO KWAMBA SIYO WAAMINFU. TUJARIBU KUTUMIA AKILI JAPO KIDOGO KUFIKIRI KAMA HATUJAWEKA COMMENTS ZETU HAPA. SUALA LA MTU MMOJA KUTOKUWA MWAMINIFU HAIMAANISHA TUWAHUKUMU WENGINE WOTE WANAOTOKA MKOA MOJA NAYE. MKURUGENZI WA TBS NA MWINGINE YEYOTE YULE ASIPOKUWA MWAMINIFU, BASI AWAJIBISHWE YEYE KWA MUJIBU WA TARATIBU NA SI KUJA NA MAWAZO KAMA YA KWAKO YA KUHUKUMU MKOA MZIMA KWA DHAMBI ZA MTU MMOJA. OTHERWISE, KAMA UNA MOTIVES ZAKO ZINGINE UNGEZISEMA NA SI KUTOA COMMENT KAMA HIZO ULIZOTOA.

  NAOMBA NIELEWEKE KWAMBA SITETEI HATA KIDOGO UFISADI AU UWIZI ULIOFANYWA NA MKURUGENZI WA TBS KAMA NI KWELI LKN SIKUBALIANI NA HOJA HAFIFU ZAKO WEWE BARUBARU ZA KUHUKUMU MKOA MZIMA KWA DHAMBI YA MTU MMOJA, HUKO NI KUKOSA UELEWA UNAOHITAJIKA.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kwamba nimechelewa kuiona thread hii, lakini nadhani ni muhimu ni kaweka mchango wangu katika hili.

  Barubaru kama kweli una uhakika na unachokiongea, ninakushauri utoe mifano halisi kushadidia hoja yako. Lakini hii ya kusema kiujumla kwamba watu wa Mara si waadilifu unakuwa unajitahidi sana kuudanganya umma.

  Sichelei kusema kwamba huenda kuna madudu uliyafanya na kujikuta katika wakati mgumu dhidi ya bosi wako, huenda alikuwa ni mtu wa kutoka mkoa wa Mara, sasa unatumia nafasi hii kuwashambulia watu wote wa mkoa wa Mara, na natambua pia chuki uliyonayo kwa Mwl .Nyerere kwahiyo haya yote nikiyaunganisha, nakuona hauna hoja wala ushahidi bali ni majungu na fitna.

  Kama kweli unadhani unayo mifano halisi ya watu wa Mara na kukosa kwao uadilifu, tafadhali iweke hadharani. Maana katika watu wachache waadilifu wanaoweza kutajwa ndani ya nchi hii, watu wa Mara hawatokosekana. Mtu mmoja mmoja bila kujali anatoka wapi anaweza kuwa na ukosefu wa uadilifu kama tunavyoshuhudia kila siku skandali mbalimbali zungumzia EPA, RICHMOND, LOLIONDO, Wanyama KIA, CHC, Nyumba za serikali, ATCL, NSSF, PPF, KIWIRA na nyengine nyingi, humo kuna watu mchanganyiko, tena ukifuatilia kwa makini hukuti mtu kutoka mkoa wa Mara katika haya madili.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sitarajii hata siku moja umkubali Nyerere kama kiongozi bora katika nchi hii. Kuanzia kwenye masimulizi ya historia ya wazee wenu wa gerezani, nilikuona rangi zako halisi tunapomzungumzia Nyerere.
  Ukweli ni kwamba wenye akili zao timamu na wanaozitumia vizuri wanajua na kukubali kwamba Nyerere alikuwa ni kiongozi muadilifu. Hakuna mtu amewahi kulalamika kwamba Nyerere katumia madaraka yake kumpora shamba, nyumba ama kampuni. Sasa hivi tunashuhudia maraisi wenu bora wanavyokimbizana kufanya biashara wakiwa ikulu. Wanaanzisha makampuni ya kuwaibia watanzania, wanajaza watoto wao, wake zao, wajomba, mashangazi na mabinamu zao serikalini na kwenye mashirika ya umma.

  Nyerere kwa uadilifu wake hata siku moja hakuwahi kumbeba mwanaye yeyote, kumuingiza katika serikali ama mashirika ya umma.
  Kwa mfano tumeambiwa watumishi wa ofisi za makao makuu ya cuf upande wa bara imejaa wapemba watupu, wenzake na maalim seif lakini upande wa zanzibar watumishi wote ni wapemba. Huo ndio uhuni mnaofanya huko kwenu na ambao mwalimu hakuufanya na asingethubutu kumvumilia mtu aufanye. Je ni sawa kusema kwamba chama chote cha cuf si waadilifu ama huo ni mzigo wa maalim na washikaji zake wachache wanaoshiriki kuchakachua ajira ktk chama?
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  TELO,

  Achana na huyu barubaru, sisi tuliokuwa naye hapa jf kwa muda mrefu tunamfahamu vizuri sana.
  Huyu amejazwa na chuki dhidi ya ukristo na zaidi ya yote amejazwa na chuki dhidi ya mwalimu Nyerere, kwahiyo sio ajabu akitumia fursa hii ya Ekerege kuboronga kuwashambulia watu wa Mara.

  Kwa taarifa yako huyu barubaru ni mpemba mmoja alisomeshwa na serikali ya Tanganyika na baadae akaajiriwa kuitumikia nchi. Lakini kutokana na kuwa na damu ya usaliti akaamua kuikimbia nchi na kujitwalia uraia wa Oman, kwahiyo pamoja na kujilipua lakini bado kila siku yeye akili yake inawaza Tanganyika. Kwahiyo huyu msaliti hayo uliyomueleza yanamtosha, na imekuwa ni muhimu kwa ajili ya kuweka sawa kumbukumbu hapa jf ili asije akatokea mtu bila kujua agenda ya siri aliyonayo barubaru akaamini uzushi wake.
   
 17. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Maranya;
  Ahsante kwa kujitokeza na kuweka haya mabo sawa. Huyu Barubaru nahisi ni chuki tu zake binafsi dhidi ya watu wa Mara. Na kitu cha ajabu ni kwamba michango yake kwenye thread mbalimbali zinanipa wasiwasi na mchango wake, kwani nilidhani ni kijana fulani mdogo ambaye bado hana uelewa wa kutosha katika mambo ya kisiasa na kiuchumi. Lkn nilipokuta mchango wake kwenye thread ya CHADEMA YAINGIA MAREKANI, ndipo nilipoishiwa nguvu kabisa kwani pale inaonekana ni mtu wa siku nyingi na wengine wanamwita DR., na hata USA amewahi/anaishi lkn michango yake haina hadhi ya kuitwa Dr., labda Dr. wa heshima.

  Hata hivyo, nashukuru kwani atakuwa ameelewa nini maana ya makosa ya mtu mmoja kutohusisha mkoa husika anakotoka mtuhumiwa.
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Chami: I need proof of allegations against TBS

  Industry and Trade Minister Cyril Chami yesterday shrugged off pressure to suspend Tanzania Bureau of Standards director Charles Ekelege, over the allegations of massive corruption in pre-shipment vehicle-inspection. The minister was reacting to a call by the Parastatal Organisations Accounts Committee Chairman Zitto Kabwe to uspend the TBS director to pave way for smooth investigations into the claims of corruption in pre-shipment vehicle inspection.

  "We (POAC) are giving the minister only one week to suspend him failure of which we will take further action," Kabwe said, adding: "If he is proved innocent, he would resume work." Kabwe has accused the TBS boss of producing false information about the entire pre-shipment vehicle inspection exercise. But minister Chami described the claims as mere allegations which had not been proved. He explained that the allegations were raised recently in the Parliament by three parliamentary committees, noting: "As the responsible minister, I need to get proof."

  "Removing Ekelege from his position would not help to establish the truth…it doesn't mean everything will be changed. It won't reduce importation of counterfeit goods. Before taking any action against Ekelege, we need to get last year's report of POAC's tour in the respective countries," noted Chami. According to Chami, POAC members toured the countries on August 2011, but since then they had not presented any report concerning their findings to his office.

  He claimed to know the saga from the media on returning from a neighboring country where he had been attending a meeting. The minister said it was not easy to suspend pre-shipment exercise or penalise a person without substantive evidence, observing doing so amounts to taking away someone's right. "The problem is not him but the system of importing the goods and how to control them from being of low quality," said Chami.

  Minister added: "I am not disputing what Members of Parliament observed. I am asking them to give us their report because before MPs go to inspect any national institution they must have permission from the Parliament. After the tour they present a report to the Bunge Office which has the responsibility of informing the government on the real situation observed by the committee. "But until today no report has been received from Bunge office," he insisted.

  Recently, the government said it was still making a follow-up on the POAC report accusing the Tanzania Bureau of Standards management of giving the oversight team wrong information on vehicle inspection offices abroad. Kabwe yesterday explained that his committee had already compiled a report on the committee's visit to Singapore and Hong Kong, where TBS claims to have set up reshipment vehicle inspection offices, and submitted the document to the Speaker of the National Assembly, Anne Makinda. Kabwe declined to disclose the contents of the report.

  POAC acting chairman Deo Filikunjombe told a recent meeting of the House committee that the bureau under the leadership of Ekelege had lied to the team by telling it that it (TBS) owns and runs vehicle inspection offices abroad. "We traveled abroad to inspect those vehicle inspection offices - going to Singapore, Hong Kong and in China - as per information from the bureau's management, but what we saw were worlds different from what we had been told (by TBS)," he said.

  Parliamentary Public Accounts Committee (PAC) chairman, John Cheyo, said Ekelege once took them to an office that was not meant for vehicle inspection, adding: "That happened when we went to Singapore and Hong Kong where, after questioning him, he said that it was only a temporary office." He subsequently turned down the 2011 TBS report, saying it was full of errors, some of which were in relation to the number of vehicles inspected and the amount of money collected during the period.

  SOURCE: THE GUARDIAN


   
 19. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hii midudu inatikiwa kufa itupishe
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Itakufaje?
   
Loading...