Madudu EPZA: Ubadhilifu, uendeshaji mbovu na wakurugenzi Miungu Watu!

Kabusinja

Member
Dec 3, 2012
6
0
Ndugu wana JF.
Mifumo ya EPZ au kama inavyojulikana kwa majina mengine kama SEZ, Freeport, Industrial Zones au majina mengine kama hayo imekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya viwanda na uwekezaji kwa nchi nyingi sana duniani, China karibu asilimia 75 ya uchumi wake ni viwanda vilivyo chini ya mfumo wa SEZ, hata ndugu zetu wa Kenya uchumi wao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na muundo huo. Pamoja na dhamira nzuri ya Serikali kuanzisha mfumo huu wa EPZ kwa ajili ya maendeleo na tija kwa Taifa, adhma hii inakwamishwa sana na baadhi ya wakurugenzi wa EPZA, wakurugenzi hawa wamekuwa kazi yao ni kuongea tu na kutaja taarifa za uongo huku wakijua kabisa kuwa wanadanganya serikali na umma kwa ujumla.

Baadhi ya mambo ambayo hata mtoto mdogo akifanya utafiti atagundua ni haya yafuatayo;

1. Uongo katika taarifa na takwimu wanazozitoa serikalini na kwa jamii
Ukisikiliza presentation zao utaona wanajigamba kuwa Taasisi ya EPZ imezalisha mpaka sasa ajira 16,500, lakini ukweli ni kuwa hakuna hata wafanyakazi elfu tano 5000, anayebisha apitie viwanda vya EPZ akikuta wafanyakazi zaidi ya hao arudi jamvini kusema mimi muongo. Hali hii imeendelea hata katika takwimu ya viwanda vinavyofanya kazi chini ya EPZ, takwimu zao zinaonyesha kuwa kuna viwanda zaidi ya 80 lakini ukipitia viwanda vyote hivyo ukweli ni kwamba ni viwanda chini ya kumi 10 tu vinavyofanya kazi. Mitaji na mauzo ya nje vyote ni vya kupikwa, haya yote yanafanywa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Taasisi hiyo Bi Zawadia Nanyaro huku Mkurugenzi Mkuu akibariki uongo huo. Nashauri wakaguzi wanaokagua maendeleo ya EPZ wasiishie tu kwenye nyaraka za ofisini wanazopewa na wakurugenzi waende kwenye hivyo viwanda vinavyodaiwa kuwepo.

2. Kutoa Leseni kwa upendeleo kwa baadhi ya watu wasiokidhi vigezo
Chini ya muundo wa EPZ utoaji leseni upo chini ya mkurugenzi wa maendeleo Bi Zawadia Nanyaro ambaye amekuwa akitoa leseni kwa wawekezaji marafiki zake wasiokidhi vigezo vya uwekezaji wengine mpaka leo wamekamata plots ambazo hawajaziendeleza kwa zaidi ya miaka mitatu licha ya kuwepo kwa sheria ya kuwanyanganya kama wasipoendeleza ndani ya miezi sita kuanzia walipopewa leseni, amekuwa akiwakumbatia na kuwatetea kwa Mkurugenzi Mkuu Dr Meru, na Dr Meru bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu na vilevile ni kujihushia credibility yake anakubaliana naye. Hali hii inasababisha wawekezaji wazalendo walio tayari kuwekeza na wenye vigezo kukosa nafasi.

3. Uhusiano mbaya kazini, Staha kwa wafanyakazi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma
Hapa sasa ndo hali mbaya, kwani ukimuuliza mfanyakazi yoyote EPZA ni nani ana personality mbaya na bad image jibu utakalopata haraka ni Zawadia Nanyaro, Zawadia amekuwa siku zote akilalamikiwa kwa kauli zake mbaya kwa wafanyakazi, fitina na majungu kupeleka maneno ya kuwaua wafanyakazi wenzake tena wa chini yake kuwa hawawezi kutenda kazi na Mkurugenzi mkuu kwa sababu inasemekana wana mahusiano ya kimapenzi kazini inamlazimu akubali ili kumridhisha kumbe anachofanya ni kujichafulia career yake hasa kipindi hiki anachokaribia kustaafu, nadhani uhusiano huu ndo unaomfanya ashindwe kumchukulia hatua pale anapotumia mali ya taasisi kwa shughuli binafsi, kwa mfano ratiba ya gari la serikali STK 5768 limekuwa likifanya kazi za binafsi za Mkurugenzi Zawadia Nanyaro kwa ratiba ifuatayo, asubuhi linakuwa school bus kupeleka watoto katika shule mbili tofauti, mchana linafanya kazi za nyumbani, ikifika saa nane tu haijalishi kuna shughuli gani kiofisi gari lazima liondoke kufata watoto na kuwarudisha nyumbani huku shughuli za serikali zikilala, achilia mbali jumamosi na jumapili kupeleka watoto kuimba kanisani, sijui kama kila mkurugenzi angekuwa anafanya hivi kama shughuli za kiofisi zingefanyika. Me namshauri Mkurugenzi Mkuu aangalie yasije kumkuta ya wenzake wa TBS na TANTRADE ambazo zote pamoja na EPZA ni taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda.

Naomba nieleweke kuwa lengo si majungu ndo maana nimeleta takwimu, lengo ni kurekebisha baadhi ya watendaji wakuu wa hizi taasisi zetu za umma wanaodhani kuwa taasisi ni mali zao, huku wakifanya ubadhilifu wa mali za umma na utendaji sifuri. Naomba niachie wanajamvi wengine wachangie then nitarudi baadaye na taarifa nyingine. Mabadiliko ya kweli huanzia JF. Nawasilisha!
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
What a no-man's land!Kila uchao ufisadi ujambazi mauaji wizi unyang'au, sanaa na kila upuuzi! Tushikwe wapi ndipo tustuke?
 
ALINDAO

Member
Nov 21, 2011
6
0
Mtoa mada, una uhakika? au una lako? Nimefanya kajiutafiti kadogo pale epza na kugundua kuwa maneno yako japo ni mengi, uongo pia ni mwingi! - mfano; EPZ Kisongo Arusha pekee ina wafanyakazi zaidi ya 8000; Mazava Morogoro 1650; Touku Dsm 355; hapo tu tayari ni zaidi ya 10,000! Upo hapo? Nimepewa list ya viwanda 60, na zaidi ya 40 hata mimi navifahamu. Matumizi ya magari tusidanganyane, hata wewe ukipewa utafanya hivyo hivyo! Hujatoa ushahidi wa ubadhirifu zaidi ya majungu!! Nakushauri uchape kazi kwa bidii ili nawe uukwae ukurugenzi; yakikushinda, jiondoe kuliko kupika majungu!
 
Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
886
368

Unatetea ubadhirifu wewe !! Tumelogwa sisi.
 
Kabusinja

Member
Dec 3, 2012
6
0
By ALINDAO
Mtoa mada, una uhakika? au una lako? Nimefanya kajiutafiti kadogo pale epza na kugundua kuwa maneno yako japo ni mengi, uongo pia ni mwingi! - mfano; EPZ Kisongo Arusha pekee ina wafanyakazi zaidi ya 8000????; Mazava Morogoro 1650; Touku Dsm 355; hapo tu tayari ni zaidi ya 10,000! Upo hapo? Nimepewa list ya viwanda 60, na zaidi ya 40 hata mimi navifahamu. Matumizi ya magari tusidanganyane, hata wewe ukipewa utafanya hivyo hivyo! Hujatoa ushahidi wa ubadhirifu zaidi ya majungu!! Nakushauri uchape kazi kwa bidii ili nawe uukwae ukurugenzi; yakikushinda, jiondoe kuliko kupika majungu!

  • Nadhani ALINDAO umetumwa kuja kutetea na kuwasafisha hao waliokutuma, again bado wakakupa na takwimu za uongo, me naomba tusiwe wavivu, hebu jaribu hata kutembelea EPZ kisongo Arusha uone huo uongo wa wafanyakazi aliouandika alindao, nikikuambia utaje angalau Viwanda vya EPZ kumi 10 tu vinavyofanya kazi, I can assure you, you will hard count to ten thats the plain fact and I can bet with you for that! Hapa hatuongelei majungu we ndugu yangu ALINDAO tunazungumzia masuala nyeti kwa mustakabali wa Taifa letu. Pia hatuzungumzii mfumo mzima bali tunazungumzia watendaji wabovu wanaoharibu juhudi za Serikali katika kukuza uchumi. Naona pia umenikumbusha mwenyewe kuwa sijatoa ushahidi kuhusu ubadhadhirifu? Hili like wazi na nod maana sikuona haja ya kwanza kurudia the obvious, ila nadhani wadau wengine watakujibu hilo. Jiandae kutetea tena.
 
MERCYCITY

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
986
1,091
Ninafikiri haya ni majungu. Wewe una ugonvi fulani na huyo dada. Maana juzi tu ulikuwa hapa na ukasema ulinyimwa safari ya Arusha. Ukaambiwa ukajipange uje na data za ubadhirifu. Sasa umerudi na data za uongo. Rafiki yangu maisha hayaendi hivyo kwa kuharibiwa watu kwa kuwatangaza magazetini. Peleka data hizo kwa mwajiri wake zichunguzwe, Sasa sisi unatuletea hapa hili tufanye nini. Kwanza kumwambia mtu ana uhusiano wa mapenzi na bosi wake bila kuwa na uhakika siyo kwamba unahatarisha familia za watu. Mimi ninafikiri wewe unahitaji msaada wa mawazo, mambo ya mapenzi na mtu acha kukurupuka yana adhari zake katika familia. Embu naona ujichunguze moyo wako kama unayosema yanatoka moyoni kweli na ni ya kweli au umepania kulipiza kisasi. Uwezi kupata maendeleo kwa kulipiza kisasi maana watu wakikujua kila utakapokwenda kufanya kazi utakutana na hayo hayo. Ninafikiri ni mwanya tu wa kula kama ungeupata sema kweli tusingesikia haya majungu.
 
Adam Msafiri

New Member
Feb 9, 2012
3
0
JF muwe mnaruhusu taarifa zenye ukweli na utafiti, ukisoma unaona Kabusinja ana issue binafsi na huyo Zawadia, kuna nahisi, nadhani, inasemekana nyingi tu, mkiruhusu hisia humu mnakuwa irrelevant.

Siamini taasisi kama EPZA inaweza kufanya kazi kwa matakwa ya mtu mmoja bila checks and balances, hizo fitna, majungu, ubadhirifu etc ni zipi specifically? Kile kiwanda cha net tu cha A to Z Kisongo Arusha kina zaidi ya wafanyakazi 5,000.
Unaweza ukakuta Kabusinja hajui kuwaa mikataba mingine ya kikazi inaruhusu matumizi ya gari na vitu vingine, mikataba ya kazi sio standard.

Huyu jamaa alikuja juzi hapa akiwa analilia safari anaonesha ndio walewale. Watanzania ndio hivi chuki binafsi, juzi MD wa NBC alipigwa zengwe na whistle blower mfitini, bahati nzuri wale wana system transparent wakachunguza wakakuta fitna tu za waswahili kama huyu hapa. Hatutaendelea kwa majungu ila kwa kuchapa kazi kwa bidii na maarifa. AM.
 
ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
Mtoa mada, una uhakika? au una lako? Nimefanya kajiutafiti kadogo pale epza na kugundua kuwa maneno yako japo ni mengi, uongo pia ni mwingi! - mfano; EPZ Kisongo Arusha pekee ina wafanyakazi zaidi ya 8000; Mazava Morogoro 1650; Touku Dsm 355; hapo tu tayari ni zaidi ya 10,000! Upo hapo? Nimepewa list ya viwanda 60, na zaidi ya 40 hata mimi navifahamu. Matumizi ya magari tusidanganyane, hata wewe ukipewa utafanya hivyo hivyo! Hujatoa ushahidi wa ubadhirifu zaidi ya majungu!! Nakushauri uchape kazi kwa bidii ili nawe uukwae ukurugenzi; yakikushinda, jiondoe kuliko kupika majungu!
kwenye red hapo umeharibu credibility ya mchango wako, ni ngumu kuamini hata vingine ulivyochangia. unaonekana ni walewale. si kwamba umeniudhi tu bali nakuchukia from the bottom of my heart.
mtu akikuona atadhani una kichwa kumbe ni kifuu cha nazi.
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,503
2,938
Kabusinja,

Wewe unasema kuna ajira 5000 tu! pengine kweli pengine sio kweli ila nakukumbusha kitu kimoja. Chukulia mfano wa kiwanda cha saruji Wazo Hill pale kunaweza kuwa na ajira labda 200 lakini unaweza kukuta kuna ajira ambazo zinategemea hicho kiwanda nje ya hata 1800. Kwahiyo naomba kwa ajili la ajira ujipange upya maana unazungumzia tU direct employment lakini wapo wengi nje ya hivyo viwanda wanaopata ajira kutoka na kuwepo kwa hivyo viwanda.
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
252
Huyu jamaa ni kilaza sana maana ajira anazoongelea sijui ni zipi. Ajira ni kuanzia yule mzalishaji wa kwanza mpaka kabla ya mlaji wa mwisho. Mleta uzi acha hasira, fanya kazi maana huko serikalini majungu nasikia ndo sehemu ya kazi.
 
tru rasta

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
303
323
Ndugu wana JF.
Mifumo ya EPZ au kama inavyojulikana kwa majina mengine kama SEZ, Freeport, Industrial Zones au majina mengine kama hayo imekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya viwanda na uwekezaji kwa nchi nyingi sana duniani, China karibu asilimia 75 ya uchumi wake ni viwanda vilivyo chini ya mfumo wa SEZ, hata ndugu zetu wa Kenya uchumi wao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na muundo huo. Pamoja na dhamira nzuri ya Serikali kuanzisha mfumo huu wa EPZ kwa ajili ya maendeleo na tija kwa Taifa, adhma hii inakwamishwa sana na baadhi ya wakurugenzi wa EPZA, wakurugenzi hawa wamekuwa kazi yao ni kuongea tu na kutaja taarifa za uongo huku wakijua kabisa kuwa wanadanganya serikali na umma kwa ujumla.

Baadhi ya mambo ambayo hata mtoto mdogo akifanya utafiti atagundua ni haya yafuatayo;

1. Uongo katika taarifa na takwimu wanazozitoa serikalini na kwa jamii
Ukisikiliza presentation zao utaona wanajigamba kuwa Taasisi ya EPZ imezalisha mpaka sasa ajira 16,500, lakini ukweli ni kuwa hakuna hata wafanyakazi elfu tano 5000, anayebisha apitie viwanda vya EPZ akikuta wafanyakazi zaidi ya hao arudi jamvini kusema mimi muongo. Hali hii imeendelea hata katika takwimu ya viwanda vinavyofanya kazi chini ya EPZ, takwimu zao zinaonyesha kuwa kuna viwanda zaidi ya 80 lakini ukipitia viwanda vyote hivyo ukweli ni kwamba ni viwanda chini ya kumi 10 tu vinavyofanya kazi. Mitaji na mauzo ya nje vyote ni vya kupikwa, haya yote yanafanywa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Taasisi hiyo Bi Zawadia Nanyaro huku Mkurugenzi Mkuu akibariki uongo huo. Nashauri wakaguzi wanaokagua maendeleo ya EPZ wasiishie tu kwenye nyaraka za ofisini wanazopewa na wakurugenzi waende kwenye hivyo viwanda vinavyodaiwa kuwepo.

2. Kutoa Leseni kwa upendeleo kwa baadhi ya watu wasiokidhi vigezo
Chini ya muundo wa EPZ utoaji leseni upo chini ya mkurugenzi wa maendeleo Bi Zawadia Nanyaro ambaye amekuwa akitoa leseni kwa wawekezaji marafiki zake wasiokidhi vigezo vya uwekezaji wengine mpaka leo wamekamata plots ambazo hawajaziendeleza kwa zaidi ya miaka mitatu licha ya kuwepo kwa sheria ya kuwanyanganya kama wasipoendeleza ndani ya miezi sita kuanzia walipopewa leseni, amekuwa akiwakumbatia na kuwatetea kwa Mkurugenzi Mkuu Dr Meru, na Dr Meru bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu na vilevile ni kujihushia credibility yake anakubaliana naye. Hali hii inasababisha wawekezaji wazalendo walio tayari kuwekeza na wenye vigezo kukosa nafasi.

3. Uhusiano mbaya kazini, Staha kwa wafanyakazi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma
Hapa sasa ndo hali mbaya, kwani ukimuuliza mfanyakazi yoyote EPZA ni nani ana personality mbaya na bad image jibu utakalopata haraka ni Zawadia Nanyaro, Zawadia amekuwa siku zote akilalamikiwa kwa kauli zake mbaya kwa wafanyakazi, fitina na majungu kupeleka maneno ya kuwaua wafanyakazi wenzake tena wa chini yake kuwa hawawezi kutenda kazi na Mkurugenzi mkuu kwa sababu inasemekana wana mahusiano ya kimapenzi kazini inamlazimu akubali ili kumridhisha kumbe anachofanya ni kujichafulia career yake hasa kipindi hiki anachokaribia kustaafu, nadhani uhusiano huu ndo unaomfanya ashindwe kumchukulia hatua pale anapotumia mali ya taasisi kwa shughuli binafsi, kwa mfano ratiba ya gari la serikali STK 5768 limekuwa likifanya kazi za binafsi za Mkurugenzi Zawadia Nanyaro kwa ratiba ifuatayo, asubuhi linakuwa school bus kupeleka watoto katika shule mbili tofauti, mchana linafanya kazi za nyumbani, ikifika saa nane tu haijalishi kuna shughuli gani kiofisi gari lazima liondoke kufata watoto na kuwarudisha nyumbani huku shughuli za serikali zikilala, achilia mbali jumamosi na jumapili kupeleka watoto kuimba kanisani, sijui kama kila mkurugenzi angekuwa anafanya hivi kama shughuli za kiofisi zingefanyika. Me namshauri Mkurugenzi Mkuu aangalie yasije kumkuta ya wenzake wa TBS na TANTRADE ambazo zote pamoja na EPZA ni taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda.

Naomba nieleweke kuwa lengo si majungu ndo maana nimeleta takwimu, lengo ni kurekebisha baadhi ya watendaji wakuu wa hizi taasisi zetu za umma wanaodhani kuwa taasisi ni mali zao, huku wakifanya ubadhilifu wa mali za umma na utendaji sifuri. Naomba niachie wanajamvi wengine wachangie then nitarudi baadaye na taarifa nyingine. Mabadiliko ya kweli huanzia JF. Nawasilisha!

Join Date : 3rd December 2012
Posts : 4
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given0taarifa zako zinaelezea vyema nia yako.try again later
 
Muadilifu

Senior Member
Sep 26, 2007
149
22
Wana-Jf, kutokana na mlolongo wa mtoa mada hii inadhihirisha kuna msukumo wa bifu kati yake na mkurugenz aliyemtaja? ukiangalia na kufanya analysis utakuta hapo hakuna kitu, maelezo yake yote yamejaa ubabaishaji na wivu. Kama mimi ningekuwa bosi wake na kwa hakika namshauri amtafute na amtimue kazi kwa maana mtu yeyote anayelalamika kupitia kwenye mitandao bila kua-address tatizo lake kwa mamlaka zinazohusika kwa taratibu ambazo shirika lao limeweka, kwa kweli ni mtu hatari sana.
 
SASATELE

Senior Member
Sep 12, 2011
167
89
wadau, mimi namfahamu Zawadia at a personal level. sio rafiki yangu walal nini lakini ni jirani yangu tu. Yule dada ni jembe lisilo la kawaida. Alikuwa TBL akafanya mambo hadi wawekezaji wakampenda sana. Alikuwa anavuta mkwanjwa wa maana!! Ana kichwa na anachapa kazi vibaya. Bosi yeyote aliekuwa rational lazima utampenda na kumpa nafasi ya karibu akushauri. Sasa huku chini kuna vilaza wanataka vijisafari wapate per diem. Wakiambiwa leta issue hawana issue wanaanza majungu. Katika ofisi za serikali kuna watu kila siku wanasafiri kwenda nje kufanya presentations na vitu kama hivyo. Wengine hawapewi kwa sababu za wazi kabisa- capaity hawana. Sasa hao wasiokuwa na capacity wataanza majungu na kuloga ili wachukue nafasi zenye visafari wapate per diem wamalizie vibanda vyao huko mabonde kuinama> basi hauishi majungu na wivu!! Acheni hizo bana, fanyeni kazi kwa bidii. If you are not important you will not be seen and opportunities will pass u by!!
 
Zinedine

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,188
694

Sina nia ya ku-support alichosema mtoa mada, lakini hapo penye red pa kwanza umesema uongo. Kimsingi overall performance ya EPZA ni hovyo kwani imekaa katika namna ya Uchumi wa Tanzania unavyosifiwa na wenyewe lakini hakuna repercusion yoyote katika maisha ya wananchi wa kawaida ambao ndo wengi.
Kuhusu huyu dada simfahamu in personal lakini namfahamu sana kikazi kwani niliwahi kumfundisha kazi somewhere katika carrier zake-Not bad, not good, just average which is good, but in reality she has more personal attack nadhani ndo hidden feeling ya mtoa mada. Kwa sasa siko naye kikazi kwani nilishaachana na kuajiriwa lakini naweza kuthibitisha kuwa ana "over mass ambitious" ya kufika juu hivyo watu wa tabia hii wana tendency ya kufanikiwa kufika huko kwa kutumia njia yoyote hata kama si nzuri na hivyo wanapofika wanakuwa na tendency ya kujenga dharau kwa watu wengine kwa kuwa wana-happen kuwa juu katika age ndogo ukilinganisha na mafanikio yao, which is also bad. Hii red ya pili haina maana, yoyote kwa kuwa under-performance ya taasisi za kiserikali na serikali na serikali yenyewe ndo source ya hao watu kwenda kujenga huko mabonde kuinama, otherwise kama Housing entity zetu zingekuwa zinazingatia vipato vya wananchi wake, kusingekuwa na pressure ya kujenga huko na offcourse, fedha nyingi za watu binafsi zingesaidia katika uwekezaji wa kijasiriamali badala ya kutupwa huko mabonde kuinama. Fuatilia Housing charge za kwa hayo mashiriki yanayojenga nyumba utabaini kuwa kuna zaidi ya matatizo juu ya walengwa wa nyumba husika. Kuhusu matumizi ya gari mtoa mada anatuhimiza kuwa suala la Mtendaji wa Serikali kuhudumiwa na gari la serikali kwa kweli si sahihi, ni bora akopeshwe, au anunuliwe then aachiwe mwenyewe kila kitu alitumie atakavyo, maana hili si kwa Zawadia tu, hata madereva wanaoendesha gari za serikali hawayajali magari haya which is not good.
 
SASATELE

Senior Member
Sep 12, 2011
167
89
Sawa Zinedine, Umeongea kwa busara sana. Asante. I am retracting the statement "mabonde kuinama" in my earlier post. Nakubaliana nawe pia kwamba Zawasia is over ambitious na ana nyodo lakini nasisitiza ni mchapakazi na ni above average Tanzanian woman wa umri wake
 
Kabusinja

Member
Dec 3, 2012
6
0
Sina nia ya ku-support alichosema mtoa mada, lakini hapo penye red pa kwanza umesema uongo. Kimsingi overall performance ya EPZA ni hovyo kwani imekaa katika namna ya Uchumi wa Tanzania unavyosifiwa na wenyewe lakini hakuna repercusion yoyote katika maisha ya wananchi wa kawaida ambao ndo wengi.
Kuhusu huyu dada simfahamu in personal lakini namfahamu sana kikazi kwani niliwahi kumfundisha kazi somewhere katika carrier zake-Not bad, not good, just average which is good, but in reality she has more personal attack nadhani ndo hidden feeling ya mtoa mada. Kwa sasa siko naye kikazi kwani nilishaachana na kuajiriwa lakini naweza kuthibitisha kuwa ana "over mass ambitious" ya kufika juu hivyo watu wa tabia hii wana tendency ya kufanikiwa kufika huko kwa kutumia njia yoyote hata kama si nzuri na hivyo wanapofika wanakuwa na tendency ya kujenga dharau kwa watu wengine kwa kuwa wana-happen kuwa juu katika age ndogo ukilinganisha na mafanikio yao, which is also bad. Hii red ya pili haina maana, yoyote kwa kuwa under-performance ya taasisi za kiserikali na serikali na serikali yenyewe ndo source ya hao watu kwenda kujenga huko mabonde kuinama, otherwise kama Housing entity zetu zingekuwa zinazingatia vipato vya wananchi wake, kusingekuwa na pressure ya kujenga huko na offcourse, fedha nyingi za watu binafsi zingesaidia katika uwekezaji wa kijasiriamali badala ya kutupwa huko mabonde kuinama. Fuatilia Housing charge za kwa hayo mashiriki yanayojenga nyumba utabaini kuwa kuna zaidi ya matatizo juu ya walengwa wa nyumba husika. Kuhusu matumizi ya gari mtoa mada anatuhimiza kuwa suala la Mtendaji wa Serikali kuhudumiwa na gari la serikali kwa kweli si sahihi, ni bora akopeshwe, au anunuliwe then aachiwe mwenyewe kila kitu alitumie atakavyo, maana hili si kwa Zawadia tu, hata madereva wanaoendesha gari za serikali hawayajali magari haya which is not good.

ZINEDINE umetoa a very fair analysis kuhusu Zawadia may be in a better way than I wanted to, u have said it all, mimi sina kinyongo na Zawadia ila sikubaliani na tabia yake mbaya ya dharau, nyodo na kujiona yeye is everything, na nashukuru hata mtetezi wake ndugu SASATELE amekubaliana na hilo. Kama Zawadia angekuwa performer basi EPZA ingekuwa way over the sky kwa sababu idara yake nod muhimili Mkuu wa Taasisi hii. Labda nikukumbushe kitu ambacho pengine hukukijua ni kuwa hata nafasi yake kwenye tangazo la kazi ilitangazwa kwa qualification tofauti kabisa na zake. Tangazo hilo (of which I have the extract) lilitaka candidate wa post hiyo awe ni Engineer tena registered na ERB na vile vile awe Member of Institution of Engineers Tanzania (MIET) of which Zawadia Lacks, yeye alisoma bcom Akaja kuipandishia MBA baadaye. Sasa aliingiaje EPZA that's another twist, na kwa bahati mbaya kwa taasisi au nzuri kwake kipindi hicho ajira serikalini zile kuwa zinafanywa na kuratibiwa na taasisi husika na siyo secretariet ya ajira kama ilivyo sasa ambapo sidhani hata kama angeingia kwenye mchujo. My theory is pengine under performance ya EPZ ambayo in big chunk iko kwenye idara yake inatokana na ukweli kuwa she didn't qualify for the post at first place, pengine nisimlaumu sana kwa hilo.

Kuhusu Magari ya serikali, jamani Kanuni za utumishi wa umma ziko wazi kabisa, kuwa yatatumika kwa shughuli za kiofisi na kwa muda wa ofisi, sasa inapotokea shughuli za ofisi zinalala eti kisa gari lina fixed timetable ya kubeba watoto wa Mkurugenzi kupeleka shule na kwenda kubembea that's very wrong na anajitengenezea unnecessary attention yeye mwenyewe, mbona wakurugenzi wenzake including Mkurugenzi Mkuu hafanyi kitu Kama hicho.

Jamani on a fair look majority ya Kampuni nyingi za EPZA ni za kiujanjaujanja zinauza bidhaa zake ndani ya nchi, contrary na SHERIA yao inayotaka kuwa zaidi ya 80% ya production iwe ni for export, only kampuni ya Mazava fabrics, Tooku garments, na zingine mbili tatu ndo zinauza nje, the rest zinauza ndani asilimia mia, hii inaumiza kampuni za wazawa ambazo zinalipa kodi serikalini, ikumbukwe kuwa kampuni zilizo chini ya Mfaume wa EPZ hazilipi kodi yeyote.

Labda niseme kwa kumalizia kuwa hebu tujaribu kuwa wazalendo na nchi yetu, pale serikali inapojitahidi kuanzisha stimulus za kiuchumi Kama hizi za EPZ na SEZ basi wahusika na waliopewa dhamana wafanye kazi kutekeleza dhamira njema ya Serikali na siyo kujiona ni kuwa sasa same pasta sehemu ya kutafuna, wanawaza safari kila siku huku mambo ya msingi ya taasisi yanabaki yanalala, ikifika mwisho mwaka wanatoa takwimu za kutengeneza ili kazi ionekane inafanyika wakati in reality what is reported is not what is happening on the ground!
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
11,992
11,163
Only in Tanzania yaani hii nchi ni ya ajabu sana ikija kwenye maswala ya maendeleo ya taifa, ni majungu kila kukicha watoa habari mara nyingi uandika as if they are addressing those inside the circles.

Mfano huyu kabusinja kaja na malalamiko chungu mtele how do you side with him or his opponents. Anatuambia kuna upendeleo kwenye kutoa plots kwenye reserved areas, upendeleo unakuja vipi are investors given grants au mwenye hela ndio anawekeza....this leaves the question of those given the plots without developing? how do you critisize or defend such a statement (did they fail raising investment funds or misused the given funds). Hili tujue upendeleo hapa unafananaje?

Halafu role ya huyo Mdada/Mama, mhuni apparently according kwa mwandishi ni hipi, yeye ni mtoa plots tu and what are is duties and how is her success measured in terms of her job description.

Ndio jamaa kaongelea umuhimu wa kukuza ajira kwenye hizi programmes but how are those jobs supposed to be created. Worst of before the overseer is employed, the job description required an engineer to oversee the programmes in an economical sector, mungu wangu.

What the heck is going on in this country ni kama vile nchi inaongozwa na headless chickens and things are allover the place.

Out of topic, mtu akipata muda apitie new regulations za pension funds and the new regulators (if he can differentiate the role of Central bank and the regulators binafsi zinanipa tabu) my god utaona malalamiko ya walipiaji yapo vingine na rules zipo kivingine yaani amna maelekezo kwa walipiaji kuwa wanapolipia lazima wajulishwe hizo pesa zinaenda ekezewa wapi na huo mfuko (that is supposed to be the role of the employer for the benefit of employee), despite clear guidelines kwenye new act watu hawafuati masharti kabisa inavyoonekana yaani ni fujo tupu.

Cha aibu kabisa sheria inasema pension funds are not to invest in equity (venture capital firms) institutions which can offfer aspiring business people capital to start with and a grip to moniter their progress. No wonder kule kwenye jukwaa la biashara wanalilia kuungana because of shortage of funds and the fear of big coorparates taking them out of business (sasa basi unajiuliza yule bwana anajua athari za kuungana or he is just desperate). Which brings us to the final point what are the policies for SME with the current government? Something tells me zipo somewhere and very clear hila watoa habari ni wavivu kama mleta hii thread kutoa picha kamili.

Only in Tanzania ndio maana hata wakenya wanaweza kutu-exploit. Like i said not everybody is suitable for every post bwana mteuzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom