Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
...SteveD, unalifikiriaje suala hili?
Mbu,
Kama mtoto ana wazazi walio hai na anafamilia iliyopo karibu naye, mtoto huyo haitaji kuchukuliwa na kupelekwa kwingine kulelewa. Gharama ambazo angetumia kwa ajili ya mtoto mmoja akiwa huko ng'ambo na kukaa naye kama mtoto wake wa kumzaa, naamini ni kubwa sana. Angeweza kabisa kuendeleza kundi jingine la watoto wengine wengi kwa gharama hizo, maana maisha ya ma-celebrity na watoto wao huko ng'ambo tunayasikia yallivyo aghali.
Kama huyo mtoto angelikuwa ametelekezwa au kuwa amekuwa yatima, kwa maoni yangu mimi ningemsupport Madonna kwa 75% na iliyobakia ningeiweka kwenye support ya maelezo hapo juu, yaani ku-support kundi kubwa huko Malawi. Nimesoma kuwa Madonna tayari ana support ma/kundi la watoto wanaolelewa kwenye vituo. Hata hivyo naamini bado anaweza akajitolea zaidi na kuendeleza vituo vingine kwa gharama ya mtoto mmoja ambaye angeenda naye kumlea.
Support yangu kwa 75% ya kumchukua mtoto kama ametelekezwa jumlajumla au amekuwa yatima, ni kutokana na imani yangu kuwa, mazingira kama haya yakimkumba mtoto wa miaka michache na akawa hana huduma zinazohitajika pahala alipo, basi haki (mahitaji) ya mtoto huyo kuishi na kulelewa kwa neema na mtu mwingine na pahala pengine inaongezeka zaidi, maana tayari huyo mtoto atakuwa amepungukiwa na viunganishi asilia vya jamii yake kutokana na upweke alio nao.
SteveD.