Madonna Alikuwa Akimtaka Kimapenzi Michael Jackson | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madonna Alikuwa Akimtaka Kimapenzi Michael Jackson

Discussion in 'Entertainment' started by Mbonea, Sep 28, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Madonna
  Monday, September 28, 2009 3:43 AM
  Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson aliyefariki na kuzikwa wiki chache zilizopita alikuwa akifikiria kwamba nyota mwenzake wa muziki wa Pop, Madonna alikuwa akimtaka kimapenzi lakini aliamua kumtosa kwakuwa Madonna hana mvuto wowote.


  Katika mahojiano aliyofanya mwaka 2001 na rafiki yake Rabbi Shmuley Boteach ambayo yameanikwa wiki hii, Michael Jackson alisema “Nafikiri Madonna ananipenda sana na anataka niwe mpenzi wake lakini sina mapenzi yoyote kwake”.

  “Anafanya mambo mengi ya kipuuzi, najua hatuendani, hana mvuto wowote wa kike” alisema Michael Jackson.

  Mbali na kufikiria kuwa Madonna alikuwa akimpigia misele, Michael alifikiria pia kuwa Madonna anamwonea wivu kwa mafanikio aliyopata kimuziki.

  “Wanaonyesha kukupenda kwakuwa wanajua una mafanikio lakini wana wivu sana wanatamani wachukue nafasi yako. Madonna ni mmoja wa watu wenye kunionea wivu, anajaribu kuwa kama msichana na mwanamke kwa wakati mmoja”, alisema Michael.

  Katika mahojiano hayo Michael Jackson alikiri pia kumnyemelea kimapenzi rafiki yake wa zamani Elizabeth Taylor ambaye alimzidi kiumri Michael kwa miaka 25.

  Hata hivyo Michael alisema kwamba aliamua kutozifuata hisia zake kwa kuhofia kuandikwa vibaya na magazeti kwamba ana mpenzi mkubwa kuliko yeye kwa miaka 25.

  Mahojiano hayo ya Michael yamechapishwa kwenye kitabu kipya kilichotolewa hivi karibuni kinachokwenda kwa jina la “The Michael Jackson Tapes: A Tragic Icon Reveals His Soul In Intimate Conversation".
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Now that Michael is dead we will hear all sorts of nonsense, afterall the dead tell no tales!
   
Loading...