- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Dkt. Sospeter Mathayo anaeleza kuwa Vidoti vyeusi kwenye unyayo vinaweza kutokea kwa mtu yeyote, awe na VVU au asiwe navyo. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonesha uhusiano kati ya vidoti hivyo na maambukizi ya VVU, hivyo hali ya mtu haiwezi kutambuliwa kwa kuangalia unyayo. Njia pekee ya kuthibitisha hali ya VVU ni kupitia vipimo vilivyoidhinishwa vya VVU.
Juni 11, 2025 Wizara ya Afya ilikanusha taarifa iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia video ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Mentor Chery and WellbeingHub, akidai kuwa moja ya dalili za mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) ni uwepo wa vidoti vyeusi katika dole gumba hadi kwenye kisigino.
Wizara ya Afya ilisisitiza kuwa huwezi kumtambua mtu aliye na VVU kwa kumtazama kwa macho wala kupitia dalili hizo alizotaja mtu huyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, njia sahihi na ya pekee ya kujua hali ya maambukizi ya VVU ni kwa kufanya vipimo vya afya katika vituo rasmi vya kutolea huduma.
"Njia pekee ambayo mtu anaweza kutambua hali yake ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni kufanya vipimo kwa mujibu wa miongozo iliyopo. Hivyo, Wizara inaiasa jamii kupuuza taarifa hizo na wale wote wanaotaka kujua hali zao za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, wafike katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupima na kutambua hali zao.
Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya inatoa onyo kwa watu wote ambao si wataalam wa afya, kujiepusha kutoa taarifa za afya huku wakijua hawana weledi au taaluma ya kufanya hivyo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayetoa na kusambaza taarifa zinazopotosha jamii na kufifisha juhudi za Serikali na wadau katika kupambana na maambukizi ya VVU." Taarifa hiyo ilisisitiza