Madiwani wote ishirini Monduli wabwaga manyanga CCM, wahamia CHADEMA

Kadi za CCM wamepata wapi wakati walizichoma hadharani? Hilo gazeti litakuwa Uhuru. Na CCM wanavyotaka sifa, TBC CCM lazima ingeitoa tu. Hicho ni kilio cha mamba machozi naenda na maji.
 
Kwa akili ya kawaida tu, haiwezekani CCM wasingekaa kimya hasa katika kipindi hiki kigumu. Unawajua Lumumba au unawasikia wale ndio wazee wa propaganda. wangeitisha mpaka TV za kenya kuonyesha jinsi CHADEMA walivyo waongo.
 
Tumewashihudia kwa macho yetu wakichana kadi za ccm na kuzitia moto,timeshuhudia wakikabidhiwa kadi mpya za chadema,wengi wao nimekuwa nawafahamu vyema,kwa hilo la kuchukua fomu za ccm labda ni habari mpya,inawezekana tu,ila hatujaona wala kusikia hilo kabla ya gazeti la UHURU la leokuandika hivyo,hakuna ushahidi,over.
 
CCM bhanaaaaa, imechanganyikiwa!!!! Sasa inafuata mkondo wa yule Waziri wa Habari wa Iraq enzi za Sadam Hussein! AIBUUUUUUUUU!!!!!!!
 
Me nafikiri umeona vibaya kanunue hilo gazeti au wewe pia mfanyakazi wa tbc na gazeti la uhuru? Pole zako
 
ccm walikanusha kwenye tv wale madiwani wakahojiwa wakasema ni kweli wamerudisha kadi
 
wao wahame tu. inaonesha walivyowanafiki. inamaana kama lowasa angeshinda hapo ccm ingekua nzuri. Tunawajua sana nyie mlisha tafuta urais kwa kila mbinu mnafeli. hii ndio tanzania organised body. kaeni mtulie endelezeni biashara zenu tu, urais sahauni ng'o.
 
Katika kipindi cha watanzania tuongee magazeti asubuhi ya leo tarehe 20/07/2015 kuna gazeti limeandika wale madiwani wa Monduli waliotajwa kujiunga na CHADEMA wamechukua fomu za kugombea udiwani kupitia CCM.

My take: Je, hii ilikuwa ni propaganda za CHADEMA ili waungwe mkono na wapenzi wa Lowassa kuelekea harakati zao za kukamata dola?

Chanzo: Star TV

Star TV sio gazeti, we tuambie ni gazeti gani limeandika tukaliangalie.
 
Back
Top Bottom