Madiwani wawili wa CCM Rorya wajiudhuru

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,428
2,000
VITA ya Uenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya imeacha makovu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya madiwani wake wawili, Ongujo Wakibara na Lukio Ambogo, kujivua udiwani kwa kile walichodai kunusuru mpasuko zaidi ndani ya chama wilayani Rorya.

Madiwani hao, Wakibara wa Kata ya Mkoma Shirati na Ambogo wa Kata ya Nyahongo, walikuwa wanawania uenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo iliyoanzishwa katika miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, mmoja wa aliyetangaza kujiengua jina lake limo katika orodha ya wana CCM watatu waliopitishwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa ajili ya kuwania uenyekiti wa halmashauri hiyo.

Huyo ni Wakibara ambaye amepitishwa kuchuana na Charles Ochele na Yamo Odemba. Lakini habari zaidi zinasema kwamba, Wakibara amehofia kuendelea kwa makundi kutokana na kuwa na tofauti na wenzake waliopitishwa, hivyo kuamua kujiweka kando.

Kutokana na malumbano ya mara kwa mara yasiyoisha na kusababisha chuki ndani yetu, sisi tunaona kuachia ngazi za udiwani na kuwaachia wanachama wengine na tutabaki kuwa wanachama wa kawaida wa CCM," alisema Wakibara huku Ambogo akiwa pembeni yake.

Waliokatwa katika mchakato huo, Ambogo na Okea Ogigo ndio wanaotajwa kutokuwa na makundi na kwamba ndio waliokuwa wamepitishwa katika hatua za awali za mchujo, tofauti na waliopitishwa.

Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwam alikuwa Rorya kusikiliza malalamiko ya baadhi ya madiwani zaidi ya 10 waliokuwa wametishia kujiuzulu uanachama na kuachia ngazi baada ya majina ya wagombea waliokuwa wanawataka kukatwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara chini ya Mwenyekiti wake, Makongoro Nyerere na Katibu, Ndekubali Ndengaso.

Kwa ujumla, kumekuwa na makundi ndani ya CCM katika Wilaya ya Rorya, hali inayotishia
ustawi wa chama ndani ya wilaya husika.

Mvutano ulianzia wakati wa kuamua panapofaa kuwa makao makuu ya Wilaya mpya ya Rorya, wengine wakitaja Shirati yawe makao makuu na wengine Ingiri Juu, hatua iliyosababisha kuchafuka kwa hali ya amani na kuilazimu Serikali kuingilia kati.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom