Madiwani wawe na Elimu isiyopungua kidato cha nne

Mopero

Senior Member
Apr 5, 2012
107
16
Kutokana na madiwani wengi kuwa na uelewa mdogo wa mambo wizi na ubadhilifu unafanyika bila hata wao kujua nini cha kufanya hivyo ni vema wakawa na elimu ambayo inaweza kuwawezesha kutambua mambo kwa urahisi.
 
Wakati kuna wabunge darasa la saba mfano Aeshy Hilaly Halfan wa sumbawanga sasa kwa nini tusianzie ubunge kwanza
 
Mdau umuhimu wa kuanzia na madiwani ni mkubwa sana kwani katika halmashauri baraza la madiwani ndio wanaoandaa bajeti za halmashauri pia katika ripoti za CAG zimeonesha pesa zinaliwa/ibwa sana katika ngazi za halmashauri kutokana na umbumbumbu wa madiwani waliowengi,binafsi napendekeza madiwani wawe na certificate yoyote.
 
Kwa hiyo unaamnin Diwani akiwa na elimu isiyopungua kidato cha 4 atakuwa na uelewa mkubwa? Bado hujanishawishi.
 
Mi nadhani elimu itakuwa moja ya vigezo ananvyotakiwa kuwa amekidhi ili achaguliwe kuwa diwani na vigezo vingine but sio elimu tu mfano pamoja kuwa na elimu vilevile awe na uwezo wa kuisemea jamii kwa niaba ya maendeleo (my take elimu jambo la msingi katika ulimwengu wa sasa
 
right, elimu ni muhimu, sio diwani anaingia katika vikao hata uelewa wa taarifa zinazotolewa hakuna, taratibu za uendeshaji wa halmashauri hajui, nk pia wapewe orientation wanapoanza hata kama ana elimu ili kupata uelewa wa general issues
 
zamani ilitakiwa mtu ajue kusoma na kuandika na awe na umri wa miaka zaidi ya 18, nyakati zile wasomi hawakuwa wengi, sasa nadhani kiwango kipande, hii ya kusoma na kuandika imepitwa na wakati. Ndio maana zamani hizo kidato cha nne mtu alikuwa anapata ajira wakati sasa hata graduates wanachakaza viatu kuzunguka mtaani kuomba ajira
 
Back
Top Bottom