Madiwani wavunja mkutano kwa kukosa watu wa Television na Kamera

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 29th October 2011

MADIWANI wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, wameshindwa kufanya mikutano yao na waandishi wa habari kwa zaidi ya mara mbili kutokana na kutokuwepo kwa kamera za televisheni.

Kwa mara ya kwanza, madiwani hao waliomba kuzungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam, walifika na walipoona hakuna kamera za televisheni wakaahirisha.

"Hatuwezi kuzungumza bila kuona watu wa televisheni," alisikika akisema mmoja wa madiwani hao, kauli ambayo iliwakera baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo ukumbini humo.

Katika hatua nyingine, madiwani hao walipanga kuzungumza na waandishi wa habari kwa kile kilichoelezwa katika tangazo lao kwamba ni kuhusu matatizo ya kata ya Mkuranga, lakini wakazidi kuwaacha solemba waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa tangazo lao lililokuwa limebandikwa katika ubao wa matangazo wa Idara ya Habari, na kutiwa saini na aliyejitambulisha kuwa ni diwani wa kata ya Mkuranga Saidi kubenea, lilieleza kuwa yeye na madiwani wengine wangezungumza na waandishi wa habari saa nne
asubuhi juzi.

Jambo ambalo hawakulitekeleza.
 
Tujiulize kwanini TV;
  • waandishi wengine hawaaminiki?
  • madiwani hawa wanapenda kujionyesha live kwa watu?
  • Ni ulimbukeni tu walionao?
  • Hawakuwa na jambo la maana sa kulizungumzia ndiyo maana wakaona hata wakiacha haina taabu?
  • .....................
  • .....................
 
Back
Top Bottom